Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,494
- 1,874
Nawashauri vijana wote 854 waandike barua rasmi kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan na nyingine kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo; waombe msamaha na kujutia makosa yao au uasi wao. Waahidi kuwa raia wema na ikiwapendeza Rais na Mkuu wa Majeshi wawasamehe na kuwarudisha jeshini.
Kwa upande mwingine, na kwa heshima na unyenyekevu mkubwa; nitoe ombi rasmi kwa Rais wangu na dada yangu Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Majeshi na kaka yangu Venance Mabeyo, wawaone vijana hao kuwa ni watoto wao. Wamekosea sana kwa taifa na kwao wenyewe, lakini Rais na Mkuu wa Majeshi nawajua sana kuwa pia ni wazazi na walezi wenye huruma, wapole na waungwana kwa watoto wanapotubu makosa yao na kujirudi.
Aidha, huku mitaani kumejaa vijana wengi wasio na ajira na wamechanganyikiwa, hawajui la kufanya, hawana mitaji, wengine hawana hata ndugu wa kuwasaidia na wamekosa ubunifu. Wamekata tamaa!
Tusiwaongeze wengine waliokata tamaa mitaani, tena wanaojua kutumia silaha za moto. Vijana waliokata tamaa wako tayari kufanya lolote maana hawana cha kupoteza zaidi ya kutuachia uchungu na madhara pindi wafanyapo uhalifu.
Wengine husema ni mabomu yanayotembea. Naomba sana, tena sana; tuwasamehe, tuwafunde na kuwapatia ajira ili wasiwe mabomu yanayotembea yanayoweza kulipuka wakati wowote!