Ushauri wa masomo ya QT

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
Habari wakuu wanaJF, nahitaji ushauri kwa wajuzi wa jambo hili

Mimi niliishia form 2 nilikatiza shule kutokana ugumu wa maisha ya wazazi wangu hivyo sikubahatika kuendelea na masomo nikaingia kwenye utafutaji wa maisha mtaani sasa nahitaji kujiendeleza kupitia hizi shule za Qt.

Msaada wangu ninaoomba ni masomo gani ambayo huwa wanajifunza kwa mwaka wa kwanza ili nianze kujifunza huku mtaani ili ikifika mwakani panapo uhai nikianza QT iwe rahisi kuanza kupambana juu ya utafutaji wangu wa elimu

Ahsanteni sana kwa watakaonipa moyo na ushauri pia
 
Sikiliza hii story ita kumotivate kidogo kama una nia.

Niliacha shule September 2013 nikiwa form one nikaendelea na Mishe mtaani mambo yalipokuwa magumu mtaani nikarudi shule 2019 kuanza QT but nilijitoa kwa hali na Mali kusoma na nikawa mwanafunzi kweli nikawa nasoma masomo yote kumi 2019 nikafanya paper la QT nika pass 2020 nikajisajili form four nikiwa Naendelea kusoma masomo yote 10, nikafanya paper la form four nikapata division one ya 12 nikifeli hesabu na fizikia kwa kupata "F" pekee huku kemia nikiwa na D na biology C lakini masomo yote ta arts ni A na B pekee sina C kwenye somo la art hata Moja.

2021 nikaanza form five na six kwa Mwaka mmoja nikijisajili kwa kombi ya HGL Mwaka huu mwezi wa tano nikafanya paper nikapata division one ya 8, mpaka muda huu Niko chuo Mwaka wa kwanza na boom juu.

Kwaiyo nimesoma madarasa 6 kwa miaka 3 na Niko chuo kikuu.

Hivyo basi kama uko willing anza kujiandaa kiuchumi na ujitoe hasa kusoma kufaulu inawezekana nimekuwekea matokeo yangu ya sayansi na matokeo yalikua sio poa sana kulingana na mzigo wa masomo mengi niliobeba na ugumu kwa hayo masomo ya sayansi hivyo nikushauri uchukue masomo nane History, English, kiswahil, mathematics, biology, civics, geography na literature.

Kila la kheri.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wa mechanical engineering department (moja kati ya port flan hapa Tz) aliishia form one akawa fundi wa mtaani baada ya life kumchapa akaenda kupiga QT form one to four miaka 2 then akapata devision two then akapiga diploma ya mechanical akaunga degree now tupo nae na kidiploma chake anapush harrier

QT inabidi ujitoe haswa achana na dei waka piga kitabu (soma ukiwa unakaa kwenu au kwa shemeji yako)

Kuhusu usahishaji huwa ni propaganda tu japo ni ngumu kupata A
 
Nenda Katika kituo au center wanazo toa Huduma ya kufundisha watu wa QT na wanao rudia masomo ya kidato Cha Nne , utapa mwongozo mzuri na namna ya ku- Archive dreams zako
 
Mkuu wa mechanical engineering department (moja kati ya port flan hapa Tz) aliishia form one akawa fundi wa mtaani baada ya life kumchapa akaenda kupiga QT form one to four miaka 2 then akapata devision two then akapiga diploma ya mechanical akaunga degree now tupo nae na kidiploma chake anapush harrier

QT inabidi ujitoe haswa achana na dei waka piga kitabu (soma ukiwa unakaa kwenu au kwa shemeji yako)

Kuhusu usahishaji huwa ni propaganda tu japo ni ngumu kupata A
Umemotivate vizuri sana pia "A" inawezekana nina "A" tatu na "B" na ninesoma QT then PC tatu, lakini cha msingi ajitoe haswa.
 
Back
Top Bottom