The Senetor
Member
- Aug 23, 2014
- 41
- 23
Ni hivi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye nilitegemea kumwoa mwaka huu ila alinisaliti na kuniacha baada ya muda nikapata mpenzi mwingine,kwa sasa ni mjamzito na nategemea kuishi nae.Nilipata ajali mwezi wa saba na hii ilipelekea mimi kuacha kazi maana nilikuwa nafanya kampuni binafsi iliyokuwa inanilipa kwa siku,matibabu yamenigharimu na nimepona kabisa.Baada ya kupona nikaamua kutafuta kazi upya maana sina pesa kabisa na bibie anakaa kwao na mimi nipo kwa mjomba maana nilikuwa na hali mbaya baada ya ajali na sijapanga.Ila wiki hii nimepata kazi kwa kampuni moja ya wahindi shida wananilipa pesa kidogo sana basic salary 350,000,nauli 89,000,allowance(pesa ya kodi ya chumba) 52,000,lunch napata job free ila sijakubali kuanza kazi mpaka kesho ndio nitatoa jibu.Wakuu nishaurini maana sina pesa kabisa na bibie sijampa hata kidogo pia mwakani February atajifungua najiuliza nifanye hii kazi au nitafute kwingine mimi elimu yangu ni ya chuo kikuu nahitaji msaada wa mawazo yenu hata ya kupata job mapema