Habari zenu wanaJF
Lengo la uzi huu ni ukuomba msaada wa mawazo pamoja na ushauri wa hiki ninachofikilia kukifanya, maana naamini humu kuna watu tofauti.
Nadhani katika pitapita zenu mmekutana na wale vijana wauza aidha dawa za mswaki, Sabuni, vyombo huku wakiongea maneno yenye ushawishi sana kwa kuelezea kuwa wanatokea katika kampuni fulani.(biashara ya promosheni )
Nimekuwa na wazo hili zaidi ya mwaka mmoja ila sijui pa kuanzia mpaka kufungua kampuni ya namna hiyo ili niweze kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili tusaidiane maisha.
Naomba kujua pa kuanzia nikimanisha ni mamlaka zipi zinazohusika na hiyo biashara,
changaomoto zake na ushauri mwingne pia nitaupokea asanteni sana.
NB:mtaji si tatizo upo wa kutosha.
Kabla sijakushauri,labda nikuulize kitu..hicho unachotaka kukifanya/hiyo nia yako ya kufungua kampuni ya kuuza bidhaa mbalimbali ni kitu unachokipenda kwa dhati ya moyo wako??au umeona ufanye tuu kwasababu mtaji upo wa kutosha??