Ushauri wa mahusiano kwa kutumia wimbo wowote uliowahi kuusikiliza

Ivan Breaker

JF-Expert Member
Jun 13, 2020
1,379
5,488
Habari za leo Wakuu!

Leo nakuja na uzi maalumu kwa wote wanaohitaji ushauri unaohusiana na suala zima la mahusiano, kwa kutumia baadhi ya maneno kutoka kwenye nyimbo za wasanii mbalimbali ( Hasa Wasanii wa HIP HOP )

Kwa kuanza na wimbo wa MWANA FA - Bado Nipo Nipo

Kuna mengi sana ya kujifunza kwa wale ambao wamekuwa wakiteswa na kulilia na mapenzi.

VERSE ya 2

Hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani ?
watu wana watu wao wengine toka zamani
ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako
wadogo usoni wanahifadhi wazee wako
sijui ni dhiki au tamaa tu ?
watoto wanaanika njaa tu
hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu

Msinipe headache staki kufuata Mkumbo
Nyie anzeni mi niacheni, staki kufanya gamble
marafiki wanauzana, ndio zao vicheche
na daima wanateteana, siwaamini usiniangushe

Anataka kuolewa na anamegwa kama kawa
demu wako akiuza wenzake, zinduka nae analiwa YES
Sitaki kuoa sababu sitaki kulia
najipanga nisiharibu sitaki mje kunihurumia
nafahamu nna Bahati mbaya kama nalala na bundi
ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi

Alilala na bibi harusi siku moja kabla ya harusi
na wala sio bwana harusi,
Bado mnanishauri harusi?
Eti nizibe maskio
wengine nifumbe macho
nisione wakati naibiwa?
hamuwezi kuwa hamjalewa

VERSE ya Mwisho

Usiseme unamwamini mwanamke hata kama unamtania
watu na akili zao washajichuuza na wakalia

Sikatazi watu kuoa
na hata nikiwakataza neno langu sio sheria

Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa simu na gari

Inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri
ndio maana mi nipo nipo sitaki kuvamia shari

Wanatoroka na wazungu, wanamegwa na vibabu
wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu

Ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe
au kata mgomba uufiche mtaani usishindaniwe

Wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee
haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume

Kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafkiria?
Sio kila demu umuonae unaweza muoa.



Mstari ambao nimekuwa nikiishi nao siku zote na ninauelewa nao vilivyo na haujawahi kunisaliti ni huu

" UKITAKA WAKO PEKE YAKO LABDA UMUUMBE MWENYEWE AU KATA MGOMBA UUFICHE MTAANI USISHINDANIWE

WAKIKUMEGEA DEMU WAKO NAWE TAFUTA MNYONGE UMMEGEE HAIPUNGUZI MAUMIVU INARUDISHA HADHI YA KIUME, KUMEGEWA NI JAMBO MOJA KUKIMBIWA USHAFIKIRIA? "

Dondosha ushauri wako chini usaidie kizazi cha sasa kinachoteswa na mapenzi, kwa kutumia wimbo wowote uliowahi kuusikiliza.

Karibuni!
 
Sijui ndo anaitwa Pass- memories hyo nyimbo c mimi wala yeye..huwa akiiskiliza lazma anitafute na kunieleze vile tulikuwa tume deep down ila ss iv kila mtu na yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom