Aisee kaka/dada nakushkru sana hasa pale namba nne, mie nafanya biashara na aliyeniunganisha katika group hili namfahamu na ananifahamu, pointi kubwa ni kuwa kama mfanyabiashara tuna deal na bidhaa ambazo ni affordable kwa jamii inayokuzunguka. Kama bidhaa zina bei kubwa basi sio muda wa kupoteza kunadi bidhaa isiyouzikaUFAFANUZI.
1/Hiyo ni biashara ya mtandao(Sio mtandaoni) ambayo iko katika mfumo wa Pyramid, yaani kama upatu fulani(Wengi wanatumika kuwafaidisha wachache).
2/Ni biashara halali katika nchi yetu na mataifa mbalimbali duniani, kiufupi hakuna nafasi ya kirahisi ya kutapeliwa pesa zako kama ukikubali kujiunga(Taratibu zao ziko wazi kabisa).
3/Biashara hiyo haina tofauti yoyote ile kimfumo na Forever Living, Trevo nk. Utofauti upo kwenye bidhaa, mtaji wa kujiunga na Ukubwa wa faida.
4/Bidhaa zake ni bidhaa halisi, zenye ubora, Ghali zaidi na haziuziki kirahisi kwa mazingira ya Tanzania au watu wa kawaida au chini.(Unaweza ukakuta dawa ya mswaki(Meno) tube moja tu inauzwa shilingi Elfu 15, wakati Colgate ya ujazo huo huo inauzwa mtaani kwa shilingi Elfu 3)
5/Kufanikiwa katika biashara hiyo hapa Tanzania kwa sasa ni jambo la bahati nasibu sana. Kwa sababu faida kubwa haipo kwenye kuuza bidhaa zake bali ipo kwenye kutengeneza network follow up ya watu wengine watakaojiunga kwenye biashara hiyo nyuma yako. Huo ndio mtiti wake, ni issue nzito kushawishi watu wajiunge, sio jambo rahisi kwa watu kutoa mitaji yao ili wajiunge kupitia wewe.
6/Siku zote wahusika wa biashara hii watakuvutia kwa maneno mazuri ya kuonyesha Biashara hii ni rahisi kuifanya na itakuletea faida kubwa ya mamilioni tena kwa muda mfupi, na kamwe hawatakueleza upande wa Pili wa sarafu wa biashara hii kuhusu changamoto zake au hasara. Ni vizuri ukawa makini na mtafiti zaidi ili kujua kila kitu kabla ya kuamua kujiunga nayo.
Kwa leo nitaishia hapa.....
....mnakandafua...Wamejikita sana kwenye vipodozi na urembo. Mimi hapa member Oriflame pia na Trevo. Tatizo WanaJF nyinyi ni wagumu sana kufanya maamuzi. Kinatomaso sana nyinyi. Nimewatangazia humu ndani Trevo mkaishia kunitukana. Hamtaki kuielewa kiufasaha. Wengine humu ndani kazi hamna. Tunaleta Neema kwa wote mnakandafua. Sasa kwa taarifa sisi tunaendelea, mtakapozinduka ndipo utasema kwanini sikukata shauri tangu mwanzo saa hizi ningekuwa mbali. Uoga wako kuamua jambo ndio umaskini wako.
Hakuna kitu isipokuwa wamejiandaa vzr kutafuta masoko kwa kutumia lugha nzuri,ukweli anaefaidi ni mmoja tu tena kwa usawa huu na hizo bei zao utaishia kusoma namba kama ile ya nambari oneWamejikita sana kwenye vipodozi na urembo. Mimi hapa member Oriflame pia na Trevo. Tatizo WanaJF nyinyi ni wagumu sana kufanya maamuzi. Kinatomaso sana nyinyi. Nimewatangazia humu ndani Trevo mkaishia kunitukana. Hamtaki kuielewa kiufasaha. Wengine humu ndani kazi hamna. Tunaleta Neema kwa wote mnakandafua. Sasa kwa taarifa sisi tunaendelea, mtakapozinduka ndipo utasema kwanini sikukata shauri tangu mwanzo saa hizi ningekuwa mbali. Uoga wako kuamua jambo ndio umaskini wako.
Ahaa....sawa mi nikadhani ushalipia km zilivyo kampuni nyingineSi kwamba kupewa namba ya siri unakuwa umejiunga. Sijalipia chochote ninachotaka kufahamu hapa ni kwamba je hawa jamaa wapo nchini na mienendo yao ikoje. Kama wako na taratibu salama pamoja na huduma zuri basi tajiunga lkn kama hawaeleweki naachana nao. Sina nia mbaya na kampuni.
hebu nipe huo mchongo wa uber nione upoje upojeKaa mbali na hiyo business, infact kaa mbali na Network marketing business nyingi ambazo zinauza products... kama una gari nitafute nikushauri kuhusu Uber upate hela ya uhakika. its the only Online business yenye kichwa na miguu, zingine zote ukiingia utalia.. nilishafanya kazi na jamaa wanaitwa Organo Gold, pesa ilienda na hamna nilichoambulia... Njoo Uber kama una gari
Mkuu umenivunja mbavu moja ya kushotoHii ni sawa na MATAIRI ya gari, kazi kubwa na kupeleka body ya gari na waliokaa humo wafike wanapotaka. Tairi zitakabiliana na jua, mvua, miba, na kila aina ya vikazwo. Mwisho wa safari zimechakaa, zimepata moto, zimelika, yaani ziko taabani. Tafakari chukua hatua with this puzzle
Vipi mkuu mbilizi ulipaki, na je kuhusu kalandarugoKuwepo macho na hawa watu wanao tuona sisi kaa jalala la bidhaa zao, wapo akina Forever, Travo,GNLD na hao walio kufata hawa watu mmmmhhhh...... miaka mingi imepita kidogo nilipigiwa cm na hawa watumwa wa GNLD na kuanza kuniambia kuhusu bidhaa zao na semina zao, nikaenda kwenye semina zao mmmhhh.......... kuweni macho na utajiri wa kwenye makaratasi.... kigezo kikubwa wanachotumia eti ukiwa member utapata nafsi za kusafiri mara kwa mara kwenda kutembelea sehemu mbali mbali na kukutana na watu walio tajirika na hizo bidhaa..... sasa na mimi mwaka kesho naanza kupaki dawa aina ya MBILIZI naombeni member wa kuwauzia
Biashara yoyote ya Network Marketing kaa nayo mbaliiiii, narudia kaa nayo mbaliiii - Hakuna cha,
- AIM GLOBAL
- HELP HAND INTERNATIONAL
- GNLD
- TREVO
- AGRO INTERNATIONAL
- FOREVER LIVING
- ORIFLAME
NK
Hizo ni biashara ambazo zinawatajirisha waanzilishi tu tena wachache na kujitengenezea WATEJA wa kudumu na wa lazima wa bidhaa zao
- Biashara gani unaingiza watu hawafiki mwisho, Network Marketing ni biashara mbovu kuwahi kutokea duniani, kuna watu zimewafanya mazuzu mpaka mtu kama ameoa anaingiza mimba