Ushauri wenu ni muhimu sana

Ushauri wenu ni muhimu sana

minzakunza

Senior Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
193
Reaction score
444
Habari wapendwa, nimekuja humu maalum kwa ajili ya kupata ushauri wenu ingawa sio mgeni kivile, mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 30 ni muajiriwa katika shirika moja la serikali hapa jijini Mwanza, nimewahi kuwa kwenye mahusiano mara moja ambayo mahusioano hayo yalikoma mwaka 2010 kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu mimi na mwenzangu tangia hapo sikuwahi kumpenda mtu yeyote kiufupi ni kama moyo wangu ulipatwa na ganzi kuhusu mapenzi mpaka hivi majuzi miezi kama miwili nilipotokea kumpenda kijana mmoja ambae alihamishiwa hapa kazini kwetu si kijana sana kwani amenizidi miaka kama 7 hivi na kikazi ni Boss wangu kwani naripoti kwake, mwanzo sikuwa nimefikiria kabisa kama ningempenda mpaka yeye mwenyewe alivyoonyesha interest za kuvutiwa na mimi moyoni nikahisi hata mimi amenivutia,siku moja akaniomba nimsindikize kupata chakula ilikuwa jioni kama sa 12 kwa sababu mchana alikuwa hajala ndipo akaanza kunieleza kwamba amenipenda sikumpa jibu la moja kwa moja kuwa hata mi nimempenda ingawa sikukataa pia cha kushangaza akaomba tukalale pamoja siku hiyohiyo kiukweli sikuweza kumkubalia na hii ni kutokana tumefahamiana nadhani ilikuwa ni wiki 2, baada ya hapo ilifuatiwa kama mara mbili kwa siku tofauti kumbushia swala la kwenda kulala kwake na mimi bado sikukubali nikiamini kwamba tutakaa tuongee kwa sababu sijui maisha yake ya mapenzi na hata yeye hajui maisha yangu ya mapenzi ingawa alinambia alishawahi kuoa ila waliachana na mkewe miaka 5 iliyopita na ana mtoto mmoja, baada ya hapo kama kweli anamaanisha tukapime then vingine viendelee lakini kabla hatujafika huko kwa wiki mbili sasa namuona amebadilika mawasiliano hakuna tena hata nikijitahidi nimtumie sms hajibu yaani kiufupi amebadilika mwanzo ilikuwa tukitoka kazini tunaweza tukaongozana tukaa sehemu kuongea mawili matatu sasa hamna tena anaondoka tu haniagi au anaweza asije asinambie yuko wapi tofauti na mwanzo hata akichelewa tu ananiambia kusema ukweli naumia sana moyo ni kipindi kifupi lakini nahisi sijawahi kupenda hivi yaani sielewi nifanye nini nimekuwa kama mgonjwa siwezi kula wa kulala ni wiki mbili tu sasa tangu aanze vituko hivyo lkn nimepungua uzito kwa kiwango kikubwa muda wote nimekuwa mnyonge maswali ya kama naumwa yamekuwa kawaida sana naona siku zinavyoendelea nitashindwa hata kufanya kazi naomba mnisaidie nifanyaje kuondokana na kadhia hii kiukweli hali ni mbaya sana kwangu yaani muda wote usiku na mchana yupo kwenye mind yangu ninaweza kupata usingizi masaa 2 tu usiku nikishtuka usingizi hauji tena mpaka asubui msaada wenu pls maana huko ninakoelekea nahisi nitachanganyikiwa kabisa, ninaweza nikachukua simu hivi nasema nampigia nimuulize lakini najikuta natetemeka mwili wote jasho linanitoka nashindwa kabisa
 
Mie nashauri hapo kwenye kutopata usingizi,
Tafuta dawa za usingizi kunywa usiku lala mpaka asubuh unaenda ofisini na kuwa busy na kazi futa mawasiliano nae yote yasiyolazima
 
Mfuate mwambie leo nakuja kulala kwako,atarudisha tena mapenzi kwani kwa sasa kasusa.
 
Pole aisaidii wew nenda kwa mganga wa kienyeji sawa ndo kiboko yao
 
Kwa nini suala la kupima limfanye abadilike? Labda yuko ++++ . Inabidi udhibiti hisia zako kwake uzishinde maana naona kama unelekea katika shimo.
 
Pole sana Dada angu nakushaur achana nae halafu ntafut mm kwan kisa chako kinafanana na changu.
 
dada kuwa makini huyo mtu afya yake sio nzuri umemwambia mkapime ndo maana akapotezea huyo hamna jingine
 
Kwa nini suala la kupima limfanye abadilike? Labda yuko ++++ . Inabidi udhibiti hisia zako kwake uzishinde maana naona kama unelekea katika shimo. Wanaume sio adimu kiasi cha kurisk namna hiyo.
 
2 options my Sister, give it up and hurt more, or stand your ground and hurt, but with dignity. Brotherman is only after the apple pie.

You should always avoid getting romantically involved with colleagues. Now you suffer even more, cuz y'all keep running into each other often. And it's affecting your career big time.
 
Punguza waka, mpe anachotaka. Ila muelezi asifosi sana. Mazuri hayataki haraka.
 
sitaki nataka....wanaume wa isku hizi hawatongozi mwanamke mwaka mzima. It is only twice. You take it or you leave it.
 
Achana nae huyo hakukupenda ila alikutamani maumivu unayojisikia kwa sasa ni mara kumi zaidi utakayosikia utakapo mpa mwili wako kabla hata ya kupima kwasababu kuna kitu anakuficha....;jaribu kujichanganya fanya mambo amabayo yatakufanya uwe busy
 
sitaki nataka....wanaume wa isku hizi hawatongozi mwanamke mwaka mzima. It is only twice. You take it or you leave it.

Ndio akatae kupima? Alishakubaliwa sasa alipoambiwa tu kupima HIV akapata kichaa.
 
Ndio akatae kupima? Alishakubaliwa sasa alipoambiwa tu kupima HIV akapata kichaa.

Did she expected a 37 years old man to be a virgin, and easy to go for HIV test. Ikiwa jamaa amempuuza kwa sababu ya HIV test...bibie anaumia moyo na lipi, haoni kuwa amesalimika na drama?
 
Kwanza hongera kwa kupunguza uzito magonjwa ya sukari si mazuri, alafu pia nakuomba sana ule muda wa usiku unaoamka kumuwaza jamaa utumie kumuomba Mungu upate swawabu za kuuona ufalme wa Mwenyezimungu. Usijipe stress dada yangu mapenzi yakigoma yaache fanya vtu vingine.
 
Tatizo ni High expectations to both of you,jamaa ya papuch kazira anaona unamzingua na wewe expectation kubwa ya kupata Ndoa.tafutia majibu ya haya na ni wewe pekee ndo unayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom