masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Jiji la Dar es salaam linaendelea kukua kwa kasi ambayo imeweka rekodi si tu Afrika bali Duniani.
Halmashauri ya Jiji na Tume zake za Mipango Miji zimelemewa kabisa namna ya kudhibiti maendeleo ya Jiji letu la DSM, Jiji ambalo kama lingepangwa lingekuwa la mfano Barani Afrika.
Kutokana na Bomoa bomoa inayoendelea , ni wazi kuwa upande mmoja ni wa wananchi wnaojichukulia hatua zao wenyewe za kimaendeleo na upande wa pili ni Serkali inayoamka kila baada ya miaka mitani toka usingizi wa pono, huku ikiangalia Jiji linavyokua bila mpagilio wowote,
Leo nawapa NEMC/JIJI na hata mamlaka zilizopo sehemu chache tu ambazo zinaweza kushughulikiwa na Jiji linaweza kupendeza.

- Jiji liwe na Mamlaka ya Mito na Mabonde, kama ilivyo barabara. Mito na mabonde haya yalindwe kisheria ili yasivamiwe kwa hali yoyote ile.
- Mto Mkuu wa Msimbazi upate Mamlaka yake. Na mto na bonde hili lichimbwe na kupanuliwa toka Selander Bridge hadi Kigogo. Bonde hili laweza hata kutumika kama njia kuu ya usafiri wa majini. Hili limefanyika nchi nyingi , hata kule Singapore kuna bonde kama la Msimbazi ambalo bila hata kutumia msaada au ujuzi toka nje, wenzetu waliuchimba mkondo ule wa bahari na kuuwekea kina ili hata boti ziweze kuingia ndani ya Jiji na kuboresha mandhari ya Jiji kwa kuweka Sea Front businesses kama restaurants, maduka ya souvenirs na general leisure. Tatizo hapa kwetu wahandisi/viongozi wa Jiji hawawezi kuthink outside the box!! Eneo lote la Msimbazi kuanzia Selander/Upanga hadi Magomeni linaweza kuwa another business district ya kuwaondoa kabisa maachinga mtaa wa Congo!
- Drainage ya Jiji la Dar es salaam ni tatizo dogo sana kwa viongozi wa Jiji ambao watakuwa creative. Jiji linaweza kuchimba mtaro mkubwa sana (kama diameter ya mita 5)wa chini ya ardhi kuanzia pale Jangwani hadi Posta ya Zamani kutokea baharini. Maji yote ya mvua yanaelekezwa humo. Mtaro mwingine mkubwa kama huo wa mita 5 unaanzia sehemu za Upanga na kuishia sehemu za Kariakoo, mtaro huu ukiunganika na ule unaotoka Jangwani. Hapo habari ya mafuriko kati kati ya Jiji kwisha kabisa. Miji yote yenye uendelevu wa kimipango na fikra za utatuzi wa matatizo kama haya duniani yamefanya hivyo.
Last edited: