Ushauri wa Msigwa ulipuuzwa.

Ushauri wa Msigwa ulipuuzwa.

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
Wiki iliyopita Mh. Peter Msigwa aliongelea tatizo la Wamachinga wa Iringa.

Alishauri yafuatayo:

1. Serikali ifanye mpango wa kuongea na wamachinga na kupata suluhisho la pamoja. Anasema kuwa Mwanza, Mbeya na Moshi wakuu wa Mikoa walikuwa tayari kuongea na wamachinga wa huko na tatizo lao likatatatuliwa.

2. Alionya juu ya kutumia nguvu za polisi kama suluhisho la suala hili, kwa kuwa hawa ni wananchi wenye shida inayohitaji kutatuliwa, hivyo ni busara wasikilizwe kuliko kutishwa na kuletewa polisi.

3. Alionya kuwa Polisi wanapotumika kuzuia sauti za wamachinga, wanatengeneza mazingira ya wananchi kuchukia serikali yao na kuona inawakandamiza.

Angalia zaidi video hii
 
Last edited by a moderator:
msigwa amepotoka na anakokwenda siko kwenyewe sijui kama ndiyo siasa alizochagua au ndiyo mikakati yake iko hivyo katika uongozi wake,yawezekana yapo kwenye ilani ya chama chake kwani hata lema ni hivyohivyo.
 
Acha upumbavu mkuu, kama umeiangalia hii video kiukweli jamaa amezungumza sio kama Chadema wala CCM bali kama Mtanzania anayeguswa na "dhiki" za watanzania. Si vema katika maisha haya ya dunia always nyeupe kuita nyeusi, kuna ujumbe unasema "Hayakuwa maisha ya dunia ispokuwa ni upuuzi" kwamba iko siku tutapita na kuulizwa yale tuliyoyashuhudia katika macho na nafsi zetu; jiepushe kuita nyeupe kwa nyeusi kwani ww unaona dogo lakini kiukweli si dogo. Alikopotoka kwenye video hii wapi? kwamba machainga si tatizo, kwamba wanasiasa hawawatumii machinga, kwamba utaratibu wa kupiga wananchi unaotumiwa na polisi unasababisha watu wajenge chuki na Taifa lao, kwamba chuki zidi ya seriklai yao ni kupungua kwa uzalendo kwa Taifa lao? Wapi amepotoka huyu. Sipendi sana katika maisha yangu kutetea upuuzi kama ufanyavyo ndugu yangu, siyo vema.
 
msigwa amepotoka na anakokwenda siko kwenyewe sijui kama ndiyo siasa alizochagua au ndiyo mikakati yake iko hivyo katika uongozi wake,yawezekana yapo kwenye ilani ya chama chake kwani hata lema ni hivyohivyo.
Niambie amepotoka nini?

Niambie kama wewe ungekuwa mbunge ungeishauri nini serikali juu ya kutatua tatizo la Wamachinga? Kuwapiga mabomu?
 
Sasa mtu kama huyu anakamatwa na polisi hahahahahahaha. Oh! my Tanzania. Mungu akuondolee kikombe hiki!!!
 
Kuwatuliza wamachinga kwa nguvu siluhisho wala machinga siswala lakisiasa kama wanavyotuambia viongozi wa mkoa
Wairinga ninyi viongozi ivimnajua kujua mizizi ya matatizo nikipaji lakini kutatua matatizo nigarama za kukosa kipaji cha kujua matatizo endelezeni ushabiki wakijinga kwenye maswala ya nguvu yataifa
 
Sasa mtu kama huyu anakamatwa na polisi hahahahahahaha. Oh! my Tanzania. Mungu akuondolee kikombe hiki!!!
Halafu wengine hawaelewi kwa nini CCM inapoteza umaarufu.

Yaani unazima kero za watu kwa kuwapiga mabomu badala ya kuwasikiliza halafu unategemea watu hao hao wakupende!

Solution sio kushinda humu mitandaoni na kupiga propaganda, bali kusikiliza kero za wananchi na walau kuonyesha kuwa mnajali.
 
CCM wanatapatapa....wanatumia nguvu badala ya akili....napendekeza polisi ibadilishwe jina,iitwe idara ya chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom