USHAURI WANGU KWA WIZARA YA ELIMU ILI TUWE NA WAHITIMU MAHIRI.

ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,121
5,332
Kutokana na janga la vijana wengi kumaliza vyuo na kukaa nyumbani bila ya ajira wala uwezo wa kujiajiri, tatizo kila mdau anasema tatizo ni mfumo wetu wa elimu. Mimi pia nakubaliana nao.

Sasa basi, nimejaribu kuangalia kwani nchi nyingine wanafanyaje, kufupi kila nchi kuna tatizo la ajira, tunachotofautiana ni ujuzi walionao wahitimu.

Moja ya njia moja nzuri ya kupunguza tatizo ni serikali kupitia wizara ya elimu kuingia makubaliano na makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi, ili ziwe zinachukua wanafunzi vyuoni wakati wa likizo zao waende kufanya kazi za kujitolea kwenye taasisi hizo, hata kwa posho ndogo au bure iwe ni kama sehemu ya masomo yao ya hiari.

Kuwe na mfumo mzuri, mfano wanaosomea Dar basi wachukuliwe na taasisi zilizopo jirani na vyuo vyao ili kuepusha gharama za ziada.
Wanafunzi wakafanye kazi zilizo ndani ya field yao na zilizo nje kabisa ya field yao.
Mfano mwanafunzi wa sheria mwaka wa pili akaitwa kwenda kuwa mwalimu wa civics olevel,
Mwanafunzi wa udaktari, akaitwa kwenda kuwa nurse, kufanya usafi uwanja wa ndege, au kuwa dereva wa mwendokasi kama ana leseni.
Mwanafunzi wa Computer engineering, akaitwa kwenda kusimamia mashamba ya Mo Dewji, au kuswaga ng'ombe kwenye lunch za Bakhresa, nk.

Iwe hivyo ili mradi mwanafunzi asikae likizo bila kazi, labda awe na sababu, na isiwe ni lazima bali wawe na uhuru wa kukubali au kukataa kwenda, na kazi hizo zinakuwa zinaongeza CV ya mwanafunzi husika.
Pale tu likizo inapokalibia, basi tayari wadau wa kutoa hizo kazi wanakuwa na mawasiliano na chuo husika, ninatoa majina na wao wanachagua na kuwapangia kazi.

Huko kwenye hizo kazi, kama tayari zina watu, basi watu wao watakuwa ni kama supervisors wao kuwafundisha pale panapohitajika, au la basi watapewa likizo kazini ili kupisha wanafunzi wafanye kazi zao.

Hii itasaidia mwanafunzi anakuja kuhitimu akiwa na ujuzi wa vitu vingi kichwani, ndani na nje ya taaluma yake. Hii inaongeza ujasiri wa kupambana maana anajua anaweza kufanya kazi tofauti totauti.

Hebu wadau wa Jf, hii haiwezi kuwa msaada kwa vijana wasomi nchi hii??
Najua wahusika toka wizara mbalimbali huwa mnapita Jf, basi chukueni hata na hii iwe msaada kwa taifa.
 
Safi Sana Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo Oyo
tapatalk_1544879002398.gif
 
Hili ni wazo zuri sana ila pia huko vyuoni tupunguze tan ta lila yaani practical zitawale zaidi pia wahadhiri wetu wajifunze techs mpya wasikae bar na kujisifia tu
 
Back
Top Bottom