Kuna msemo mmoja hivi wa Paulo Coelho ni muhimu huyo mpenzi wako aujue. Huo msemo uko hivi;
"There are people who love us but don't know how to show it, and we understand their shyness as indifference"
"Kuna watu wanatupenda lakini hawajui namna bora ya kutuonesha mapenzi yao, na tunafikiri hawatujali kwa sababu ya aibu zao"
Mpenzi wako anatakiwa ajue kila mtu ana namna yake ya kupenda. Binadamu hatufanani kwenye mapenzi. Kinachomsumbua ni kukulinganisha wewe na wapenzi wake waliopita. Anafikiri jinsi alivyooneshwa mapenzi na wapenzi wake wa zamani ndio namna bora ya kupendwa bila kujua kuwa watu wako tofauti.
Unataka kujua cha kufanya? Usijali, mfanye ayajue haya niliyoandika.