Ushauri wenu wakuu nimefikwa

Ushauri wenu wakuu nimefikwa

B40

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
820
Reaction score
538
Habari wakuu
Kuna dada mmoja nilikuwa naishi nae kama mwaka bila kufunga ndoa Yale mapenzi ya sogea tuishi. Kwa bahati nzuri akapata mimba na kujifungua mtoto ingawa kiukweli mimi sikuwa na nia ya kuishi nae baada ya kuwa tabia zake ni za ovyo sana.

Siku moja nilikuta mazungumzo ya kurekodiwa ya kimapenzi kati yake na mwanaume ktk simu yake. Pia niliwahi kumsikia akiongea na hawara yake ktk simu.

Baada ya mambo kuwa hivyo nikaacha kila kitu na kuamua kupanga sehemu nyingine ila bado nahudumia kila kitu kuanzia chakula, nalipa kodi na mahitaji mengine ya mtoto. Ili mtoto asipate shida nimeajiri house girl baada ya yeye kuwa anazurura

Nina miaka 2 sasa sifanyi nae mapenzi na yeye huondoka na kurudi muda anaotaka. Siku nyingine mfano leo analala huko huko anarudi asubuhi.

Kinachoniuma ni mimi kumlipia kodi kumlisha na bado dharau hizi anazoonyesha. Anasema mtoto atamgawa na kumpa mwanaume mwingine na mimi sipendi mwanangu apate shida. Yeye hawezi tunza mtoto maana hata familia yao ni balaa tupu.

Wakuu nishaurini namna ya kumuokoa mtoto na mimi kuishi kwa furaha
 
Endelea kumtunza mwanao, au bado unamuonea wivu? Kama bado unampenda ukiondoa umalaya wake ishi nae tu, umalaya wao kwao labda ni sababu ya uzuri wao, acha wivu, hata wewe ni Malaya tu kwa vile umemuacha na kuchukua mwingine

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Habari wakuu
Kuna dada mmoja nilikuwa naishi nae kama mwaka bila kufunga ndoa Yale mapenzi ya sogea tuishi.
Kwa bahati nzuri akapata mimba Na kujifungua mtoto ingawa kiukweli mm sikuwa Na nia ya kuishi nae baada ya kuwa tabia zake ni za ovyo sana
Siku moja nilikuta mazungumzo ya kurekodiwa ya kimapenz kat yake Na mwanaume ktk cm yake
Pia niliwahi kumsikia akiongea Na hawara yake ktk simu
Baada ya mambo kuwa hivyo nikaacha kila kitu Na kuamua kupanga sehemu ingine
Ila bado nahudumia kila kitu kuanzia chakula nalipa kodi Na mahitaji mengine ya mtoto
Ili mtoto asipate shida nimeajiri house girl baada ya yeye kuwa anazurura
Nina miaka 2 sasa sifanyi nae mapenzi Na yeye huondoka Na kurudi muda anaotaka

Siku nyingine mfano Leo
analala hukohuko anarudi asubuhi

Kinachoniuma ni Mimi kumlipia kodi kumlisha Na bado dharau hiz anazoonyesha
Anasema mtoto atamgawa Na kumpa mwanaume mwingine Na Mimi sipendi mwanangu apate shida
Yeye hawez tunza mtoto maana hata familia yao ni Malaya tupu

Wakuu nishaurini namna ya kumuokoa mtoto Na Mimi kuishi kwa furaha

Sent from my M910 using JamiiForums mobile app
wewe uliekubali kuishi nae bila ndoa huku ukiyajua maadili tukuiteje?
 
"Maana hata familia yao ni Malaya tupu"


Inaelekea umemnyanyasa na kumzarau Sana sasa acha uvune ulichopanda na ujifunze ni mbaya sana kumtukana mwanamke na ukaihusisha na familia yake huku hujui shida alizopitia mpaka kukutana nawe.
 
Anaanzaje kumgawa mtoto ambaye wewe ndiye biological father?

Huduma zote unazotoa kwa ajili ya malezi ya mtoto bado haujiamini mkuu?

Mwisho ningependa kukushauri kama ni ugomvi ni kati yako wewe na huyo mzazi mwenzio familia yake haihusiki sio vizuri kusema familia yao wote malaya.

Ina maana baba yake ,mama yake ,bibi yake n.k wote hawajatulia na ikawaje ukaingia kwenye familia isiyo na maadili then ukakubali kugegeda bila kutumia kinga?

Lea mtoto mpaka atakapo jitambua umchukue mtoto wako hizo dharau zake wewe mpuuze tu.
 
Mkuu kwann usitoe kodi nusu halaf nayeye aongezee nusu maana mtt ni wenu...hamna sehem inayosema uhudumie kila kitu punguza matumizi akili itamkaa sawa
 
Endelea kumtunza mwanao, au bado unamuonea wivu? Kama bado unampenda ukiondoa umalaya wake ishi nae tu, umalaya wao kwao labda ni sababu ya uzuri wao, acha wivu, hata wewe ni Malaya tu kwa vile umemuacha na kuchukua mwingine

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Simuonei wivu ndio maana ninamuacha afanye atakavyo

Sent from my M910 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwani mbegu ilikua hiyo moja tuu....kama ulibaki na mbegu nyingine mwambie amgawe utanzalisha mwingine maana mpaka hapo waweza kuta hata mtoto sio wako wewe nikama mfadhili tu
 
Kwa nn usifanye mpango umchukue huyo mtoto umlee wewe au mtu wa kwenu ili umwache huru bisa kusumbuana naye?
Mkuu hataki kunipa mtoto anasema nikimuacha sina changu

Sent from my M910 using JamiiForums mobile app
 
Kama ana uwezo wa kumpa mwanaume mwengne mwanao means ana uwezo wa kukurudishia mwanao hata wewe,
Chukua dada wa kaz na mwanao watunze mwenyewe ila chonde chonde huyo house girl usje kumfanya mkeo tena.
 
Baadhi ya wavulana kama wewe ndo mnaotuangusha wanaume. Hizi ni siri za ndani. Kama wakati wa kuamua kuishi na hatimaye kuzaa naye hukutushirikisha ni vema na matokeo uyabebe mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: B40
Mchukue mwanao kama una mama ako akusaidie kulea, si lazima alee yeye,
Huyo ana poor mothering ability.

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Mama angu alifariki Rwanda genocide

Sent from my M910 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom