Ushauri wangu ili Kunusuru vijana wa JKT

Ushauri wangu ili Kunusuru vijana wa JKT

FRELIMO

Member
Joined
Apr 12, 2014
Posts
42
Reaction score
4
Kiukweli huwa inauma sana kukosa ajira baada ya mafunzo yote ya miezi 24 na wengine kama mimi wa JLC miezi 27 pamoja na maneno matamu ya matumaini ya viongozi wetu ingawa FORM YA KUJITOLEA tulijaza wenyewe.

Naomba yafuatayo yaweze kufanyika kunusuru hasira ya vijana wanaokosa ajira maana hata mimi asira hiyo ilisha nikuta kabla ya kukubaliana na hali hiyo na kuanza maisha mengine, kiukweli ile hasira hufikia hatua ya kutaka kutumia mafunzo kinyume na sheria ya nchi.

1. Posho wanayolipwa kipindi cha muda wa kujitolea ikatwe 50% itunzwe ili mwishoni mwa mkataba wapewe wale wote walio kosa ajira kama mtaji waendako

NB: makato ya wale wote waliopata ajira ndani ya mkataba makato yao watapewa waliokosa ajira kwa kikosi husika.

2. Wapewe ajira za mkatamba katika ofisi ya washauri mgambo ili kusaidia mafunzo katika jeshi letu la akiba(mgambo) hasa wale waliopitia JLC (kozi ya uongozi mdogo)

3. Kuwa na taratibu za kutangaza nafasi uraiani, japo robo ya zile zinazo pelekwa katika vikosi mbalimbali vya JKT kwaajiri ya vijana waliopo ndani ya mkataba.Kwani huwa kuna vijana humaliza mkataba na kukosa ajira kwa kigezo cha ELIMU,lakini kuna vijana hutambua tatizo hilo na kuamua ku-reseat mitihani na wengine kusoma QT-PC nakufaulu,basi wapewe nafasi hii kwa qualifications zile zile zinazotakiwa.

4. Kwakuwa vijana walio wengi wanaomaliza mkataba hukimbilia katika security companies basi wamiliki wawekewe masharti ya kuajiri vijana wenye vyeti kutoka JKT tu katika idara ya ulinzi na si wasio na mafunzo kutoka jkt.

5. SUMA JKT,Serikali iichukue hii kampuni kisha kuchukua jukumu la kulinda katika mashirika ya umma kama:TRL,TPA,TAA,NACTE,NECTA,VETA,DIT,GVNT HOSPITALS and etc.

6. kupunguza idadi ya ya vijana wa kujitolea au kuwachukuwa vijana kulingana na uwezo wa kuweza kuwapatia ajira.

NB: Kwani vijana walio wengi dhana ya "UZALENDO" na"MBINU ZA UJASILIAMALI" kwa sasa imekuwa nadharia tu hakuna tena anaeenda kule kwa hilo bali ni kwa lengo la AJIRA tu, kulingana na tatizo la ajira huku mtaani.

NAWASILISHA; wenu V/LCPL ED 757O -832KJ.
 
Volunteer Leader daah wamelalia peki wengi mno street OP yenu.
 
Kaka posho yenyewe 50 elfu alafu ikatwe nusu tena duh
 
Kwa jinsi kijana alivyoandika kaongea jambo ambalo linamsibu yeye na wengine wote waliopitia hayo mafunzo. Kwa mamlaka/Serikali zilizomakini litaichukulia kwa umuhimu, maana vijana wameiva mafunzo na hana mtaji, je, akikodiwa na kundi baya na kumpa mshiko atakataa? Mfumo wa nchi yetu unahitaji kufumuliwa! Nchi ipo "turing point", tuiombee sana hasa mwaka huu wa uchaguzi
 
Du! pole kiongozi miye bwana hiyo hiyo 832 nilichana nyavu baada ya kujua kuona msoto navyojituma nikawaza hivi nikienda kitaa nikijituma kama navyofanyishwa hapa tena kwa amri sitatoboa nikawaza sana usiku nikatoroka

kiukweli nilurudi kitaa na akili mpya na siyo siri mpaka sasa akili yangu inamtazamo mpya juu ya maisha baadad ya kutoroka jkt nipo kitaa hali si haba maisha yanasonga

nikikumbuka doso nakaza zaidi kitaa
 
Back
Top Bottom