USHAURI WAKO NISIPOTEE

baba mausingizi

Senior Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
189
Reaction score
120
KWELI MCHEPUKO MPYA UNA NGUVU

JOHN:-Habari yako bwana

Baba mausingizi-mzuri we Nani

JOHN:-Natumaini hatufahamiani.

Baba mausingizi:-yes, sikufaham wewe nani nikumbushe..

JOHN:-mimi naitwa mr JOHN au baba Hellen.

Baba mausingizi:-ndio..

JOHN :-Mke wangu ni ANITA ambae kwa sasa ndio mpenzi wako kipenziiii kwa maelezo niliyoyakuta kwenye simu yake.

Baba mausingizi (**kimyaa**)

JOHN :-Leo nakutumia sms hii sio kwa ubaya bali kwa kukupongeza kwa kumbadilisha sana mkewangu.

Baba mausingizi- (**nisamehe bro, nipo mwanza kwa Sasa*)

JOHN:- Usijai Jana nilikuona unavuka barabara, umekutana na mke wangu mmepanda Bajaji Sikujua mlielekea wapi. ..

Baba mausingizi:-(**kimyaa**)

JOHN:-lakini Usijali, kitu ambacho nakupongeza ni kwa kumbadilisha mkewangu.

kitu ambacho hata mapadre na wazazi wake walishindwa.

Baba mausingizi:-(**kimyaa**)

JOHN:-kwa kweli Anita Mke wangu sasa hivi kabadilika sanaaa.
hanywi tena pombe kupitiliza kama hapo mwanzo, hafokei hovyo watoto na kuwapiga kama mwanzo, harudi nyumbani usiku tena. sasa hivi Mke wangu ananipikia na kunifulia.

JOHN:-Unanisikia kaka..

Baba mausingizi-**ndio**

JOHN:-Yaani Nimeshangaa sana. haya mambo niliyasahau muda kutoka kwa mke wangu Anita mpendwa.

Baba mausingizi:-umejuaje bro

JOHN:-Nimejua, Tatizo lilikuwa ni mimi mwenyewe. baada tu ya kunifumania na mwanamke mwengine ndipo mke wangu alibadilika sanaa mpaka nilijuta.

Baba mausingizi:-aliniambia...Pole Sana

JOHN:-Ansante, yaani kila jitihada zilishindikana za kumrudisha awe kama zamani, ikawa inapotokea nashindwa kutimiza haja zake za kimwili kama zamani basi ni ugomviiii, naonekana kama nimemalizia nguvu huko nje.

Baba mausingizi-kwani amebadilika nini?

JOHN:-ndio, Kwa Mabadiliko ya hivi karibuni ndio kitu kimenishangaza mke wangu amekuwa na furaha kama mwanzo, amekuwa mcheshi na watoto. anapika na kufua.

Baba mausingizi:-mbona uwa akija kwangu anafua

JOHN:-Lakini nimegundua sababu kubwa ya mabadiliko haya ni wewe baba mausingizi, toka akupate uwe mchepuko wake amekuwa akikuheshimu sana amekuwa akikusikiliza sanaaa.

nimekuta sms zako nyingi ukimuuliza mke wangu Anita
*umewapikia watoto*?
*Mtunze mmeo mimi wa kupita tu*
*umempikia mme mwenzangu chakula gani*
*ulivyonipa Jana mpe na mzee hivyo hivyo ila usimchoshe*..
*Anita nimenunua Suti na viatu uje kesho uchukue hivyo Kwa ajili ya mmeo*
*msalimie Mhe*
*Anita uko wapi saa hizi muda wa kurudi mumeo, rudi kwako haraka*

Nimefurahi sana kwani nae amekuwa akitii maagizo yako kuliko yangu.

Nimefurahi zaidi kwakuwa hunywi pombe na hivyo hata yeye umemkataza kunywa pombe na ameacha kabisaaa, hata nilizo nunua mimi ili anywe ziko tu kwenye friji.

hataki kabisa kunywa pombe kwakuwa anakuogopa.

Wewe ni wanaume wachache sana ambao hutembea na mke wa mtu na bado akahitaji asiharibu ndoa yake.

yaan wewe kutembea na mke wangu kumeimarisha sana ndoa yangu.

Hata unapomuudhi wewe huwa najua.

maana atashinda hana raha kabisa.
Ahsante sana baba mausingizi

ila ninachokuomba mwambie na mie asinisahau sana kwenye tendo la ndoa.

Baba mausingizi-Sawa nitamwambia....

JOHN :-maana mkiahidiana kukutana wiki ijayo ujue wiki nzima sipewi anakutunziaa.

Baba mausingizi:-Nimekuelewa kaka..

JOHN :-Naomba umwambie hilo.

Baba mausingizi:-aya..

JOHN:-mimi ni mtu mzima.nahitaji kulea wanangu kwa amani zaidi.

Baba mausingizi-ni kweli.

JOHN😛engine nguvu zangu za sasa siwezi mtimizia mahitaji yake ya kimwili.

Bora adui mmoja ninaekujua kuliko akiwa anahangaika ovyo kutafuta kukidhi haja ya mwili wake.

usimwambie Anita kama nimekujua maana atachukia sana na anaweza nuna mwezi mzima..

Baba mausingizi-siwezi kumuambia, ilo nalijua Usiofu Bro..

JOHN:- SIKU NJEMA KAKA TUMPENDE MKE NA AMENIOMBA KESHO TUKUTANE TUPATE KINYWAJI NA KUONGEA VIP NIENDE AU MTEGO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…