Ushauri: Waliogushi vyeti wasifungwe, wasamehewe. Wengi wametoa mchango kwa Taifa

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,006
3,643
Taarifa zilizopo, kuna uwezekano wa kufungwa jela watumishi watakaopatikana kugushi vyeti. Kwa vyovyote iwavyo,kugushi ni kosa la jinai.

Lakini, kuna aina za kugushi. Mfano,mtu anagushi cheki ya benki kwa sahihi feki, anachukua fedha ambazo hajazifanyia kazi yoyote! Huyu ni mhalifu anayestahili afungwe.

Ukilinganisha huyu na mtu kama Nesi aliyefoji cheti ni watu wawili tofauti. Huyu nesi utakuta mathalani kafanya kazi miaka 20 na hicho cheti feki. Kazalisha almost wajawazito kijiji kizima kwa njia salama!

Ni kweli,alipokea mshahara,lakini aliufanyia kazi kwa ufanisi na uaminifu mkubwa! Ametoa mchango kwa Taifa. Utakuta pia cheti alichofoji ni cha form 4, lakini cha nursing miaka 4 amefaulu vizuri na aliattend chuo kikamilifu.

Ni maoni yangu,watumishi wa aina hii wafikiriwe katika adhabu.
 
Aha nani kasema watafungwa wewe??!
Hao wanaachwa tu, kama kufungwa si wangeanza wale waliotumbuliwa mkuu??
Kina Mwakyembe wanajinadi wanaushahidi lakini mahakamani hawaendi inamaana wameridhika.
Hakuna kufungwa mtu hapo.
 
Taarifa zilizopo,kuna uwezekano wa kufungwa jela watumishi watakaopatikana kugushi vyeti. Kwa vyovyote iwavyo,kugushi ni kosa la jinai. Lakini,kuna aina za kugushi. Mfano,mtu anagushi cheki ya benki kwa sahihi feki,anachukua fedha ambazo hajazifanyia kazi yoyote! Huyu ni mhalifu anayestahili afungwe. Ukilinganisha huyu na mtu kama Nesi aliyefoji cheti cheti ni watu wawili tofauti. Huyu nesi utakuta mathalani kafanya kazi miaka 20 na hicho cheti feki. Kazalisha almost wajawazito kijiji kizima kwa njia salama! Ni kweli,alipokea mshahara,lakini aliufanyia kazi kwa ufanisi na uaminifu mkubwa! Ametoa mchango kwa Taifa. Utakuta pia cheti alichofoji ni cha form 4, lakini cha nursing miaka 4 amefaulu vizuri na aliattend chuo kikamilifu. Ni maoni yangu,watumishi wa aina hii wafikiriwe katika adhabu.

Naona Bashite umekuja na ID mpya jf
 
Aha nani kasema watafungwa wewe??!
Hao wanaachwa tu, kama kufungwa si wangeanza wale waliotumbuliwa mkuu??
Kina Mwakyembe wanajinadi wanaushahidi lakini mahakamani hawaendi inamaana wameridhika.
Hakuna kufungwa mtu hapo.
Kuna ushahidi,wameshaanza kufungwa jela!
 
Forgery is an offence..punishment should be in accordance with the provisions of penal code..over
 
Taarifa zilizopo,kuna uwezekano wa kufungwa jela watumishi watakaopatikana kugushi vyeti. Kwa vyovyote iwavyo,kugushi ni kosa la jinai. Lakini,kuna aina za kugushi. Mfano,mtu anagushi cheki ya benki kwa sahihi feki,anachukua fedha ambazo hajazifanyia kazi yoyote! Huyu ni mhalifu anayestahili afungwe. Ukilinganisha huyu na mtu kama Nesi aliyefoji cheti cheti ni watu wawili tofauti. Huyu nesi utakuta mathalani kafanya kazi miaka 20 na hicho cheti feki. Kazalisha almost wajawazito kijiji kizima kwa njia salama! Ni kweli,alipokea mshahara,lakini aliufanyia kazi kwa ufanisi na uaminifu mkubwa! Ametoa mchango kwa Taifa. Utakuta pia cheti alichofoji ni cha form 4, lakini cha nursing miaka 4 amefaulu vizuri na aliattend chuo kikamilifu. Ni maoni yangu,watumishi wa aina hii wafikiriwe katika adhabu.
Hata mimi naunga mkono hoja. Na hilo naomba nimshauri Rais ili aamini kwamba hao waliandikwa kwenye Ripoti wana vyeti feki walikuwa ni watu wa namna gani katika utendaji kazi. Atumie wakuu wa idara au vyombo vya usalama naamini ataambiwa hao walikuwa ni wachapakazi na watu makini. Mimi bado siamini sana katika vyeti vya form four maana huwa naona kuna walimu mathalani wanaajiriwa wana vyeti vya form four tena division 3au2 wana uwezo mdogo kuliko hata wale wa UPE ambao ni darasa la saba. Pamoja na ripoti hiyo nakushauri Rais wangu mpendwa najua una vyombo mbalimbali unavyoweza kuvitumia kukupa taarifa za kiutendaji za watu hao na amini utapewa sifa lukuki za watu hao juu ya nidhamu kazini na moyo wa kujituma.
 
Na wale wanaotumia vyeti original lakini si vyao watawambuaje?,suala la Bashite ni mfano mzuri, mpaka awepo anayejua/anayemjua huyo muhusika na hao watu wapo wengi sana, hii vita iwe endelevu.....
 
Hata mimi naunga mkono hoja. Na hilo naomba nimshauri Rais ili aamini kwamba hao waliandikwa kwenye Ripoti wana vyeti feki walikuwa ni watu wa namna gani katika utendaji kazi. Atumie wakuu wa idara au vyombo vya usalama naamini ataambiwa hao walikuwa ni wachapakazi na watu makini. Mimi bado siamini sana katika vyeti vya form four maana huwa naona kuna walimu mathalani wanaajiriwa wana vyeti vya form four tena division 3au2 wana uwezo mdogo kuliko hata wale wa UPE ambao ni darasa la saba. Pamoja na ripoti hiyo nakushauri Rais wangu mpendwa najua una vyombo mbalimbali unavyoweza kuvitumia kukupa taarifa za kiutendaji za watu hao na amini utapewa sifa lukuki za watu hao juu ya nidhamu kazini na moyo wa kujituma.
Umenena.
 
Acheni ujinga,mnajua hao wa vyeti fakewameleta madhara gani kwa jamii?Kama ni nesi kasababisha vifo vingapi?Kama ni doctor pia,kama ni mwanasiasa maamuzi yake yamesababisha sintofahamu gani
 
Mbona mna wasiwasi sana? Utetezi na porojo za nini? Msimtengenezee urahisi Bashite, ashtakiwe afungwe fullstop.

Mbona mwanzo hamkuja na hizi arguments wakati wengine wanafungwa?
 
JPM akiwachukulia hatua hao watu elfu 10 peke yao na kumwacha BASHITE Tutafanya kampeni nchi nzima kuwaambia wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani naye,hatutaki double standard hapa kama anamuacha BASHITE na hao elfu 10 awaache hivyo hivyo.
 
Kweli wanamakosa ila tunamuomba Mh. Rais atumie busara zake tu kwani vinginevyo Nchi itaingia kwenye taharuki.
Aanze kuwabana waajiriwa wapya 'ya kale ni dhahabu' na 'Awali ni awali hakuna awali mbovu '.
 
Hiyo imeshapita mkuu kaanzia ya kale sasa ni mwendelezo, kwa hyo hakika hakna msamaha kwa watakaokuwa hatiani, naamn kazi hawana na sheria Kali kuchukuliwa juu yao!
 
ACHENI UJINGAT,MNAJUA HAO WA VYETI FAKEWAMELETA MADHARA GANI KWA JAMII?KAMA NI NESI KASABABISHA VIFO VINGAPI?KAMA NI DOCTOR PIA,KAMA NI MWANASIASA MAAMUZI YAKE YAMESABABISHA SINTOFAHAMU GANI
Amefoji cha form 4, ila cha ufanisi wa kazi yake ya Unesi amefaulu.
Madhara yangekuwepo Kama angeenda moja kwa moja kufanya kazi baada ya kupewa cha form 4
Ila alipewa na kwenda kujiendeleza
 
haijalishi we jua kufoji ni criminal ofence awe amefoji cha chekechea au cha nini sijui hao wanapaswa kuwa segerea
 
Mimi naomba asiingie jeshini, polisi wala magereza najua wamejaa kibao ila awachunie tu, kwani hawa jamaa wakitimuliwa siku wakiamua watumie utalaam wao kufanya uhalifu tutatafutana, hawa majambazi ambao wamejifunza wenyewe kutumia silaha kienyeji wanatusumbua, kuwatuliza, jee hawa ndugu zangu wenye utaalam wakutumia silaha ya kila aina si tutatafutana.
 
Taarifa zilizopo,kuna uwezekano wa kufungwa jela watumishi watakaopatikana kugushi vyeti. Kwa vyovyote iwavyo,kugushi ni kosa la jinai. Lakini,kuna aina za kugushi. Mfano,mtu anagushi cheki ya benki kwa sahihi feki,anachukua fedha ambazo hajazifanyia kazi yoyote! Huyu ni mhalifu anayestahili afungwe. Ukilinganisha huyu na mtu kama Nesi aliyefoji cheti cheti ni watu wawili tofauti. Huyu nesi utakuta mathalani kafanya kazi miaka 20 na hicho cheti feki. Kazalisha almost wajawazito kijiji kizima kwa njia salama! Ni kweli,alipokea mshahara,lakini aliufanyia kazi kwa ufanisi na uaminifu mkubwa! Ametoa mchango kwa Taifa. Utakuta pia cheti alichofoji ni cha form 4, lakini cha nursing miaka 4 amefaulu vizuri na aliattend chuo kikamilifu. Ni maoni yangu,watumishi wa aina hii wafikiriwe katika adhabu.
Wakati mwingine tuwe tunasikiliza yanayosemwa,Mheshimiwa raisi amesema wale watakaojiondoa wenyewe kabla ya May 15 hao watasamehewa,lakini watakao komaa hadi kupita hiyo tarehe na huku wanajua kuwa wana vyeti visivyo halali basi hao wanaitafuta jela,na wale ambao wanataka kujiendeleza nafasi ipo.
 
Back
Top Bottom