Ushauri wangu kwa askari polisi wote

Mr Kind

Senior Member
Mar 4, 2017
178
308
Ushauri wangu kwa askari polisi (sio jeshi la polisi, namaanisha waajiriwa na jeshi hilo), matukio haya yanaendelea kutokea Mkuranga na Kibiti hasa ya kupigwa risasi kwa askari polisi na kupolwa siraha na viongozi wengine wa serikali hasa za mitaa yawe funzo kwenu kwamba na nyie ni Raia kama Raia wengine, ni binadamu kama binadamu wengine, mkipata jeraha mnatoa damu kama walivyo binadamu wengine, na mkipigwa risasi mnakufa kama wanavyokufa binadamu wengine haijalishi mnazibeba kila siku na mnauwezo wa kuzichezea mtakavyo! Lakini muhimu zaidi, mtambue kuwa kwa vile mnaweza kufa kama binadamu wengine, hivyo mnaacha simanzi kubwa na pengo kubwa katika familia, jamii na taifa kwa ujumla kama ambavyo watu wengine wakiwemo wanaopotelea mikononi mwenu bila kosa lolote.

Kama ilivyo kwa binadamu wengine wengi ambao walipotelea au kuteswa na polisi au kutiwa vilema vya kudumu au kuuliwa kinyama na polisi iwe kwa amri (Mfano wale wafanyabiashara wa madini waliopigwa risasi miaka kadhaa iliyopita) au kwa ubabe wenu pasipokuwa na kosa lolote, leo taifa, jamii na familia NANE zimepoteza watu wasiokuwa na KOSA LOLOTE waliokuwa wanalitumika jeshi la polisi. Ni hakika hawa marehemu hawana kosa lolote kwani wamevamiwa tu tena wakiwa barabarani! Labda kosa lao nikubeba siraha ambazo wauaji wametokomea nazo! Au labda kosa lao ni kupenda kwao kufanaya kazi kazi kama askari polisi!? Mimi na wewe hatujui na hatuwezi kuona kosa lao, labda hao wanaharamu waliowaua.

Hata hivyo, matendo haya ya unyama yawe fundisho kwa watu wote wanaofanya kazi kama askari polisi kuwa binadamu yeyeto yule anatakiwa kutendewa haki! Anapoonewa anaumia, jamii inaumia, Taifa linaumia na pia familia zinaumia na kuhuzunika sana! HAKI HAKI HAKI, IWE KWA WOTE KWANI MUNGU ALIPOTUUMBA ALITUUMBA WOTE KWA USAWA NA KILA MTU ANATAKIWA KUTENDA NA KUTENDEWA KWA HAKI!

Pole sana kwa familia, jeshi la polisi na watanzania wote kwa ujumla kwa kupotelewa na askari wengi kiasi hiki kwa wakati mmoja. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi - Amina!
 
Lakini lazima tujiulize:- Hivi kweli hao wanaoua polisi na viongozi wa vijiji mkoani Pwani ni chuki gani iliyo ndani yao? Bila shaka wamewahi kutendewa vitendo viovu. Sio majambazi maana hawachukui mali. Na sio magaidi wa kutoka nje wanaotaka kuharibu nchi yetu maana hawaharibu miundombinu wala vitu vilivyowekezwa kwa thamani kubwa. Inaonyesha ni watu waliofundwa vema na wana uzoefu mkubwa wa mambo ya kivita. Najiuliza tu, je labda ni askari wastaafu waliodhulumiwa mafao? Au ni watu ambao wao wenyewe au ndugu zao wamewahi kuteswa na polisi? Au labda jamaa zao wameuawa bila kosa na askari polisi? Hebu na nyie fikirini mtoe mawazo yenu
 
Pole sana,R.I.P.....Free Ben Saanane pls....tujitafakari kwa umoja wetu,tusiwaige wabunge wengi wa ccm kwa kuzarau mambo ya msingi.....,pia kuzikataa hoja za msingi za wapinzani km utekaji na mauaji...Mungu awape nguvu na uvumilivu wote wenye mazira haya ktk kipindi hiki kigumu.
 
Lakini lazima tujiulize:- Hivi kweli hao wanaoua polisi na viongozi wa vijiji mkoani Pwani ni chuki gani iliyo ndani yao? Bila shaka wamewahi kutendewa vitendo viovu. Sio majambazi maana hawachukui mali. Na sio magaidi wa kutoka nje wanaotaka kuharibu nchi yetu maana hawaharibu miundombinu wala vitu vilivyowekezwa kwa thamani kubwa. Inaonyesha ni watu waliofundwa vema na wana uzoefu mkubwa wa mambo ya kivita. Najiuliza tu, je labda ni askari wastaafu waliodhulumiwa mafao? Au ni watu ambao wao wenyewe au ndugu zao wamewahi kuteswa na polisi? Au labda jamaa zao wameuawa bila kosa na askari polisi? Hebu na nyie fikirini mtoe mawazo yenu

Au wauza mbao na mali nyingine zinazopatikana kwenye misitu.
 
Tatizo nililoliona, likitokea tukio wanakamatwa wale wafuga ndevu. Kwa maoni yangu ndo inazidi kuongeza chuki.

Wahusika walifuatilie kwa undani hili swala ili lipatiwe ufumbuzi. Askari wetu wataendelea kupoteza maisha hadi lini? Inahuzunisha sana.
 
Back
Top Bottom