Author
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 1,709
- 8,007
Niende moja kwa moja kwenye mada,
Tumeona kero kubwa sana kwa Wananchi wakati wa ufuatiliaji wa namba za utambulisho kwa ajili ya kupata vitambulisho cha taifa.
Foleni ndefu sana na NIDA wanasuasua sana kwenye kukamilisha zoezi hili kama walivyoplan. Huku msukumo mkubwa ukiwa kwa wananchi kupata vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za Vidole (mwisho ikiwa Desemba 31, 2019).
Wapo wananchi wengi walioamua na wanasema "liwalo na liwe. Wafunge tu hizo laini tutatumia simu zetu kwa matumizi ya tochi, kusikiliza nyimbo na Radio". Kiuhalisia NIDA wameshindwa kukamilisha zoezi hili.
Na hili linathibitishwa mambo kadhaa ambayo wananchi tunayatumia kama ushahidi
1. Namba ya kutumia kupata namba ya utaambulisho (kwa kutumia simu) kutofanya kazi na kutokuwa na uwezo wa kuwapatia wananchi namba za utambulisho.
2. Website ya NIDA kutokufanya kazi
3. Foleni ndefu zisizopungua kila siku kwenye vituo vya NIDA na muda mrefu unaotumika mpaka mwananchi kupata kitambulisho.
4. Wananchi wachache kuwa wamepata vitambulisho mpaka Desemba, 2019 (tofauti na waliopata wakiwa vyuoni)
5. NIDA kuwa inatoa taratibu mpya kwa wananchi kupata namba ya utambulisho tofauti na mpango walioanza nao.
MAPENDEKEZO KWA SERIKALI
1. NIDA na NEC (Tume ya taifa ya uchaguzi) ziunganishwe kukamilisha zoezi hili; Ubora wa vitambulisho vya taifa na vya kupigia kura ni ule ule tena zaidi cha taifa kina taarifa nyingi zaidi za raia kuliko cha kupigia kura.
2. Vitambulisho vya taifa vitumike wakati wa kupiga kura; Kupata kitambulisho cha taifa sharti mojawapo uwe 18+ (kigezo pia kwa kupiga kura). Raia asajiliwe kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwa kutumia kitambulisho chake cha taifa.Hii itapuguza gharama za kutengeneza vitambulisho na muda wa wananchi kupanga foleni tena kwa ajili ya kupata kadi za kupigia kura.
3. Muda wa kusajili laini kwa alama za vidole uongezwe kuendana na ukamilishaji wa zoezi hili. Serikali iombe tathmini kutoka kwenye makampuni ya simu na NIDA kufahamu Watanzania wangapi wameshapata vitambulisho ili kufahamu ni kwa muda gani zoezi hili litakamilika. Ni vyema ofisi husika kufahamu inaweza kuhudumia watu wangapi kikamilifu kwa siku.
Wadau mnaweza kuongeza mawazo yenu kwenye mada hii.
Nawasilisha.