Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Kwa tulio mbali na Mkoa wa Kilimanjaro, tumepokea kwa hisia tofauti kwa yaliyotokea pale Dodoma. Mkuu,huyo (Mama Anna Mghwira) amehamia rasmi Chama Tawala na kuachana na upinzani. Ni ushauri tu, wanamkoa huo wamuunge mkono pia kiitikadi ili kusukuma maendeleo mbele.
Siyo siri,kwa muda mrefu sasa, Mkoa wa Kili umekuwa ngome kuu ya siasa za upinzani kwa Chama Tawala. Ukiangalia kwa jicho la pembeni,huenda Mkoa ukawa umejirudisha nyuma kutokana na aina ya siasa za upinzani zenye uelekeo wa ubishi zaidi kuliko tija.
Tumeona mikoa mingi ikianza kuimarika zaidi ya hata Mkoa huo uliokuwa ukisifika kuwa wa mfano kwa maendeleo hapa nchini.
Ninaamini,Mkuu wa Mkoa Anna Mghwira ameona mbali katika mageuzi ya uchumi lazima aendane na itikadi ya ChamaTawala,hivyo ni vyema aungwe mkono.
Njia nzuri ya kumuunga mkono, ni kwanza, wananchi wa mkoa huo kwa wingi wao,kuweka mwelekeo mmoja wa kiitikadi ili kumtia moyo, yeye,chama chake, na Viongozi wake waliomteua na wanaomsimamia.
Hayo ni maoni yangu binafsi.