Ushauri wangu kwa Ungozi wa CHADEMA!!

Ushauri wangu kwa Ungozi wa CHADEMA!!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Ni ukweli usiopingika kwamba sasa Jiji la Arusha ni Kioo na Ngome kuu ya CHADEMA kwa siasa za Tanzania.
Baada ya mlipuko wa bomu kutokea ktk mkutano wa hitimisho la kampeni za CHADEMA ktk viwanja vya Soweto tar 15/06/2013,na kupoteza maisha ya watu 4 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa na risasi zilizokua zikirushwa na polisi hali iliyofanya kuahirishwa kwa mkutano huo hadi juzi tar 14 takriban mwezi mmoja sasa tangia kutokea kwa tukio hilo,hatimae CHADEMA kimeshinda uchaguzi huo kwa kuchukua kata zote 4.

Kwa wale wanaofuatilia siku ambayo Viongozi na Wafuasi wa CHADEMA walipotawanywa kwa Mabomu ya machozi na polisi wakati wakiwa wamejikusanya ktk viwanja vya Soweto kuwaaga Marehemu wa mlipuko wa bomu,viongozi wa CHADEMA wakiwemo waliokua Wagombea udiwani wa Kimandolu na Themi pamoja na wabunge SAID ARFI, MUSTAFA AKUNAY, TUNDU LISSU na LUCIY MUKIA walila rumande.

Baada ya matukio hayo yote ya kukatisha tamaa,hatimae wana Arusha hususan wafuasi na wapenzi wa CDM juzi waliwafuta machozi na kuwapa matumani wale wote waliokua wameumia na waliokua wamekata tamaa kwamba basi sasa CDM wanaenda kushindwa uchaguzi huo kwa sababu ya Propaganda na mbinu zote chafu na za hila dhidi ya CHADEMA zilizokua zikiendeshwa na Wafuasi wa Lowassa,Mwigulu Mchumba,na Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo kuhakikisha kwamba Cdm haishindi.

Ombi langu ni kua baada ya Ushindi huu ambao sio ushindi wa wana Arusha pekee bali ni kwa Tanzania nzima na Wapenda haki kote nchini,basi Uongozi wa Chama taifa ifanye yafuatayo.
1; Kufanya mkutano wa wananchi ktk jiji la Arusha kwa kuwashukuru wale wote walioonyesha upenzi na Uvumilivu kwa kuwachagua madiwani wa CDM ktk Mazingira magumu.

2.;Mkutano huo uhudhuriwe na Wabunge wote na viongozi wa juu wa Chama kama sehemu ya ule wa kuwaaga Marehemu wa mlipuko wa bomu ambao kwa makusudi kabisa polisi walikataza kwa kisingizio cha AICC kukataa uwanja wao kutumika. Mtu kama Saidi Arfi hakuwahi kuhutubia mkutano Jijini Arusha hivyo tunapenda sana kumsikia Kamanda huyu na wengine.

3; Mwisho tunaomba uwongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha kufanya uchunguzi kuhusu watu ambao siku ile iliyokua ya kuwaaga Marehemu wale baada ya polisi kuwatawanya watu na kukimbia wengi wa vijana waliacha pikipiki 106 uwanjani na kwa waliokua wakishuhudia Askari polisi ambao wengi wao walikua ni wanafunzi kutoka CCP MOSHI,walifanya uharibifu mbaya sana kwa zile pikipiki na magari likiwemo langu kwa kuvunja vunja taa na kuchana matairi. Vijana wengi sina uhakika km wamesharudishiwa pikipiki zao hadi sasa kutokana na kua zilipakiwa ktk lori la polisi km uchafu na kwenda kumwagwa kituo cha kati.

Itapendeza sana km Chama kitawakumbuka vijana hawa wafia Chama kwa kuwapa angalao kifuta machozi na km inawezekana kuna ambae bado hajapewa pikipiki yake basi asaidiwe ijulikane kwanini hakupewa. Hii itafanya vijana wengi kuendelea kuwa na Moyo wa kujitolea bila kuogopa.Nilisikia kwamba lengo la polisi kuharibu pikipiki na magari ya wafuasi wa CDM ni ili kuhakikisha kwamba siku zijazo vijana hawatakubali tena kushiriki ktk mikutano na maandamano ya CDM kwa hofu ya kukamatiwa na kuharibiwa magari na pikipiki zao. Lakini hata baada ya tukio hilo bado siku ya Mazishi ya Mama yule Kiongozi wa CDM Judith vijana wa boda boda zaidi ya 300 walishiriki ktk msafara wa kuelekea nyumbani kwa marehemu.

Naomba uongozi wa CDM ikiwezekana haya yafanyiwe kazi kwa manufaa ya Chama.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 
Ni ushauri mzuri sana kwa lengo la kufarijiana na kupeana moyo bila kutokukata tamaa katika kuleta mabadiliko chanya ya kisiasa nchini.Naamini ushauri wako utafanyiwa kazi!
 
dah,huu ni moja kati ya ushauri mzuri kuwahi kutokea nadhan viongozi wetu watalitazama hili kwa mapana zaidi na kulifanyia kazi.pole kwa kuharibiwa gari lako mpiganaji mwenzetu
 
Nipo tayari kuchangia uharibufu wowote uliotokea juu ya magari na pikipiki endapo itathibitika -- tupo pamoja makamanda -- Arusha imetoa mwanga mikoa mingine inafuata -- Aluta....
 
good advice,hili ni swala nyet sana hasa ukizngatia vijana wengi ndio makamanda na wapambanaji hi italeta hamasa na moral kwa wote walioharbiwa mali zao na hata wale ambao bdo ni waoga kujitokeza ktk mikutano yetu.
 
Ni wazi kabisa Kamanda Lema pamoja na cdm wanao wapenzi wengi sana Arusha . Ushauri wangu kwa Kamanda Lema .uchaguzi umeisha. Sasa kinachotakiwa ni maendeleo. Kwa kuanzia tunakushauri uwahamasishe vijana ili ipangwe siku moja kila mwezi kwa kuweka mazingira ya mji wetu kuwa masafi iwe ni pamoja na kuotesha miti kandokando ya barabara, maeneo ya kuzunguka mashule na sehemu nyingine itakayo onekana. Mitaro mingi imeziba kwa uchafu, nina imani kutokana na ushawishi mkubwa ulio nao kwa watu hili kwako linawezekana. Na nia ni kuwaonesha hawa wachumia tumbo kuwa tunaweza. Wanachukua fedha kila mlango wa duka kwa kila mwezi lakini wameshindwa kuweka mazingira ya mji wetu kuwa safi. Nina imani kubwa kwa Kamanda kuna mambo mengi sana ya kuyafanyia kazi kwa mfano kuna kibanda kilijengwa eneo la soko mjinga ungaltd eti ni kwa ajili ya soko na tunasikia kimegharimu mamilioni ya shilingi ni zaidi ya miaka 4 kimekaa tuu
Hakika tukijipanga tutawasuta
 
Ni ukweli usiopingika kwamba sasa Jiji la Arusha ni Kioo na Ngome kuu ya CDM kwa siasa za Tanzania.
Baada ya mlipuko wa bomu kutokea ktk mkutano wa hitimisho la kampeni za Chadema ktk viwanja vya Soweto tar 15/06/2013,na kupoteza maisha ya watu 4 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa na risasi zilizokua zikirushwa na polisi hali iliyofanya kuahirishwa kwa mkutano huo hadi juzi tar 14 takriban mwezi mmoja sasa tangia kutokea kwa tukio hilo,hatimae CDM kimeshinda uchaguzi huo kwa kuchukua kata zote 4.

Kwa wale wanaofuatilia siku ambayo Viongozi na Wafuasi wa CDM walipotawanywa kwa Mabomu ya machozi na polisi wakati wakiwa wamejikusanya ktk viwanja vya Soweto kuwaaga Marehemu wa mlipuko wa bomu,viongozi wa CDM wakiwemo waliokua Wagombea udiwani wa Kimandolu na Themi pamoja na wabunge SAID ARFI, MUSTAFA AKUNAY, TUNDU LISSU na LUCIY MUKIA walila rumande.

Baada ya matukio hayo yote ya kukatisha tamaa,hatimae wana Arusha hususan wafuasi na wapenzi wa CDM juzi waliwafuta machozi na kuwapa matumani wale wote waliokua wameumia na waliokua wamekata tamaa kwamba basi sasa CDM wanaenda kushindwa uchaguzi huo kwa sababu ya Propaganda na mbinu zote chafu na za hila dhidi ya CDM zilizokua zikiendeshwa na Wafuasi wa Lowassa,Mwigulu Mchumba,na Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo kuhakikisha kwamba Cdm haishindi.

Ombi langu ni kua baada ya Ushindi huu ambao sio ushindi wa wana Arusha pekee bali ni kwa Tanzania nzima na Wapenda haki kote nchini,basi Uongozi wa Chama taifa ifanye yafuatayo.
1; Kufanya mkutano wa wananchi ktk jiji la Arusha kwa kuwashukuru wale wote walioonyesha upenzi na Uvumilivu kwa kuwachagua madiwani wa CDM ktk Mazingira magumu.

2.;Mkutano huo uhudhuriwe na Wabunge wote na viongozi wa juu wa Chama kama sehemu ya ule wa kuwaaga Marehemu wa mlipuko wa bomu ambao kwa makusudi kabisa polisi walikataza kwa kisingizio cha AICC kukataa uwanja wao kutumika. Mtu kama Saidi Arfi hakuwahi kuhutubia mkutano Jijini Arusha hivyo tunapenda sana kumsikia Kamanda huyu na wengine.

3; Mwisho tunaomba uwongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha kufanya uchunguzi kuhusu watu ambao siku ile iliyokua ya kuwaaga Marehemu wale baada ya polisi kuwatawanya watu na kukimbia wengi wa vijana waliacha pikipiki 106 uwanjani na kwa waliokua wakishuhudia Askari polisi ambao wengi wao walikua ni wanafunzi kutoka CCP MOSHI,walifanya uharibifu mbaya sana kwa zile pikipiki na magari likiwemo langu kwa kuvunja vunja taa na kuchana matairi. Vijana wengi sina uhakika km wamesharudishiwa pikipiki zao hadi sasa kutokana na kua zilipakiwa ktk lori la polisi km uchafu na kwenda kumwagwa kituo cha kati.

Itapendeza sana km Chama kitawakumbuka vijana hawa wafia Chama kwa kuwapa angalao kifuta machozi na km inawezekana kuna ambae bado hajapewa pikipiki yake basi asaidiwe ijulikane kwanini hakupewa. Hii itafanya vijana wengi kuendelea kuwa na Moyo wa kujitolea bila kuogopa.Nilisikia kwamba lengo la polisi kuharibu pikipiki na magari ya wafuasi wa CDM ni ili kuhakikisha kwamba siku zijazo vijana hawatakubali tena kushiriki ktk mikutano na maandamano ya CDM kwa hofu ya kukamatiwa na kuharibiwa magari na pikipiki zao. Lakini hata baada ya tukio hilo bado siku ya Mazishi ya Mama yule Kiongozi wa CDM Judith vijana wa boda boda zaidi ya 300 walishiriki ktk msafara wa kuelekea nyumbani kwa marehemu.

Naomba uongozi wa CDM ikiwezekana haya yafanyiwe kazi kwa manufaa ya Chama.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!

Nafikiri ianzishwe M4C kwa ajili ya kuchangia vijana hawa wapate pikipiki zao,lakini pia nafikiri kuwe na M4C kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika makundi kupata pikipiki kwa ajili ya vikundi vya kujiendeleza na kupata mitaji hii ikiwa kila sehemu M4C inakopita basi fedha zinazopatikana zianzishe makundi ya vijana kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
 
Mkuu sokoinei ulichosema ni sahihi kabisa. Ni changamoto inayokikabili chama chetu kwa sasa hasa kwa watu wetu wanaojitolea kwa ajili ya ushindi wetu bila kujali madhara watakayopata.
 
Last edited by a moderator:

Nafikiri ianzishwe M4C kwa ajili ya kuchangia vijana hawa wapate pikipiki zao,lakini pia nafikiri kuwe na M4C kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika makundi kupata pikipiki kwa ajili ya vikundi vya kujiendeleza na kupata mitaji hii ikiwa kila sehemu M4C inakopita bafedha zinazopatikana zianzishe makundi ya vijana kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.

Nipo tayari kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwakutumia mitaji midogo. Hii imekuwa ndoto yangu kwa miaka mingi ami baiona inavyoanza kukamilika. Nawashukuru CDM angalau kunipa green light namwomba Mungu vizuizi hivi kidogo vinavyonichelewesha ku proceed kwa haraka viondoke.
 
Naunga mkono hoja si kwa ushabiki bali kwa nguvu ya hoja yako.Naamini Makene na Dr Slaa huwa wapo humu jamvini kila mara kufuatilia mijadala basi wa note hizi hoja na kuzifanyia kazi.Kuna somo kubwa sana limepita ndani ya darasa la tarehe 14.7.2013 kwa "wanafunzi " tuliopo nje ya Arusha.Mhadhiri wa somo la Jumapili hakika hakuacha hata chembe ya wasiwasi na hakuna mwanafunzi amabaye alidiriki kuuliza swali la nyongeza.Kazi kwetu kusoma sasa na siku ya Final Exam wote tufaulu pasiwe na mtu kupata supplementary isiyo na mkia wala miguu.Asante sana wana Arusha na Mhadhiri wenu.
 
kweli kabisa mkuu ,kupeana moyo na kusaidiana ndiyo jadi yetu watanzania.... tusiwasahau wahanga waliojeruhiwa na bomu na familia za wahanga wa mabomu , ikiwezekana itengenezwe namba ya simu itangazwe Tanzania nzima tushiriki kuchangia wenzetu waliokumbwa na huo udhalimu , itasaidia kuimarisha umoja.
 
maneno yote hayo kumbe lengo ni kufidiwa kioo cha gari yako!? mmmmmmhhhh!
 
hakuna mkutano unaoruhusiwa arusha kwa sasa. hali bado tete. futeni mpango wa mkutano. kibali hakuna. by polisi
 
Ushauri wako ni mzuri sana,binafsi nipo tayari kuchangia katika hili.
Kama itafaa,bakuli litembezwe na huku mikoani tuko tayari.
 
....
3; Mwisho tunaomba uwongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha kufanya uchunguzi kuhusu watu ambao siku ile iliyokua ya kuwaaga Marehemu wale baada ya polisi kuwatawanya watu na kukimbia wengi wa vijana waliacha pikipiki 106 uwanjani na kwa waliokua wakishuhudia Askari polisi ambao wengi wao walikua ni wanafunzi kutoka CCP MOSHI,walifanya uharibifu mbaya sana kwa zile pikipiki na magari likiwemo langu kwa kuvunja vunja taa na kuchana matairi. Vijana wengi sina uhakika km wamesharudishiwa pikipiki zao hadi sasa kutokana na kua zilipakiwa ktk lori la polisi km uchafu na kwenda kumwagwa kituo cha kati.....
Kama ni kweli polisi walifanya huu uharibifu, basi nashawishika kwamba hawakuwa ni polisi wa kawaida.
 
bakuli litatembezwa mara ngapi, maana CHADEMA vurugu ndiyo sera ya chama.
 
maneno yote hayo kumbe lengo ni kufidiwa kioo cha gari yako!? mmmmmmhhhh!

Wewe una MTINDII wa Ubongo! Na kama huna basi una MAKENGEZA hadi huko kwenye O yako!! Wapi umeona nimeandika nataka fidia ya kioo cha gari langu!?

Au umetumwa kunitafutia Ban nini? Nilichosema nikuhusu madreva wa bodaboda kwa kua najua wengi wao 90% pikipiki sio mali zao bali wao ni Madreva na wengi watakua wamenyanganywa baada ya tukio lile.

Wewe inakuhusu nini hata km ningekua nataka ninunuliwe kioo? Nyie ndie wale Vihere here Mwenzako anakazwa kule wewe unakatika huku! Badala usubiri zamu yako ya kukazwa! Shwaini na GAMBA mkubwa.
 
Back
Top Bottom