USHAURI wangu kwa Nappe, Mwigulu plus Vijana wabunge wote wa CCM na UVCCM

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
I salute you

Hakuna mtu anayekataa ushauri, na mtu halazimiki kuufuata ushauri anaweza kuufikiria kisha akauacha au akaufuata kadiri ya Dira, Mtazamo na Moyo wake anapouelekezea. na pia ni vema kuelewa Nia na mitazamo yetu hubadilishwa na picha za mawazo tunayoyajenga kutokana na mazingira mtu anayoyapitia katika makuzi yake. wewe ni Mbunge, kiongozi, mjumbe au uko kwenye kada yoyote Ndani ya chama chochote cha kisiasa, unaweza kujiuliza umefikaje hapo. Kuna wazo ambalo lilikupendeza ama kwa kushauriwa, kuona na kisha ukalifuata baada ku kuikubali dhamira yako juu ya wazo hilo na ndipo ulipo chukua MAAMUZI.. lakini bado kuna safari mbele ambayo kama binaadamu bado mlango haujafungwa kupokea mawazo zaidi na uelekeo mpya wa utashi wa kile unachokitaka NA KUCHUKUA ZAIDI YA maamuzi. Nguvu hii ya ushauri inayoweza kumfanya mtu kupokea kitu kipya, ufaham mpya, upeo na welewa mpya, na kuzidi kupiga kasia la kuchukua MAAMUZI, ndiyo inayonituma Kisima, nifikirie kwamba yamkini naweza shauri kwa hili na moyo wa mtu flan, wanaweza kuwa si wote lakini mtu flan akaaamka na kuona ukweli wa mambo Na Akachukua MAAMUZI.

NDUGUZANGU, Sisi tunaoishi karne ya leo hatuwezi kujipendelea kwamba ndio bora zaidi kuliko ndugu wengi waliotutangulia ingawaje kwenye maisha kila msimu wa miaka ya kizazi hujiona bora kuliko mingine. Lakini ni kweli kwamba wote ni raia wa ulimwengu huu, na zipo kweli ambazo hatuwezi kuzipinga. Ni kitu kisicho wezekana mwanadamu kupambana na majira. majira yana nguvu ambazo hatuwezi kuziona. ni nguvu ambazo hazipo mtu kupambana na upepo. penda usipende upepo unavuma na utazidi kuvuma. kwa mkao wa Dunia yetu kwa sasa hatuwezi kupinga kwamba dunia sasa inapitia vipindi vya mizunguko, na kila mzunguko wa maisha una yake.

tunakumbuka sote kwamba maisha yalianza na familia, kisha koo na baadae jamii ikatokea. ukianzia kwenye familia, automatik kulikuwa hapana demokrasia.. lazima baba awe mkuu wa familia. na mama msaidizi wake piga ua. hapakuwa na demokrasia kwamba achaguliwe mkubwa wa familia . halikadhalika kwenye koo bado yule kigaga wa umri akawa ndio mkulu wa koo. jamii zilipoanza kuwa kubwa pakawa na complication kidogo. kigaga wa umri akifa basi wanabaki vigaga wanaofuata wa umri ambao ni zaidi ya mmoja. lakini wote wakawa wanaongoza jamii na kukawa na mkanganyiko mkubwa. huyu akihukumu hivi yule anahukumu vinginevyo kukawa na mgongano wa kimaslahi, kindugu na kiitikadi manake kila mzee alikuwa anajiundia viitikadi vyake. watu wakasema no, awepo mmoja tu kiongozi afuatwe yeye kwa mazuri na mabaya yake. so kukawa na circle, akifa aliyechaguliwa uchaguzi mwingine unafanyika miongoni mwa wazee tu. hiyo ndiyo democrasia ya kwanza kabisa watu hawajui hili. ingawa ilikuwa haiwahusishi jamii yote bali wazee waliofuzu umri mkubwa tu.

univumilie kidogo Kisima nijenge hoja, tabia ya wazee hawa kuchaguana kwa kulaza fimbo kwa wanayemtaka awe kiongozi, ilileta mtafaruku. kwanza mtawala alikuwa na vijisheria ambavyo ililazimu kumfuata mtake msitake, na akitoka huyu anaingia mwingine. wazee wakawa wanatafutiana visa ili huyu afe mwingine achaguliwe. Ndipo tamaduni za Miungu na uchawi wa kulogana zilipoanza na kuzidi. uroho wa madaraka ukawafanya wazee wetu hawa wauane sana. wakaingia kwenye mzunguko mwingine, wakasema no, hii mambo tutauwana sana, basi atafutwe mtu mmoja, ambaye miungu na matambiko yatamkubali na kufanywa kwa ajili yake, na aapizwe kwa miungu hao kwamba hatatenda mabaya watu wake, na pia aapizwe kutoiasi jamii yake. uamuzi huu ulilenga kukata mzizi wa wivu, fitina, na mauaji ya wanafamilia wazee kwamba ni huyo tu mtu mmoja kwenye familia moja ndio atakuwa na dhamana ya utawala wa kurithishana. ndipo mambo ya uchifu, utemi na mengineyo ya kifalme yalipo anza.

wafalme hawa wamedumu kwa miongo na karne kadhaa. na Dunia yote ikaamini kwamba huo ndio mfumo bora kwa sababu dunia ilitulia. imagine Australia kulikuwa na wafalme Africa, Brazil na kila pembe ya Dunia. Niulize nani aliwaambia jamii hii au ile kwamba kule kuna ufalme na ninyi anzeni? hapakuwa na mawasiliano, hapakuwa na mwingiliano wa lugha, hapakuwa na urafiki, lakini automatic Dunia nzima inajikuta inabadilika kutoka mfumo huu wa utawala kwenda mwingine, ni upepo unavuma hakuna wa kuuzuia.

lakini baada ya miongo mingi na ulimwengu kuzidi songa mbele, madhoruba yakaanza kuvinjari utawala wa Kifalme. Tamaa ya Nguvu.. ama nguvu ya mali au ardhi. si mfalme pekee aliyekuwa na mali tena bali na familia yake pia. hapo matabaka ya wenyenazo na wasionacho yakaupiga kwa nguvu utawala wa kifalme. wenye mali wakazidi kuwa nazo na wasio nazo hata zile kiduchuu wakanyang'anywa. watawala wakachekelea na kuwanyanyasa watu wa daraja la chini la maisha. lakini watu hawa wakatambua kwamba haki haipo tena bali dhuluma. kwani wao kina nani, kwanini wao tu watutawale sisi?. hali hiyo ikawapelekea baadhi ya watu katika jamii kufurukuta kutafuta mali au utawala lakini bahati haikuwa yao, nguvu hawana wala mali hawana wakaishia kukatwa vichwa. lakini dhuluma ikanawiri zaidi, na harakati za mwanadamu kujikomboa zikazidi sana kifikra. mwanajamii akitumia nguvu atauawa lakini lazima atoke kwenye shimo hilo la mateso.

Mwanadamu ni kiumbe wa ajabu sana. katika harakati za kufurukuta nae atokee kivyake ndipo mapinduzi ya Elimu taratibu yalipoanza. Elimu iliwafanya waanze kugundua vitu au nyenzo. na nyenzo hizi zilikuwa kama mashine kwenye maisha yao ya kila siku. wazee wengi wa kiafrica wakahifadhi elimu hizi kwenye simulizi. anakusimulia huyu na yule anamsimulia huyo basi kazi kazini. jamii nyingine wenzetu wazungu wakaona masimulizi si mazuri sana, bora yule mwanzilishi wa elimu ahifadhi elimu yake kwa njia nyingine mbali na simulizi. ndipo michoro ilipoanza. matumizi ya michoro na michoro na herufi kwa herufi na baadae maandishi.

wakati wenzetu wanaweka ya kwao kwenye maandishi sisi tunachapa domo kwa domo kwa kwenda mbele. Elimu kuwa kwenye maandishi kwa wenzetu kuliwafanya watu wengi kuipokea taaluma ile kwa uharaka zaidi. ugunduzi huu wa taaluma na kuiweka kwenye maandishi hasa juu ya mawe kuliipa dunia uelekeo mwingine, tokea maandishi yaanzie kwenye mawe, then mbao then ngozi, then vitambaa hadi karatasi yametoka mbali sana. mtikisiko huu wa nguvu za elimu ukazifanya tawala kuyumba, ili kuweka mambo sawa wenye elimu wakaogopwa kama miungu na kutimliwa. Wakakimbilia kwenye jamii nyingine na kupewa tuzo ya heshima na ukuu, ila baadae nao wakawatimua wale walioonekana kugundua kitu kingine ndani ya jamii hizo. timua timua hiyo iliendelea kwa namna tofauti hadi baadhi wakatimkia Africa. wazungu walitukuta na Elimu yetu ingawa tulipasiana kwa domo, wakaipiga chini na kutumezesha ya kwao hapo ndipo tulipoingizwa mjini moja kwa moja tukaikamata yao hadi leo.

elimu ilizaa nia ya kuzidhibiti falme, na wakaweka sheria mtawala asizivuke, mwisho wakaweka vigezo vya mtawala, baadae wakakubaliana kwamba sasa huyu hawezi kuwa mfalme tena lazima awe ni kiongozi wa sheria tulizo jiwekea sote. kazi yake si kuzitunga wala kuzibadili ni kuzisimamia wakati zikitekelezwa. walatini wajanja sana wakatoa jina la rais awe President.. wakiwa na maana kwa kilatin Prae-Sedere yaani Prae(mbele) , sedere(kukaa) yaani praesedere - kukaa mbele kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama tulivyojipangia.

so Rais sio tena muamuzi, mpangaji, mtoa order zake no, anatakiwa kuisimamia sheria ambayo jamii imejiwekea. na sheria hii wakaiita Katiba. jamii ikajiwekea taratibu za kumpata Kiongozi wa kuisimamia katiba na mambo sasa yakawa ahueni.

lakini katiba hizo hazikuwa mwarobaini wa kila kitu. bado jamii ilikuwa na mambo mengi sana na kila siku mambo mapya yanazaliwa. Mianya hii iliyowachwa wazi na katiba ikampelekea mtawala Kuchomeka matakwa yake kwa jina la itikadi. matakwa yale yaliyokuwa na madhaifu mengi yakapelekea kuchukiza baadhi ya jamii. na ndipo tena makundi yalipojitenga na kuanza kupambana na mtawala kwa Vita za wenyewe kwa wenyewe. nadhani watu tunajua mapinduzi ya utukufu (Glorious Revolution 1688) au Exclusion crisis. Itikadi ni kama kasumba ni kitu kinachomkaa mtu kwa Muda mrefu na si rahisi kukiacha kwa siku moja. ndipo watu wakasema basi tuvumiliane, haina haja ya kugombana, ugomvi unatokana na watu kuwa na nguvu ya kijeshi, basi tuunganishe Jeshi. jeshi liwe mali ya Serikali. Iwepo Katiba ambayo inaridhiwa na watu wote. huduma za kijamii zote ziwe mali ya wananchi. na kwa sababu kila mtu ana kasumba ya itikadi yake basi uundwe utaratibu wa kuziuza itikadi hizi kwa wananchi. na wale itikadi yao itakubalika basi wapewe jeshi na kuongoza nchi kwa kipindi flan tu cha uongozi kisha uchaguzi mwingine utengwe. Yule ataye kaidi kanunu hizi tulizo jiwekea kunyukwa na anyukwe kwa sababu hapana chama chenye jeshi. jeshi na silaha ni mali ya serikali. Nchi za Ulaya hapo zikapoa na vita ya wenyewe kwa wenyewe zikakoma.

kasheshe likawa kwetu, hawa mabwana wakawa wanatawala huko kwao na huku kwetu. lakini huku kwetu wanachuma tu na kwenda kulia kwao. Imagine tokea wametuletea maandishi yao na tamaduni zao mambo yetu yalikomea hapo wakaanza kututawala kwa mifumo yao. tulipoanza kujitawala tena kama wa Waafrica kwa kitu kinachoitwa uhuru, na sisi tuwe na rais wetu, ni kama tunakipokea kijiti kilee tulichokipoteza zamani zilee walipotuletea Elimu yao na kuipoteza yetu. lakini tunakipokea kwa misingi yao, njia zao, gunduzi zao, elimu yao, na kila kitu chao. kimsingi tunapokea kijiti chao tukiamini ni chetu.. changa la macho baya sana lile..

Watawala wetu baada ya kukipokea kijiti badala ya kwenda mbele wakaanza kwa kasi kurudi nyuma, kuelekea kulee nyuma kabisa kwenye point ambayo hata hawaikumbuki wala kuijua. hata wao maskini ya mungu waliamini wanakwenda mbele kumbe walikuwa kasi wakirudi nyuma. Hawakujua kwamba wamekuwa marais kwa taratibu za wazungu wala si zetu. mbio zao za nyuma zikagota kwenye Ufalme. wakajikuta wameshakuwa Marais Wafalme. wao tu ndio thinktanks za taifa. fikra zao, mawazo yao. mbaya zaid na jeshi lao. Chama kimoja, serikali moja kitu ambacho kilishashindwa na mzunguko wa dunia. Ni Ujinga wa kutojua Chama ni nini na Serikali ni nini, na Ujinga huohuo ndio unaolipeleka Taifa kuabudu kuwa na serikali moja-chama kimoja.

kwa wasiojua, Serikali ni mhimili, ni kama tuseme maziwa ya moto. Vyama ni kama additive au kiungo kwenye maziwa hayo. mfano majani ya chai, kahawa, Kokoa n.k ni matakwa ya mteja(mwananchi) kuchagua maziwa yake(serikali) aiunge na nini(Chama) kokoa, majani ya chai au kahawa. ni vile atavyovutika yeye. sasa imagine unaingia hotelini, mhudumu anakwambia maziwa ya moto yapo unaweza kuyaunga na viungo utakavyo.kisha unamwambia niletee hayo maziwa na viungo vilivyopo nichague. analeta maziwa na majani ya chai peke yake. unamuuliza viungo vingine viko wapi? anakujibu hakuna. Huyu lazima utamwona hamnazo. amekampein kwamba pana viungo tele kumbe ni kimoja sasa kwanini asiungie huko huko mwenyewe?.

tuliishi kwenye miongo ya kipumbavu sana, ati tunaambiwa maziwa ya moto yako tayari(SERIKALI) chagueni Viungo sasa(Chama), lakini kwa bahati mbaya pana kiungo kimoja(CHAMA), basi ndugu wananchi chagueni kama mnakipenda au hamkipendi kiungo hiki kimoja pekee.. Ujinga mkubwa, sasa inamaana tukisema ni kibaya tumekilinganisha na nini???!! au tukisema kibaya ndio tusile??!! maana mashart ya mlo tumeshajiwekea kwamba maziwa sharti yaungwe ndo mlo uliwe! na kama kiungo hatukipendi basi mlo ndo hakuna??!! kama mlo hakuna kuna nini basi? katiba haisemi chochote hapo..!! si mauaji hayo??!!kama kuna Chama kimoja na serikali moja hapana haja ya uchaguzi. ni kuongoza tu jumla uchaguzi wa nini kwa nini..?

Taratibu tawala za Kiafrica zikaanza kubadilika polepole sana. na bahati mbaya mfumo wa Kifalme automatic ulikuwa zigo zito mno kwao na ukaanza kujiondoa wenyewe. kitu cha ajabu kikaingia, Vyama vingi.. lakini vyama hivi ni kama fata upepo wa magharibi. hawajui wanaanza wapi wanatoka na wapi. kuna mapungufu mengi kwenye mfumo wa vyama vingi vya kiafrica lakini tutake tusitake tayari sisi ni sehemu ya kizazi hiki.

Kisima niweke mstari kwenye dhima ya hoja, Vijana wa CCM, Nape, Mwigulu, UVCCM na wengine, nikiangalia cv za wengi mmezaliwa kwenye miaka ya sabibi au themanini, na makamu ya kuzianza siasa ni Juzi tukiwa tumeshaanza mfumo wa vyama Vingi ulioanza 1992. hamjitendei haki wala haiba kujitukuza kwamba nyie ni sehemu ya mfumo zandiki usio na kichwa wala miguu wa chama kimoja-serikali moja uliotuburuta miaka mingi. Ninyi mmezukia kwenye makamo ya vyama Vingi. Wazee wetu waliendesha CCM kimakosa, walitenda kimakosa lakini tunawasamehe kwa sababu upeo wa ufahamu wao uliishia pale. lakini leo kuna kizazi chenye macho, ni kizazi cha visima vya mawazo sio matanki tu. Tuwaache wazee hawa na chama chao wapumzike kwa amani. sisi vijana embu tujipambanue kenye ulingo mpya wa kisiasa. Tujenge taaswira mpya ya taifa letu kwa Mtazamo mipya. Ni -------- pekee anaye weza kuwaza kwamba atakifanya chama kiwe cha mfumo mpya kwa matakwa mapya ya kiuboreshaji. huyo ni -------- wala si mjinga. ni kama mkatoliki kaokoka anawalazimisha wakatoliki humo humo nao waokoke. anafurukuta nao wee kwenye parokia yake.. unaujua ukatoliki wewe, unajua ulianzaje, unajua maagano yake.. unausukuma upepo. utachelewa!

CCM ni chama, hamjui kilizaliwa vipi, hamjui maagano yake, hamjui kafara zake, hamjui misingi na miiko yake iliwekwa kwa nini? mnadhani mnaweza kumbadili ng'ombe kuwa Punda?!. zaidi mnachofanya ni kuchota upepo mpya wa mabadiliko na vuguvugu za kisiasa na kuumimina kwenye chama chenu na hapo ni kukiharibu chama, Nyumba ya udongo, unaweka Kigae, unaweka A/c, unaipamba ionekane ya Tofali la kuchoma, utaidhibitivipi mikunjokunjo na miinuko yake? Nchi ni kubwa hii, ardhi tele na maeneo tele kwanini Kutojenga Nyumba mpya unahangaika na kukuu?.ni kero kuweka kiraka kipya kwenye nguo kukuu. Kiacheni chama na mapata yake na makosa yake na heshima yake. kikae kitulie tukiandike kwenye historia kwamba ilikuwepo CCM ilifanya haya na yale ikatulia zake kwa amani. Ingieni kwenye uwanja mpana wa siasa pevu ya Vyama Vingi, sambaza Itikadi zako kwa uwazi. jenga hoja zako ukiwa pembeni sio humo kwenye koti la bibi, jiungeni kwenye vyama vingine vyovyote tujenge taifa kwa hoja na Fikra mpya nzito. Mbona hampendio kujenga Historia Nyie. mnataka kuua historia za utu wenu kila siku. raise and shine!.. do something.. !

huo ni ushauri wangu Lakini niwape angalizo kuu, Upepo huu wa mabadiliko haujaanza jana. nimekupeni historia sikuwa natia hadithi, nilikuwa namaanisha kwamba hata kama watu wote na vyama vyote vitajiunga viwe CCM, lakini sure i am telling you, 2015 CCM kuingia madarakani hicho kitu hakipo. tuko wote, keeep watching.. sidhani kama kuna mtu anaweza kuuzuia upepo usivume.. ni kama kasi ya upepo inavyovuma sasa, mnavua nguo kuuzuia mnabaki uchi watu wanawacheka. kijana mdogo unakuwa kama zee!!?. Kukaa na wazee mwisho mtakuwa kama vizee na mtakula na kuliwa na wazee.!!. hatuwapingi wazee lakini tunataka waboreshe fikra zetu sio tabia nzuri kukaakaa na mazee muda na masaa yote hadi usiku he..! mwishowe ndio kutengeneza tabia mbaya mzee anajisahau kama ni mzee anajiona na yeye kiijana matokeo yake mzee wa miaka sabini na kitu anavua chupi na kukaa uchi mbele ya katoto ka miaka 14, kajukuu kake na kukaingizia dude ambalo angemwingizia bibi yake.. pyuuu..!! a mark of Curse business..!!

i submit..
 
Andika synopsis. Nakuhakikishia hii hakuna atakayesoma.

nakumbuka siku moja nilimimina pages like today, raia mmoja akakurupuka kuccoment "andika sammary bwanaeee".. baadae alipojituma kudidimia kwenye andiko alikuja faster kuondoa comment yake.. here you are today.. wavivu hawana nafasi kwenye nchi yoyote inayoendelea. wavivu wa kusoma hupenda mambo mafupi yenye akili fupi fupi kila siku na matukio mafupi mafupi kwa majanga mafupi mafupi....
 
Kajipange,Dikteta mkubwa wewe unayetaka taifa liwe na chama kimoja,unataka wote tuwe bavichwa,fuuiuumbafu,eti sijui makafara,upuuzi mtupu,yani unataka vijana wa uvccm wahame ccm kwa hoja zilizokonda hivi?kweli Bavicha vituko
 
Ccm itaiongoza nchi hii karne na karne, hata hivyo haitaacha kuvilea vyama vidogo vidogo vya siasa huku ikipokea maoni yao. Ccm daima
 
Mleta mada una hasira mno. Lala upunguze usingizi au nenda kaoge kwanza urudi hapa. Ukija utueleze maendeleo ya mtifuano ndani ya chadema na vipi kuhusu lema kufanyiwa kitu mbaya. Hakuambukizwa ukimwi kweli
 
Asante kwa andiko zuri na lenye ukweli uliojaa fundisho. Jamani jaribuni kulipitia andiko hilo taratibu ingawa ni refu lakini ni zuri sana.
 
Back
Top Bottom