Ushauri wangu wa bure tu kwa Mheshimiwa Rais Dr. JPM na Wasaidizi wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,882
Hilo Kosa naliona linajirudia mara kwa mara na pengine ama Yeye mwenyewe ( Mheshimiwa Rais ) au Wasaidizi wake ( Washauri ) wanadhani ni jambo jema ambalo litawaisidia ' Kisiasa ' zaidi ila kwa mtazamo wa ' Kiuwerevu ' zaidi halileti maana na sana sana linadhalilisha tu ' hadhi ' ya Urais na kuonekana ni ya Kiswahili Kiswahili sana.

Hoja yangu kama GENTAMYCINE ni ndogo sana kwamba siyo kila ' matukio ' lazima Mheshimiwa Rais wa JMT awepo. Binafsi yangu kuna ' matukio ' ambayo huwa hayana sana ' hadhi ' ya Rais kuwepo au kuhudhuria au kuyazindua lakini huwa namwona Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli akihudhuria.

Kwa maoni yangu naomba Wasaidizi wa Rais walibadili hili na badala yake Mheshimiwa Rais awe anatokea au anaonekana tu katika yale mambo ya msingi, nyeti na muhimu ya Kitaifa na haya ' matukio ' mengine amwachie Makamu wake au Waziri Mkuu.

Yawezekana kabisa kwamba sasa ameshazoeleka na kuonekana ni wa kawaida kwa Wananchi hatya wengine kumuona ni wa kawaida sana au ni mwenzao tu wa ' Kijiweni ' hivyo kupelekea kushusha heshima / hadhi yake katika Jamii.

Uzinduzi wa:

  1. Kiwanda cha Kibiriti na Njiti zake anakuwepo
  2. Uzinduzi wa dawa ya mbu na masalia yake anakuwepo
  3. Uzinduzi wa Tairi mpya za magari na zenye Pancha anakuwepo
  4. Uzinduzi wa Uwekaji Viraka na mchanga barabarani anakuwepo
  5. Uzinduzi wa Visima vya Maji yasiyo masafi anakuwepo
  6. Uzinduzi wa Watu kunywa Maziwa hata ya Popo anakuwepo
  7. Uzinduzi wa Watu kujua kunawa mikono wakitoka msalani anakuwepo
Hii haiwezekani na GENTAMYCINE naipinga kwa nguvu zangu zote. Mheshimiwa Rais akumbuke tu kwamba hata kama hatokuwa anatokea katika ' matukio ' ya Kijamii kama pengine ambavyo anapenda au waliokaribu nae wanamshauri lakini atambue kuwa hata kama Yeye hatokuwa anahudhuria na Watendaji wake wanamuwakilisha bado tu ' Sifa ' zitaenda Kwake, Chama chake na Serikali yake nzima.

Sifurahishwi na Kitendo cha Mheshimiwa Rais JPM kuhudhuria kila aina ya matukio kwani haitendei hadhi hadhi ya ' Presidency ' ambayo kokote pale duniani inatakiwa iheshimike na ikibidi hata ' Kuogopwa ' vile vile kwakuwa Yeye ndiyo wa mwisho Kimaamuzi.

Kuna nchi ambazo siku ukisikia tu Rais wao anazungumza au anatembelea mahala fulani jua ya kwamba kuna ' Kitu ' cha muhimu sana na Wananchi wote hukaa tayari kumsikiliza na hata kile ambacho ama atakisema au atakifanya kitapokelewa kwa umuhimu wake mkubwa tofauti na sasa nchini ambapo Mheshimiwa Rais ameshaonekana ni Mtu wa kawaida sana ndani ya macho na fikra za Watanzania wengi.

Nimeumbwa kusema ukweli, kutoa maono yangu na kamwe kutokuwa ' Mnafiki ' hivyo kama kuna ambaye nitamkwaza katika hili nililoliandika hapa ' mnisamehe ' ila nimelipima hili kwa marefu na mapana yake na kuona kuwa kuna ' tatizo ' mahala hivyo kama Mtu mwenye mapenzi mema na Rais wangu wa JMT Ndugu Dr. John Pombe Joseph Magufuli nimeona nilisemee na nitashukuru kama ' Wahusika ' watalifanyia ' tathmini ' kisha ushauri wangu ufanyiwe Kazi.

Nimemaliza yangu na moyoni na GENTAMYCINE nawatakieni nyote Wiki njema inayoanza leo.

Nawasilisha.
 
Sasa mukulu asipohudhuria kwenye ishu kama hizo wabongo si watamsahau kama yupo??

Maana maisha kitaa yamekuwa magumu balaa, kila mtu analia.
Angalau atokee tokee kwenye media na speech mbili tatu za kuwatuliza moyo wasimsahau.

Hapana Mkuu na haipashwi kuwa hivyo. Kama Wewe ni mpenda kufanya ' tafiti ' ndogo ndogo zisizo rasmi kidogo sasa hivi hadhi ya ' Presidency ' kwa Tanzania imeshuka na mpaka ameanza kuonekana ni kama tu Waziri. Yeye ni namba moja hivyo lazima aiweke juu hiyo hadhi yake ya kuwa namba moja katika nchi. Tunataka tukimwona ama yuko mahala au anahutubia sehemu fulani basi ' tusisimke ' na tuwe makini kumsikiliza ili hata yale ambayo ama atayafanya au atayasema yawe na matokea ' chanya ' ambayo yatapelekea kuzalisha ' Ufanisi ' wa Kiuwajibikaji na Kiutendaji kwa Watanzania wote. Hata hivyo Mkuu ni ' ushauri ' wangu tu Kwake na hao Wasaidizi wake ila siwalazimishi wauchukue japo hadi umeona GENTAMYCINE nimelileta hili jua jicho langu la mbali, la thamani na la kimaono limeona ' Kitu '.
 
Raisi inaenda kuwa rahisi

Kweli Mkuu sasa anaanza kuonekana ni wa kawaida mno na mwenzetu wa Kijiweni / Vijiweni. Ninavyojua ukiona Mtu anakushauri ni ' tafsiri ' tosha kuwa anakupenda na anakutakia mafanikio mema katika kile ukifanyacho maishani mwako au katika ' Utendaji ' wako halafu siyo ' Mnafiki ' Kwako vile vile. Naomba hili lifanyiwe sana Kazi ili Mheshimiwa asianze nae kuonekana ni Mswahili Mswahili au mpenda ' Promo ' za Magazeti na Social Media.
 
Ni kweli Gente, enzi zile ukisikia rais atakihutubia taifa lazima uwe na hamu ya kusikiliza nini kimetokea . Na mara nyingi unakuta kuna jambo kubwa la kufafanua au kuweka msimamo. Mh kawa very predictable. Watu wanakuwa wameshajua inavadvance nini ataongea kwa sababu hana jipya. Yupo kwenye majukwaa kila siku utafikiri bado yupo kwenye kampeni, hata ongea yake ni ya kikampeni kampeni. Kwa kweli hapa tumekula hasara!
 
Back
Top Bottom