Ushauri wangu kwa Mhe Tundu Lissu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu kwa Mhe Tundu Lissu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, Jun 14, 2012.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Habari za asubuhi Mhe Tundu Lissu a.k.a mbunge mmoja sawa na wabunge 50. Baada ya salamu napenda nikupe pole kwa machovu ya kukaa muda mrefu kwenye viti vyekundu kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

  Mheshimiwa ninatatizo.................. umekua ukiomba ufafanuzi kutoka kwenye kiti cha spika wa vifungu fulani fulani na wakati mwingine ukiomba ufafanuzi kwa kuuliza maswali ya nyongeza hili jambo ni zuri sana kwani linasaidia watu wanaelimika hapo sina tatizo kabisaaaa.......... Tatizo linakuja pale unapouliza swali mfano lile la kuhusu uranium bila kuwa na elimu ya kutosha na kukifahamu kile unachokizungumza hapo ndio tatizo au pale unaposema kuwa kifungu kinasema PM ataulizwa maswali yanayohusu sera za serikali au maswala yenye maslahi ya taifa na kuongezea kuwa kuuliza swali lini wananchi watasambaziwa nakala za katiba na kutembelea jimbo la vunjo ni upotezaji wa muda! hili ni tatizo na tatizo hili la kuuliza na kuomba miongozo ambayo mwisho wa siku inakuwa inakufanya kama umepwaya kwenye uweledi wako unasababisha watu waone kuwa "una kuonekana"

  Ushauri wangu ni kuwa unapouliza piga swali lenye tani 100! kama vile ulivyanza enzi zileeee!


  Nakupa tano tutaonana baada ya bunge maana nina safari ya kwenda nyumbani Nduguti.
   
 2. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  kuwa mwanasheria cyo kujuwa kila ki2, ajifunze kwa wenzake pia siasa ni kujifunza.
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Point.
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  daima hakuna swali la kijinga. ila watu hufanya makosa ya kijinga kwa kuogopa kuuliza maswali wanayodhani ni ya kijinga!
   
 5. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli leo nilitazama bunge la asubuhi, aisee ni kweli huyu jamaa anakurupuka sana kuuliza maswali yasiyo na tija ama kuomba miongozo kwa ajili ya ufafanuzi ambapo kwa sehemu kubwa kama angetulia ama kujipanga vizuri angekuwa amashapata jibu ama kuelewa kilichofanyika, lakini cha ajabu na ulimbukeni mkubwa wa kutoka media coverage anaingia kichwa kichwa na kuuliza vitu ambavyo ufafanuzi ukitolewa anakuwa amepwaya sana, kiasi kwamba huwezi kuamini kama Mh. Tundu Anthipas Lissu ni mweledi aliyebobea kwenye Sheria.
  Lazima abadilike asilazimishe umaarufu
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nampeeb
   
 7. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Uwezo wako wakufikiri na kuelewa mambo ni mdogo sana hivyo kumuelewa mtu aliyekuzidi elimu na uwezo wa kufikiri inakuwa kazi kweli kweli. Pumzika na wajinga wenzako mwanakwetu.
   
 8. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Yupi bora lissu au livingstone,wassira,lukuvi ambao hata kutaka kujua ufafanuzi hawataki kuusikia?nawashangaa sana mnaomsema lissu ikiwa waziri alikuwa hana taarifa ilhali ni wizara yake mpaka dogo janja aliyekuwa mgeni akawa na taarifa , hivyo lissu anataka kujua kupitia maelezo ya waziri husika
   
 9. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tundu si malaika, nae ana makosa yake pia kama binaadam, na mtu anayemtakia mema akiyaona na kuamua kumweleza ili naye apate kuyafanyia kazi, si mbaya. Tusiwe kama Magamba na "Zidumu fikra za Mwenyekutu". Asante sana Moh'd kwa kuliona hilo na kuthubutu kulielezea humu ili akisoma apate kulifanyia kazi.
   
 10. Joste

  Joste Senior Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee kumbe umemuona. Kila kitu anakizungumza kwa kutaka kuonekana kama ni mtaalamu sana na anauchungu sana na maisha ya watu. Ukimwangalia usoni na ukilinganisha na anacho kisema ni vitu viwili tofauti. Ananikumbusha debate club nilipokuwa shule. Wakati huo umaarufu wa kupanga maneno ya kingereza ulileta umaarufu sana. Kuna mwingine alikuwa hivyo. Bahati mbaya ubunge uliyeyuka
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo huwa anatafuta air time tu aonekane nae kauliza. Ujanja wa kizamani.
   
 12. Joste

  Joste Senior Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa tunazungumzia uwezo na namna ya kupenyeza facts. Kama hajui technologia ya uranium kama mbunge atawaambia nini wapiga kura wake?
   
 13. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lazima tukubali kuwa kila mtu anamapungufu yake na Mh. Tunde Lisu sio malaika ila sioni ubaya wa aliposema swali kama ni lini hasa waziri mkuu ataenda kutembela Vunjo ni sahihi kuulizwa katika maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu wakati taifa lina mambo mengi ya kuuliza na yamsingi kama utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya bunge na utendaji wa serikali tunamuuliza ni lini ataenda kuwaona wananchi wa vunjo that is too low kwa muuliza swali jamani.

  Pili kwenye kesi ya Uranium ni vema tukawa wazi watanzania mara nyingi tumekuwa kama bendera fata upepo leo tutaseam jamaa hajui kitu katika uranium lakini tujifunze wa wenzetu na tujiangalie uwezo wetu wa kuhandle complex issues tusije tukakutwa na mabaraa kwa sababu wengi tunafahamu hasa kwa sasa vuguvugu lililopo katika nchi za ulaya juu ya upunguzaji wa matumizi ya madini ya uranium kutokana na athari zake katika jamii(Ujerumani na Ufaransa). Kama serikali yetu inashindwa kwa sasa kuwadhibiti sawia wachimbaji wakubwa wa dhahabu kuacha kumwaga kemikali za zebaki katika mikondo ya maji wanayotumia wananchi na kusababisha madhara kwa wananchi je serikali hii itaweza kuweka kweli udhibiti wa kutosha kwa kuwalinda wananchi wake kutoka katika athari za madini ya uranium. Tuweni makini ndicho hasa nilichomwelewa Mh. Tundu Lisu kuwa serikali yetu inahitaji kufanya analysis ya kutosha na kujiweka sawa kukabiliana na madhara pindi yatakapo jitokeza na kuhusu kuweka uchimbaji wa madini sensitive kama haya karibu na makazi ya wananchi.

  Huhitaji kuwa genius kujua madhara ya madini haya ya uranium hebu google kesi ya chenobyl kidogo uweze kupata ufumbuzi
   
 14. m

  massai JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hilo nilile pandikizi la batilda buriani,nimekaa arusha kwa muda na kile kipindi cha uchaguzi kule ngarenaro ndiko kulikua na ngome kuu ya magamba.
   
 15. s

  slufay JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hiyo talent huna kajipange, au tafuta page kwenye magazeti ya udaku.
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja.
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu kawasalimie Nduguti na mimi baadae nitapitia hapo kuelekea nyumbani Isanzu! Back to the topic... Lissu ni binadamu so ana mapungufu yake.
   
 18. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Acheni unazi,wabongo kwa kujifanya muchknow,kuna ubaya gani pale kwa Mh Lissu kuomba mwongozo?Endea kamanda kuwanyuka mpaka na hivi vimizizi ya magamba tuving'oe vyote,pamb.....f!!
   
 19. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ha ha I wish ugombee ubunge, nitakupa kura yangu, sijui kama utachangia chochote na wasiwasi na uelewa. usikosoe kitu usichokijua, kama umefanya uchunguzi chama tawala na serikali yake wanamajibu ya kuridhisha sana kinadharia lakini kivitendo ni hakuna kitu, hivyo watz tushituke na utaratibu mzuri wa kupewa majibu ya kuridhisha lakini yasiyokuwa na utekelezaji wowote, bunge linaendeshwa kiutalaam kibabe kwa masilahi ya chama tawala hivyo majibu mengi ni ya kukomoa.
   
 20. M

  Malata Junior JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,207
  Trophy Points: 280
  Kama sijakosea Tundu Lissu amebobea kwenye sheria za mazingira na migodi,huenda ana idea na mambo hayo.
   
Loading...