Mimi ni mkazi wa Kigamboni,km wiki 3 zilizopita kulitokea la uvunjaji nyumbani kwangu,na kuibiwa baadhi ya vitu,nilitoa taarifa kituo cha polisi Kigamboni.Kwa gharama zangu nilikodi gari kwa ajili ya kufanya msako kuwapata wahalifu wa tukio hilo.Tulibahatika kuwakamata watuhumiwa watatu(3)kati ya saba(7)siku hiyo, akiwemo mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 12-14 na yeye ndo 'master plan' sababu ndiye anayejichanganya na watoto kusoma mazingira sehemu wanayotaka kwenda kufanya tukio na ndiye anayetumika kupenya madirishani kabla ya kufungua milango.Huyu mtoto ndiye aliyetoa ushirikiano wa kupatikana hao watuhumiwa wengine,Siku ambayo tulipaswa kwenda mahakamani niliambiwa huyo mtoto yuko nje kwa dhamana pamoja na mtuhumiwa mwingine,na hawajahudhuria mahakamani kwa mara ya pili,na yeye naweza sema ndiye kichwa cha hii kesi(mtoto) sababu hawa wengine walikana kuhusika na tukio hili pale kituo cha polisi licha ya kutajwa na huyu mtoto,anayepandishwa mahakamani ni mtuhumiwa mmoja tu.Nilitaka kujua hapa kweli kuna kesi? Na kama ndiyo nini kifanyike? Naomba ushauri wenu wadau.Mana hawa vijana ni wasumbufu hapa kwenye kitongoji chetu na wana kawaida ya kulipiza kisasi wakirudi uraiani.