MESOYA
Senior Member
- Aug 19, 2014
- 150
- 168
Mheshimiwa Kigwangala, Ukiwa waziri wa maliasili na utalii, binafisi napenda kutumia nafasi hii kukupongeza kwa kuteuliwa kwako kuwa waziri wa wizara hii nyeti na yenye maslahi makubwa kwa rasilimali za taifa letu.
Lakini katika hili niseme kwamba napata wasiwasi na mashaka makubwa juu ya utendaji wako. Na hii yote ni kutokana na mfumo mbaya wa utendaji kazi wenu wa kutumia vyombo vya habari. Ili kuwalaghai wananchi angali sheria za maliasili zikivunjwa . kwa faida ya rasilimali hii asilia ni vyema ukabadilika na kuacha siasa katika wizara hii, simamia sheria za wanyamapori kwa maana ya hifadhi zetu na sio kufuata kiu ya siasa chafu kwa kukwamisha juhudi za watendaji na wataalamu wa maliasili. Nimekuona Loliondo si jambo jema sana, badilika.
Na nikuambie kutunza mapori haya si kazi ndogo ila ni dhamira njema ya waasisi na hivyo ni vyema kuilinda tunu hii kwa masilahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.