Ushauri wangu baada ya kusoma hotuba ya James Mbatia

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Nimeipitia vzr hotuba ya mh James Mbatia,naomba kujikita eneo moja tu kuhusu uharibifu wa barabara SUPER SINGLE TYRES.

Sipingani na na hotuba wa ukweli kuhusu matairi haya katika uharibifu wa barabara,tatizo ni kwamba baada ya kuruhusiwa matairi haya wasafirishaji shehena kwa njia ya barabara wengi waliamua kutumia super single tyres kwenye trailers kwa ajili ya unafuu,badala ya matairi mawili unaweka moja,na hii ni kwa sababu hatuna kiwanda cha matairi na kodi ni juu sana ya matairi,kwa kuwa karibia61%ya trailers ni super single.

Serikalia isikurupuke kuyazuia kwa mara moja, ni vizuri wakawapa wenye super single tyres japo miezi sita ili warekebishe mfumo huku serikali ikipunguza kodi kwenye matairi na kuimarisha reli.

Tukikurupuka bandari italemewewa kabisa na mzigo na mambo yatakuwa magumu sana,waziri mhusika kwa kuwa CAG ameshauri hili pia kambi rasmi ya upinzani basi ni vzr mkawaelewesha wenye magari maana mengi ni mikopo.

Mungu aepushe maamuzi ya ghafla
 
Bila wadau kukaa hii itaumiza uchumi ni kuzuia tu yasiiingie haya yaliyopo yajimalize taratibu
 
Hivi tattizo ni barabara au tairi? Ina maana hizo tairi ni sisi peke yetu ndio tunatumia dunia nzima. Kama sivyo tujaribu kuangalia wajenzi wa hizi barabara tusitafute visingizio visivyokuwapo.
 
Hivi tattizo ni barabara au tairi? Ina maana hizo tairi ni sisi peke yetu ndio tunatumia dunia nzima. Kama sivyo tujaribu kuangalia wajenzi wa hizi barabara tusitafute visingizio visivyokuwapo.
tatizo si tairi wala barabara.....
watu wanabebesha mizigo mizito kupita kiwango cha barabara kuweza kuhimili...
 
Tatizo sio super single bali ni ubora wa barabara zetu ni hafifu , huko nchi za wenzetu hakuna tena double tyre kwenye semi sisi na vilami vyetu vya senti mita mbili na 10% zao ndio tunambwelambwela . kinochotakiwa ni ujenzi wa barabara za zenye viwango vya kimataifa sio haya maigizooo.
 
Ukizuia Super single leo utasababisha hasara kubwa sana na pia hata ukisema wapewe miez sita ki ukweli haitoshi! Nashauro watoe mwaka mmoja na kuanzia sasa wasisajili trellela yeyote ambayo ni super single.

Duc In Altum.
 
Wataalam wa malori mbona mnatuchanganya cjui super single cjui double cngo tupien bas hata kapicha
 
Back
Top Bottom