Ushauri wangu kwa viongozi wa upinzani nchini

Sdm

Member
Dec 11, 2017
40
70
Habari zenu na pia poleni kwa majukumu mnayoyafanya katika suala zima la ujenzi wa nchi.. Mimi nina ushauri kwenu nikiamini kama hamtasoma huu ushauri basi kuna watu walio karibu yenu watasoma na kuwapa huu ushauri..

Kwanza kabisa nianze kuwapa pole kwa yale yanayotokea.. Mimi kama mtanzania naumia pia.. Ushauri wangu ambao nataka kuwapa ni kwamba watanzania wengi wanapenda kuona vitu vinavyoongelewa basi wavione kwa macho haraka vikifanyika.. Kwa hiyo vyama vya upinzani muwe makini kuangalia hivo vitu na kuihoji serikali moja kwa moja... Anzeni na vitu vidogo hapo mtawakuna watanzania...

Badala ya kupigana kwa vitu vikubwa mpaka viongozi wanaumizwa.. Nyie angalie vitu vidogo ambavyo direct vinawagusa wananchi... Kwa mfano.. Mnaweza kuamua kuihoji serikali juu ya mambo haya madogo na mkakuna mioyo ya watanzania wengi..

1 Mkaiuliza serikali nini hatima ya wasomi wanaoendelea kurundikana mtaani bila ajira na serikali inaendelea kupeleka wanafunzi vyuoni..? Serikali ijibu.. Na ikikataa kujibu mnailetea vamshi kwa suala hilo tu mpaka itoe majibu..

2..serikali imeacha wanafunzi waendelee kusoma masomo ya sanaa shuleni wakati hayana maana tena hapa nchini kwa saivi.. Kwa nini isifute maana hayana maana kwa mujibu wa serikali maana waliosoma masomo hayo hawaajiriwi.. Mkipigana kwa hilo bado watu watakunwa sana na hilo jambo na kuzidi kuwapenda..

3..Msitumie nguvu kupambana na serikali kwani nayo inajiona ina mkono mpana.. Kwa hiyo tumieni akili sana.. Waulizeni maswali kupitia vyombo vya habari na wao wajibu... Wakishindwa wananchi tutajua ipi ni kweli..

4..Angalieni vitu vidogo ambavyo taifa linaona ni vidogo lakini vyenye maslahi kwa watu wengi...

5..Siku ile hamkupewa fomu za viapo.. Mngeiuliza serikali kwa lugha laini kwa nini hamkupewa na wao wangetoa majibu.. Tungepata sababu zao kwa nini walibana fomu. Yaani muwe watu wa kuihoji serikali live kupitia vyombo vya habari na yenyewe itoe majibu...

6. Viongozi wa serikali wanazunguka humu na kwingine wanawaambia watumishi wanaoidai madeni toka zamani kwamba mwezi ujao watalipa lakini hawalipi mpaka miezi inapita... Mngechukua reference ya sehemu moja na kuihoji serikali wangapi wamelipwa na hao waliobaki wanangoja nini kuwalipa.. Hilo mngewakuna sana wasiolipwaa...

7..Kuna matatizo mengi yanawakuta wananchi lakini hakuna pa kusemea... Nyie ndo watu wa kusema... Msipigane tu kukaa madarakani mkigusa majeraha madogomadogo ya wananchi yale ya jumla kwa nchi nzima... Mtashinda..

Msitumie nguvu nyingi kupambana.. Kuweni wapole lakini kila siku muihoji serikali kupitia vyombo vya habari kuhusu matatizo ya wananchi bado mambo yatakuwa sawa tu ingawa mumefungiwa mikutano ya hadhara..

Ukizungumza jambo linalowagusa wengi kwa amani na vyombo vya habari vikaliandika au kutangaza basi utakuwa umewafikia watu wengi kuliko hata mkutano wa hadhara na kikao cha ndani..

Cha msingi ni kuongea mambo ambayo hayataamsha hasira na kuonekana ya kichochezi..raha ya watu tunataka kusikia "Mbowe aihoji serikali kuhusu kitu fulani ilichosema itafanya kipo wapi........? Na serikali ijibu kipo uvunguni mwa kitanda... Siyo vurugu...
 
Back
Top Bottom