Mkwaha
JF-Expert Member
- Oct 4, 2012
- 1,732
- 3,267
Miaka kadhaa iliyopita nilisafiri kibiashara nchini msumbiji. Katika pilika pilika za biashara nilibahatika kukutana na mwanamke ambae baada ya kufahamiana tuliazisha mahusiano ya kimapenzi. Baada ya penzi kukolea wazo la ndoa likanijia, hivyo baada ya ndoa kupita tulifanikiwa kurejea nyumbani tanzania. Maisha ya ndoa yaliendelea mungu akatujalia tukabahatika kupata watoto watatu. Kama mjuavyo tena ndoa ina raha na karaha, karaha zilizidi nikaona isiwe shida ni kheri kila mtu abaki na hamsini zake. Msingi wa kuandika ujumbe huu ni kwamba baada ya kutengana mwanamke anataka aondoke na watoto wote kitu ambacho binafsi sipo tayari. Baada ya mvutano huo family yake nayo inadai kama nitaendelea na msimamo wangu watanifungulia kesi uhamiaji ya kwamba nilikua naishi na mtoto wao kinyume cha sheria. Ikumbukwe sikufuata taratibu zozote za kuishi na raia wa kigeni, kifupi niseme nilikujanae kwa njia ya panya. Hivyo naomba kujua je sheria inasemaje juu ya hili?.