Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Mimi ni dereva wa mgari makubwa (roli). Kwa takriban miaka kumi na saba sasa.
Kutokana na kazi hii huwa napita njia zote za Tanzania hii. Na mara nyingi naingia nchi za jirani pia. Mabadiliko ya dhamira ya watu hasa vijijini na mijini. Wazee kwa vijana asilimia 85% wanahubiri mabadiliko ya kiutawala. Wengi wanasema CCM 2015 basii!
Binafsi naamini pindi wananchi wa nchi yoyote wakiitaji mabadiliko hamna kitu chochote kitakacho weza kuwabadalisha.
Nashauri vitu Vinne kabla uchaguzi wa 2015.
Mosi - Tuwe na katiba itakayo leta haki kwa vyama vyote la sivyo hali ya mambo itakuwa mbaya sana. Ni sawasawa na binti kumlazimisha kuolewa na mtu asiye mpenda, nyumba kuwa na maelewano ni nadra sana.
Mbili - Chadema iandae mapema mfumo mwepesi wa kupata matokeo kutoka sehemu mbali mbali hasa vijijini kwa mfumo wa kuwawezesha mawakala wao kutuma matokeo moja kwa moja katika mkoa husika kisha kiongozi wa kanda kutuma makao makuu ili yapostiwe kwenye website ya chama. Hii tuige kidogo mfumo wa CNN, japo kwetu ayatakuwa matokeo rasmi.
Tatu - CCM kwa kutambua fika wana makosa mengi katika mfumo mzima wa kiutawala. Ufisadi, Ujangili, Ubadhirifu Nk. Ni vigumu sana kuachia madaraka kwa wepesi. Kwa hiyo ni lazima watatumia dola kuakikisha utawala wao unaendelea ili dhana ya kulindana iendelee. Watatumia usalama wa taifa pamoja na polisi ikiwezekana tutaweza sikia vitisho vya jeshi la wananchi.
Nawashauri CCM huku wakiendelea kututawala wasome alama za nyakati pamoja na hali ya mambo inavyo enda. Si vibaya CCM kujiandaa kisaikologia kukubaliana na hali ya mambo ili kuepusha Amani ya kipindi watanzania wengi wakiwa wajinga kabla ya mabadiliko waliyo nayo sasa kuendelea vizuri. CCM hivi amuoni aibu inayo wapata kwenye mikutano yenu, nalo hilo aliwashutui tu!! Miezi michache iliyopita niliudhuria mkutano wenu pale Mazense ni aibu sana. Tulikuwa wachache sana tulio amua kuja na kuwasikiliza ila wanachama wengi mliwabeba kwa mabasi yenu kutoka sememu mbali mbali hasa katika jimbo la Ubungo.
NNE - CHADEMA, Mna wakati mgumu sana 2013 wakati CCM mawazo na nia yao ni kuwadhoofisha nyinyi kwa namna yoyote ile. 2013 ni mwaka wa mshikamano sana kwa nyinyi viongozi, wanachama na wanainchi wasio wanachama wenye mapenzi ya mabadiliko. 2014 mkifika salama mtapumzika kwani vita ya Urais itaamia CCM kwa kasi kubwa sana. Vita iyo ipo kwa sasa lakini imefunikwa na agenda ya kuimaliza Chadema.
Kwa kumalizia tu, naomba viongozi wa kitaifa wa Chadema mfike Kwamtoro kondoa kwani kuna vijana wana mabadiliko makubwa kwa kuwa wafuasi wazuri wa Chadema awajapata viongozi wa kuwatia Moyo. Wakiongozwa na vijana wawili Richard Mgogo na Shabani Thyichi.
Chadema nawatakia kila la kheri katika vita ngumu mliyo nayo.