Natumai mko salama wapendwa katika Bwana na mnaendelea vyema na shugHuli zenu za kila siku na ujenzi wa taifa hili,Nimehitimu stashahada ya ualimu katika chuo kimoja hapa nchini,kwa bahati mbaya nilifeli vipindi viwili yaani Curriculum na PE (Phsical Education) hivyo sikuweza kuajiriwa ingawa sikufeli vile vipindi vya kufundisha darasani,Baada ya hapo ilinibidi nitafute kazi kwenye hizi taasisi binafsi na kufanikiwa ambako nimefanya kazi kwa takribani miaka miwili na baada ya mambo kuwa mengi na kama mnavyojua kazi hizi za sekta binafsi ilinibidi niache kazi...
Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijiendeleza katika chuo kimoja hapa Dar nasoma Diploma ya mambo IT huku nikijaribu kutafuta kazi ya kufanya ingawa nayo ni ngumu kupata...
Haja yangu kwenu ni kuomba ushauri,Je naweza tokana vipi na hii hali ya ukosefu wa ajira au naweza fanya nini kuepukana na hii hali ninayokumbana nayo kwa sasa