Pindi muwapo katika mahusiano, nafahamu mnafanya kila kitu kwa sababu ya kuakikisha mnalinda penzi lenu kwa wapenzi wenu na pengine hata kuhatarisha hali za afya zenu
Wengi wenu inafikia kipindi kukubali kufanya tendo la ndoa pasipo matumizi ya Condom. Kuna msemo usemao nyama kwa nyama inafurahisha zaidi kuliko pipi kwenye ganda Lake ila afya yako ni muhimu sana kuliko nyama kwa nyama. Ili kutunza penzi mnakubali ombi la mwanaume then baada ya tendo mnaanza na kupata masumbuko
Pindi period ikichelewa, mawazo yanaanza, mnajiangalia kwenye kioo kama kuna mabadiliko ya mwili, kununua kipima mimba, uwajibikaji ofisini unapungua mpaka hapo mzunguko ukionekana kisha mnapumua.
Kwa upande wa mwanaume yeye anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kisha anakupigia simu kukuuliza lini utaenda tena kumtembelea amekumiss.
Dada zangu, je upo kwenye hiyo hali?
Au unamjua mtu yeyote aliyo na hali hiyo?
Kwa wanaume wenzangu unafanya hilo kwa mpenzi wako? Kama ndio stop