Ushauri wangu kwa CHADEMA

Ushauri wangu kwa CHADEMA

Mr Someone

Member
Joined
Sep 15, 2018
Posts
39
Reaction score
60
Habari ya usiku huu wanajukwaa?

Kwanza niwape hongera ya kuwa hadi muda huu tuko tunaendelea kupambana na hali hii ya maisha katika uchumi uliovurugwa na wavurugaji, hopefully tutasurvive as we keep on surviving.

Kama kichwa kilivyojieleza hapo juu, uzi huu nautoa ushauri wangu kwa taasisi muhimu katika ujenzi wa demokrasia(vyama vya upinzani).

Kesho tarehe 16 september kuna uchaguzi katika jimbo la ukonga. Kwa hakika kabisa ninajua (hata upinzani wanajua) kuwa Mwita waitarav(mgombea wa CCM ) atashinda. Ndio 'ATASHINDA'. Baada ya hapo Upinzania utatoa malalamiko kuwa wameibiwa kura, mkurugenzi kamatangaza isivyo halali, vituo vimeongezwa. Watalalamika kama ilivyo kawaida miaka yote.

Chadema wanajua kuwa kila mwaka wanashindwa kwa njia na mbinu zile zile. Mule ndani wanao 'wanaccm' wanajua ni vipi ambavyo upinzani huwa unashindwa..

Wanajua fika ni vipi ambavyo council inakisaidia 'tawala' katika masuala ya kifedha mathalani za mafuta kipindi cha kampeni, inajua ni vipi polisi na council zinakisaidia katia upangaji wa ratiba za kampeni, inajua ni vipi jimbo kama ukonga RSO, DSO, RPC, OCD, DC, RC, na vyombo vyote vya dola na team zao zinahamia kule, wanajua fika huyo DED hana nguvu ya 'kusimamia upinzani' ikiwa kweli 'haki' iko kwao-yupo DED mmoja huko usukumani, alimpigia magoti ex SG wa 'tawala' baada ya kushindwa na upinzani. Wanajua mapilato wengi hawawezi kusimamia kweli baada ya chaguzi..

Ni ajabu kuwa still upinzani unasimamisha wagombea katika mazingira yale yale. Ni wakati sasa wa upinzania kususia chaguzi hizi completely kwani kushiriki ni kuhalalisha mifumo hii mbovu iliyopo. Kama wanashiriki basi hakuna haja ya kuja kusimama mbele ya jamii na kulalamikia mambo yale yale kila siku...

By the way, tujiandae na kule nyanda za juu kusini....
 
its true mkuu,huwezi ukakaa chini ya mwembe ukitegemea kupata Nazi...wangesusia chaguzi mpaka katiba mpya na huru ipatikane...ila mie siwalaumu sana hao Policcm hawako mbali yatazushiwa na kufanyiwa fujo kama watafanya hivyo….

ila upinzani kama akina Mbowe tumewasikia kitambo...sura mpya na zenye nguvu zinatakiwa zi emerge..sijui labda Chama hakijui kurecruit wanachama watakayoifikisha Chadema hatua nyingine
 
Chadema ni chama chenye watu wengi, wapya na makini sana. Labda lipo jambo tusilolifahamu linalowafanya bado waendelee kuishi kwa matumaini!
 
Waitara atashinda vizuri sana tena kwa 78%, na sio sababu ya kuwa yuko ccm, bali alionewa na wana ukonga wanajua hili vizuri sana. Ushindi wa waitara hauhutaji msaada wa aina yoyote.

Monduli , Lowassa badi ana power, na inawezekana mgombea wa CDM akashinda, na qa CCM akishinda itakuwa kwa idadi ndogo sana, tukiona idadi ya ushindi wa ccm ni kubwa, chadema waende mahakamani kwani patakuwa na rafu iliyotendeka
 
'Alionewa' kivipi na nani? Just curious.
 
Chadema ni chama chenye watu wengi, wapya na makini sana. Labda lipo jambo tusilolifahamu linalowafanya bado waendelee kuishi kwa matumaini!

kama Chama kina watu makini na wapya,then its time wa reshuffle wa zamani wachukue back seat,sura mpya zipewe front seat..hao wanachama wazamani wawa coach hao wanachama wapya...mbona simple!...uongozi huo huo sasa hivi uko kama cancer inakiua chama taratibu...
 
kama Chama kina watu makini na wapya,then its time wa reshuffle wa zamani wachukue back seat,sura mpya zipewe front seat..hao wazamani wawa coach hao wapya...mbona simple!...uongozi huo huo sasa hivi uko kama cancer inakiua chama taratibu...
Inaweza kufanyika? Utashi huo upo kweli!?
 
either wabadilike,au chama kife..choice is their's
Nadhani lipo tatizo kubwa la siasa za afrika, nalo ni ulevi na ushabiki uliopitiliza wa wananchi (fanatism). Wapenzi wa hivi vyama hawapendi kuyatazama mapungufu ya vyama hivi katika njia chanya, wanakuwa na majibu mepesi yanayowafumba macho (usaliti, umetumwa, unatumiwa)...

Kingine naona kama 'wenye vyama' hivi wanapata faida fulani fulani za kiuchumi na kimamlaka hii inawafanya wawe ni watu ambao 'wanacho cha kupoteza' hivyo inakuwa ngumu kuchukua maamuzi makubwa.
 
its true mkuu,huwezi ukakaa chini ya mwembe ukitegemea kupata Nazi...wangesusia chaguzi mpaka katiba mpya na huru ipatikane...ila mie siwalaumu sana hao Policcm hawako mbali yatazushiwa na kufanyiwa fujo kama watafanya hivyo….

ila upinzani kama akina Mbowe tumewasikia kitambo...sura mpya na zenye nguvu zinatakiwa zi emerge..sijui labda Chama hakijui kurecruit wanachama watakayoifikisha Chadema hatua nyingine
Hapa naona unapotoka au kupotosha maana na makusudi ya mleta uzi,amesema upinzani kushinda uchaguzi wowote katika hali ya kisiasa tuliyo nayo kwa sasa haitowezekana maana wenye nguvu wameshaamua kuwa lazima chama chao kishinde tu
 
Sure, kwa mazingira ya kisiasa, kisheria na kiutawala yalivyo, upinzani kushinda ni ndoto ya mchana..
 
Waitara atashinda vizuri sana tena kwa 78%, na sio sababu ya kuwa yuko ccm, bali alionewa na wana ukonga wanajua hili vizuri sana. Ushindi wa waitara hauhutaji msaada wa aina yoyote.

Monduli , Lowassa badi ana power, na inawezekana mgombea wa CDM akashinda, na qa CCM akishinda itakuwa kwa idadi ndogo sana, tukiona idadi ya ushindi wa ccm ni kubwa, chadema waende mahakamani kwani patakuwa na rafu iliyotendeka
Wewe ni mburula tu unaleta ushabiki mbuzi kwenye majadiliano ya wanaume
 
Sure, kwa mazingira ya kisiasa, kisheria na kiutawala yalivyo, upinzani kushinda ni ndoto ya mchana..
Mkuu lazima tuseme tu ukweli mimi nipo upinzani lkn ukweli lazima tuseme kwa watawala tulio nao ni vigumu
 
Hapa naona unapotoka au kupotosha maana na makusudi ya mleta uzi,amesema upinzani kushinda uchaguzi wowote katika hali ya kisiasa tuliyo nayo kwa sasa haitowezekana maana wenye nguvu wameshaamua kuwa lazima chama chao kishinde tu

sidhani kama uko sahihi mkuu,amesema katika climate hii wapinzani ni ndoto kushinda.Sasa nauliza tangia 1992 upinzani ulivyoanza hii climate Je iliwahi kubadilika??kama haijawahi kubadilika kwa nini wapinzani wanashiriki uchaguzi ilhali wanajua outcome kuwa hawatashinda?,why keeping doing the same thing expecting to get different results....
 
Mkuu lazima tuseme tu ukweli mimi nipo upinzani lkn ukweli lazima tuseme kwa watawala tulio nao ni vigumu
Hata hao ambao wanaohama upinzani wanaweza kuwa na sbb zisizo bayana(mathalani hilo la kununuliwa), lakini ukitazama kwa jicho kavu zaidi, unaona ni kama wana linda political career zao.

Tujue ubunge ni kazi na ajira, itazame kwa picha hii; mtu anafamilia bado na anahitaji kazi, anaona mazingira ya kisiasa jimboni na nchini yalivyo harsh, anaona kabisa kuwa uwezekano wa 2020 kurudi ni mdogo...amini, ni wachache sana wenye moyo mgumu wa kuweza kukataa 'kurudi nyumbani' ikiwa wamehakikishiwa ushindi sasa na 2020.
 
Back
Top Bottom