Ushauri wangu kwa Mzee Samuel Sitta

Bunge la 12 samweli sita hatoliweza, na kwa vile ccm watapeleka jina hilo na kuambiwa wamchague, nashauri na chadema wampendekeze james lemebeli akapambane na sita. Hii itakuwa hatua nzuri ya kulitabiri bunge lijalo...

Hiv lembeli ni mbunge??
 
Hapa Manyerere nakuunga kwa asilimia 1000 haiwezekani kuanzia enzi za Mwl Nyerere iwe yeye tu atapumzika lini?na jambo gani jipya atalifanya kwa sasa,kwa kuongezea naongeza ile listi ya wazee waliopata aibu kwa kung'ang'ania madaraka alikuwepo marehemu Makweta,kwa hili lazima tuseme na tupaze sauti kusema NO kwa Sitta hatufai tena,na hatujasahau alichokifanya bunge la Katiba,yeye ndie alifanya UKAWA inayoitesa CCM izaliwe ,usingekuwa uimla wake tusingekuwa na kitu kinaitwa UKAWA,kama mwenzake alisema ataenda kuchunga ng'ombe akishindwa naye sasa ni wakati wa kwenda''kurina asali''kha haiwezekani toka nazaliwa nasikia Sitta ,Sitta na sasa ninawajukuu bado tena Sitta
 
Mzee hana haya huyuu!!??
 
Jina la Spika wa Bunge la 11 lipo kwenye Mfuko wa Koti la Jakaya kama ilivyokuwa kwa Rias wa tano kama tulivyoambiwa na Mzee Kingunge.

Samwel Sitta alitumika bila kujua Kumsambaratisha Edward Lowassa 2007 kwa Kuanzisha Mjadala wa Richmond, Edward Lowassa nae akatumiwa kulipa kisasi kumsambaratisha Samwel Sitta kwa kumtumia Mzee Makamba kutumia busara za kuweka kigezo cha Jinsia kwenye nafasi hiyo kubwa 2010.

Baada ya kufanikiwa kusambaratisha Marafiki zake wakubwa sana kwenye serikali yake sasa kazi iliyopo ikawa ni kuhakikisha hawatakuwa sehemu ya serikal ijayo kazi imemalizika kwa Lowassa sasa inageukia kwa Sitta.

JK ni Zaid ya Mwanasiasa hutumia wanasiasa kumalizana bila ya wao kujijua.Ilianza Sitta vs CCM akakoswa koswa kuporwa kadi ya ccm 2010, Lowassa VS Sitta 2007-2010, Chadema vs Lowassa 2007-July 2015 , Lowassa vs CCM July 2015-to date.
 

Kuna kipindi huwa mnakengeuka sana na leo mmeanza kusomeka vizuri. Kwani Lowassa aliyeutaka urais mkamshadadia umri wake ni mdogo kiasi gani? Na kwanini unafikiri Six ana ulevi wa madaraka wakati kwa Lowassa haikusemwa ni mlevi wa madaraka, kwani kati yao nani kijana wa leo? kama mliamini Lowassa angeweza kuleta mabadiliko katika umri ule kwanini Six asiweze wakati wote ni kizazi kimoja?
 
Sitta ndo mchawa wetu Tz.,yeye ndo kaifinyanga katiba ya wananchi ya mh Jaji Warioba kwa kuwafurahisha walomtuma,leo achukue uSpika!! Magufuli atumie rungu la kiti chake kumpiga ban,maana atamharibia. Hana mana hata kidogo mzee huyu.
 
Sita ni kituko / Kinyago cha demokrasia. Yeye na samia Kwamepindisha katiba wakati wa bunge la katiba.
Wewe Mzee ebu ona aibu. mara hii Watanzania watakuchapa kama alivyokuchapa Mwalimu!
 
Bunge la 12 samweli sita hatoliweza, na kwa vile ccm watapeleka jina hilo na kuambiwa wamchague, nashauri na chadema wampendekeze james lemebeli akapambane na sita. Hii itakuwa hatua nzuri ya kulitabiri bunge lijalo...
Sasa lembeli hata kwao wamemkataa nani atampa uspika,halafu kumbuka kura za ukawa ni ndogo bungeni bado wataendelea kuisoma namba
 


huyu atafia kwenye kiti kwani lengo lake na kundi lake halijatimia
 
kama Sitta atagombea basi hakuna wa kumzuia , wabunge wengi wanampenda sana Sitta kwa sababu anawajali sana wabunge

Huo ndio ukweli mchungu,ingawa binafsi simpendi lakini lazima tukubali kuwa wapiga kura ni wabunge ambao anawajali kimaslahi
 
Wewe unajua umri wa Sitta wewe?Sita ana miaka 76 wakati Lowassa ana 62
 
Eti watu kama kina Sita hawawezi kuleta mabadiliko???
Vipi hao akina Lowasa, Sumaye na Kingunge hujawaona????
Acheni double standard nyie wenye fikra mfu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…