Ushauri wangu kwa serikali juu ya migomo ya wafanyabiashara

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Kumekuwa na tabia ambayo imezuka na inazidi kukua kwa kasi hasa juu ya muungano wa wafanyabiashara linapokuja suala linalogusa maslahi yao. Suala la muungano ni jambo jema ila muungano usiokuwa na maslahi kwa wananchi na nchi kwa ujumla huku ukiwaumiza wananchi kwangu mimi ni upuuzi.

Toka serikali itoe agizo la kuwataka wafanyabiashara kutumia mashine za electronic (EFD) pale wanapouza bidhaa zao ikiwa ni sambamba na wanunuaji kudai risiti hizo pale wanaponunua bidhaa hizo, kumekuwa na sintofahamu juu ya wafanya biashara. Wengi wao wamekuwa wakilalamika kuwa suala la EFD kwao ni gumu kwasababu ya zinapatika kwa bei kubwa ambayo hawawei kuimudu lakini pia wakidai kuwa zinakuwa na matatizo kwenye utumiaji wake.

TRA nao wamekuwa wakidai matumizi ya mashine hizi ni jambo zuri kwasababu kwanza zinamsaidia muuzaji kuwa na kumbukumbu ya mauzo yake na hivyo kumrahisishia yeye na TRA wakati wa kulipa kodi ili kuepukana na suala la kukadiria ambalo ama umpunja mfanyabiashara au TRA. Mambo yote hayo yametolewa ufafanuzi na TRA, ambao binafsi kama raia wa kawaida nisiyeegemea upande wowote nimeridhika na na hoja na majibu toka pande zote.

Lakini kuna kitu kingine nimejifunza toka kwa wafanyabiashara ambacho hicho hawakisemi bayana, kwamba hawataki kulipa kodi husika kwa mauzo wanayoyafanya, hii ni kutokana na mashine hizo kutuma taarifa moja kwa moja TRA pindi wanapofanya mauzo kwa kutua risiti za EFD.

Nilifikiri wangezichangamkia ili sasa wasiwe wanawalalamikia TRA hasa linapokuja suala la ukadiriaji wa kiasi gani kilipwe kama kodi, jambo la kushangaza ni kwamba kumbe wao walikuwa wanatumia mfumo huo wa ukadiriaji kama loophole ya wao kukwepa kodi. Mathalani anatakiwa alipe kodi milioni 30 kwa serikali.

Yeye anaomba atathiminiwe kulipa labda milioni 15 huku akimplia mtathimini milioni 5 kama takrima ambapo jumla anakuwa amelipa milioni 20 na huku akiwa ameokoa milioni 10 ambayo ingeweza kukusanywa na serikali.

Kitendo hiki cha kutaka kupata faida maradufu bila kutaka kulipa kodi bado wanaendelea nacho hata sasa kwa hao wenye hizo mashine. Mathalani utakuta mtu ananunua vifaa vya milioni moja ila ikitokea akapewa risiti ya EFD basi mwenye duka umwomba mteja wake aandike kiasi pungufu ya hicho mathahali ataandika shilingi laki 3.

Kwa kufanya hivyo tayari ameikosesha serikali mapato na wakati huo huo mnunuzi hajapata faida yoyote kwenye punguzo hilo maana yeye kalipa malipo yanayojumuisha na malipo ya kodi kwa bidhaa alizonunua.

Na ni sisi wananchi pia tunalalamika pale viongozi wanapobeba bakuli na kwenda kuomba omba misaada nje. Binafsi sipendezwi na hilo. Nyerere tunayependa kumnukuu kila mara aliwahi kutamka bayana kuwa "hakuna nchi inaweza kuendea bila kukusanya kodi" Na njia pekee ya serikali kujitegemea ni kuhakikisha inakusanya kodi toka kwa wananchi wake kwa vyanzo mbalimbali. Na hapa simaanishi kuwabana tu ili mradi wanakusanya kodi.

Muungano huu wa kugoma kufungua maduka kisa kesi ya mwenyekiti wao ifutwe ni mwendelezo wa muungano ule ule ninaouita ni muungano wa kipuuzi kwasababu hauna maslahi kwa taifa ila kwa kundi la wafanya biashara na huku ikiwaumiza wananchi.

Kwamba serikali ifikie hatua iwaache waendelee na mfumo wao wa zamani wa kuandika vijirisiti ambayo mwisho wa siku ni ngumu kujua kiasi halali cha mauzo alichofanya.

Ushauri wangu kwa serikali
  • Serikali iendelee na mpango wake wa kuwataka wafanyabiashara wote wanatakiwa kutumia mashine za EFD kutumia mashine hizo.
  • Serikali sasa iweke mikakati ya kuhakikisha wale wafanyabiashara wenye mashine hizo ambao hawatumii mashine hizo ipasavyo au wanafanya udanganyifu wanatambuliwa na kuadhibiwa ipasavyo. Hii inaweza kwenda sambamba kuwapo kwa kikosi kazi ambacho kazi yake itakuwa ni kuvizia wale wanununuzi na kuwatakisha risiti lakini pia kwenda mbali zaidi kuona kama risti iliyotolewa inaendana na thamani ya vitu vilivyonunuliwa ili sasa kuwabana wale wanaopunguza thamani ya manunuzi iliyofanywa.
  • Tumekuwa tukiwataka wanunuaji kudai risiti, sasa ifikie hatua iwekwe sheria kuwa unapofanya manunuzi yoyote yanayozidi kiwangi flani labda elfu 2 ni lazima uwe na risiti na kutokuwa nayo ni kosa kisheria ambalo litakufanya ushitakiwe kisheria.
  • Serikali iandae mpango mkakati wa kuweza kuwakopesha wafanyabiashara mashine za EFD na kuwa inawakata kidogokidogo kwa kiwango na muda unaokubalika. Hii itasaidia kuwafikia wafanyabiashara wengi kwa muda mfupi.
  • Serikali lazima iwe na kikosi kazi kila mkoa ili kuhakikisha kuwa tatizo lolote la kiufundi la mashine ya EFD linapatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi na mfanya biashara anawajibika kutoa taarifa mara tu aonapo tatizo. Kutokukutoa taarifa kutachukuliwa kama kosa la ukwepaji kodi.
  • Kama mfanyabiashara hataki kutumia mashine hizo kwa "visingizio" vyovyote vile basi mamlaka husike ichukue hatua ikiwa ni pamoja na kumfungia biashara na kuhakikisha haendeshi biashara hiyo mpaka muda wa adhabu utakapokuwa umekwisha. Neno kisingizio hapo juu ni pale ambapo kila liliotakiwa kufanyika limefanyika lakini bado mtu huo anakaidi.

Wafanyabiashara kuendelea kuonesha ubabe wa kukataa matumizi ya mashine hizo ni ishara kwamba wanakuwa wababe kwa mamlaka husika na hiyo si ishara nzuri kwa serikali. Serikali lazima ibaki kuwa serikali na vyombo vyake vyote lazima vibaki kwenye kutimiza wajibu wake.

Kwa kufanya hivyo tutaondoa migomo isiyokuwa ya lazima ya kusitisha huduma kwa umma ikiwemo hii ya wafanyabiashara wa maduka, wafanyabiashara wa mabasi ya usafirishaji, wafanyabiashara wa mafuta na kadhalika ambao nao wamekuwa na kawaida ya kutishia kusitisha huduma kwa umma na kusaau kuwa hiyo ni dhamana.

Note: Sitegemei kuungwa mkono na wafanyabiashara wenzangu (Nime-declare Interest) maana sasa nimeamua kufikiri zaidi ya wanavyofikiri. Wale tu watakaofikiri kwa manufaa ya taifa letu la tanzania wataniunga mkono, na kunikosoa kwa hoja na kuboresha zaidi huku lengo lao likiwa kujenga na kuwa na muhafaka kwa jambo hili.

Wale watakaonibeza na kunitukana nitawapuuza tu maana ndo jambo naweza kufanya.

C.C Mwigulu Nchemba
 
mbona wafanyakaz wanalipa kodi tena kwa kiwango kikubwa sana! inabid hawa wafanyabiashara washughulikiwe ipasavyo!!!
 
Kama hawataki EFD si watafute mashamba wakalime? Maana hili halikwepeki, wafanyakazi ndio wamekuwa ng'ombe wa maziwa nchi hii.
 
Choma nakuunga Mkono,lakini Pia huyo huyo Nyerere uliyemsema aliwahi kusema serikali ya kifisadi ni ile itakayoshindwa kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa,makampuni nk,na kikimbizana na hawa wadogowadogo,kwa nini nguvu hiyo hiyo ama mikakati hiyo hiyo unayoielekeza isitumike kukusanya kodi kwenye migodi.wote sisi mashaidi zile fedha walizogawana za escrow mwigulu mwenyewe alikiri kwamba zilikuwa hazijalipiwa kodi.Sasa issue Kama hizi zinawafanya watu kuchoka,kwani hizi mashine ni kwa wafanyabiashara tu ama hata kwenye taasisi za serikali,
 
Kingine jamani serikali hii hii inayosema wafanyabiashara wa Maduka hawataki kulipa kodi,ndiyo hiyo hiyo utasikia imewasamehe wawekezaji kodi mabilioni ya hela,huku inakuja kikimbizana na hawa wa huku chini,tozeni kodi toka huko juu mpaka chini.sio mje kukomaa na huku chini,na kwa wafanyakazi,afu huko juu kimya.Mara ngapi watu wamekuwa wakisema hawa homeshoping center wamekuwa wakiingiza makontener mengi tu bila kulipa kodi kisa wanajuana na mweshimiwa.hili nalo ni Tatizo
 
Nakubaliana na wewe By hair juu ya hoja yako ya kukusanya kodi hata kwa wafanyabiashara wakubwa. Binafsi sikusema kuwa wafanyabiashara wakubwa wao wawe (exempted) waondolewe kwenye kulipa kodi.
Serikali lazima ifanye kila linalowezekana ili kuhakikisha kila anayetakiwa kulipa kodi analipa kodi stahiki. Mzigo wa kodi amebebeshwa mfanyakazi na hii ni kwasababu tu serikali inachukua kodi yake kabla naye hajatia hela hiyo mkononi. Nadhani itakuwa jambo jema iwapo na taasisi za serikali nazo zitaanza kupokea malipo kwa mashine za EFD. N vema serikali inapoamua kufanya jambo isifanye kwa kupendelea au kubagua ili kuondoa dalili za ubaguzi na uonevu kwa baadhi ya watu au taasisi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom