Ushauri: Wameshaachana, ila anaota anafanya nae mapenzi

Rajabu Msechu

Member
Apr 13, 2016
35
18
Habari zenu wanajukwaa la MMU,

Natumai hamjambo na mnaendelea kutekeleza ilani ya Mzee wa Hapa Kazi Tu, bila ya kupepesa ningependa niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Nina rafiki yangu mmoja wa muda mrefu ninayeshirikiana nae kwenye shughuli za kijasiriamali katika kipindi cha muda mrefu, kusema ule ukweli tumeshibana na tunachukuliana kama ndugu.

Hivi karibuni swahiba wangu huyu ameamua kuuaga ukapera baada ya kudumu na mchumba wake/shemeji yangu kwa takribani miaka 2 hivi, kwa bahati nzuri vikao vya harusi tayari vimeshaanza na mwezi wa Tisa anategemea kufunga ndoa takatifu.

Shida ni kwanba katika siku za hivi karibuni amekuwa akiota akifanya mapenzi na Ex wake hali inayomuogopesha sana, ukizingatia mkewe mtarajiwa yupo mbali nae, I mean mikoa tofauti.

Hata hivyo amekuwa na mawasiliano ya kawaida na huyo Ex wake, na hawajawahi kushiriki tendo tangu walivyomwagana.

Amekuja kwangu akihitaji ushauri, napenda kuwakaribisha watu wote kuchangia.

Karibuni sana
 
Ni majaribu tu hayo ndugu, sali sana kipindi hiki...yatapita.
 
X yaonekana ni fundi kumzidi mchumba!..jamaa anamisi mautundu ya x...ha ha ha...hapo hata akioa atacheat tu...
 
Habari zenu wanajukwaa la MMU,

Natumai hamjambo na mnaendelea kutekeleza ilani ya Mzee wa Hapa Kazi Tu, bila ya kupepesa ningependa niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Nina rafiki yangu mmoja wa muda mrefu ninayeshirikiana nae kwenye shughuli za kijasiriamali katika kipindi cha muda mrefu, kusema ule ukweli tumeshibana na tunachukuliana kama ndugu.

Hivi karibuni swahiba wangu huyu ameamua kuuaga ukapera baada ya kudumu na mchumba wake/shemeji yangu kwa takribani miaka 2 hivi, kwa bahati nzuri vikao vya harusi tayari vimeshaanza na mwezi wa Tisa anategemea kufunga ndoa takatifu.

Shida ni kwanba katika siku za hivi karibuni amekuwa akiota akifanya mapenzi na Ex wake hali inayomuogopesha sana, ukizingatia mkewe mtarajiwa yupo mbali nae, I mean mikoa tofauti.

Hata hivyo amekuwa na mawasiliano ya kawaida na huyo Ex wake, na hawajawahi kushiriki tendo tangu walivyomwagana.

Amekuja kwangu akihitaji ushauri, napenda kuwakaribisha watu wote kuchangia.

Karibuni sana
Ndoto tuu na amuombe sana Mungu amtoe moyo ulikoifadhiwa na amuepushe na huyo jini mahaba.
 
Alitaka aote anazini na Dada yake ndo adhihirishe kuwa iyo ni ndoto inayotokana na mawazo yaliyojawa na tamaa zake...

Muambie aache kufananisha ndoto zenye ufunuo na mambo ya kipumbavu
 
Back
Top Bottom