Ushauri wa kina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa kina

Discussion in 'JF Doctor' started by quimby_joey, Jun 8, 2012.

 1. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  girlfriend wangu ana hali ambayo yeye anashindwa kuielewa, inaweza ikamchukua hadi miezi 3 hadi 6 hajaenda siku zake (bleed) mara ya mwisho kwenda bleed ilikuwa Nov. 2011 hajaziona tena hadi mwezi huu wa sita, je hali hii ni ya kawaida?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Hiyo sio hali ya kawaida mwambie aende Hospitali kumuona Daktari au atumie Dawa moja kati ya Dawa zangu hizi za tiba Mbadala.  DAWA ZA KUTEREMSHA HEDHI.


  Ikiwa hedhi imezuilika kwa kufikia umri wa kumaliza au ni kwasababu ya mimba, inafahamika lakini ikiwa si kwasababu mbili hizo basi hufanyiwa dawa na kuirudisha hedhi.


  1. Kunywa chai ya mdalasini.


  2. Mvuje ukinywewa pamoja na pilipilimanga huteremsha hedhi iliyo fungwa katika uzai au mapito yake.


  3. Manemane ikipondwa na ukinywa siku tatu asubuhi kabla ya kula chakula


  4. Thoum na maganda yake huteremsha hedhi


  5. Kunywa maji yaliyochemsha na zaatari.

  Akisha pata hizo siku zake please give me a Feedback............................................ quimby_joey
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,832
  Trophy Points: 280
  dah! @mzizimkavu umenifurahisha sana. Miye ile therapy uliyonambia kwa mama nilifanya ingawa kwa mwanzoni alikuwa na resist akidai ni uchawi ila nilipomshauri kwa kina she is doing good. kwasasa she can walk ingawa lazima awe na supporting cane but ni much better kuliko alivyokuwa mwanzon.

  yaani weye mtoa mada fanya haya utaona mabadiliko.
   
 4. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35

  asante sana mkuu kwa msaada bila shaka atatekeleza pindi nikishamtaarifu, ila nina swali kidogo, anatakiwa achague kimoja kati ya hivyo hapo juu au anatakiwa atumie vyote kwa pamoja (1-5), na hii MVUJE kwenye namba 2 ni nini....asante mkuu@ mzizimkavu

   
 5. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii hali uwapata watu wanaokaribia menopause, kama umr ni wa kawaida then aende hospital, mi niliwai pitiliza miez 2 nkaenda kwa dokta akasema eti ni normal cz wengne wanaptiliza hadi sita, nashukuru mwez huohuo nilibrid nampaka sasa ivi na hata nikipitiliza ni siku kazaa, kuna dawa mbalmbal za kisayans za kuforce dam itoke, magonjwa kama kisukari na cancer yanaweza sababisha m2 akose hedh, KAMA ALIVOSEMA MZIZI AENDE FANYIWA UCHUNGUZI CZ MIEZ 6 NI MING SANA WANGU.
   
 6. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Asante nimeshampa ushauri wa mzizimkavu na tayari kuanzia leo ameanza dose @Kilahunja

   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  gfsonwin Dawavniliyokupa sio Uchawi muondoshe mama wasiwasi, dawa yoyote ya tiba mbadala inayotibu sio ya Uchawi dawa ya uchawi ni ile inayodhuru watu au hata wew

  mwenyewe inaweza kukudhuru hiyo unaweza kuita ni uchawi au ni dawa ya uchawi. Katika Tiba za kienyeji kuna Dawa a kutibu na kuna Dawa za kudhuru kwa mfano wewe ukiwa unaumwa mtu akwambie unywe nyongo ya mamba ni sumu na

  huyo mtu amekukusudia wewe kukuwa kwani nyonga ya mamba ni sumu kubwa sana kwa hiyo amtu akikwambia utumie

  hiyo nyongo ya Mamba kwa mfano unywe huyo aliyekupa hiyo dawa sio mtu mzuri amekusudia wewe kukuuwa hiyo dawa sasa itakuwa ni uchawi. lakini unaumwa ukaenda mtibabu wa tiba mbadala akakuambia ule chumvi ndio utapona sasa wew utasema kakupa uchawi huo? mfahamishe mam apatekueelewa vizuri asante sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MVUJE ni dawa moja kwa sisi atu wa pwani tunatumia kuwavalisha watoto wadogo wanaolala usiku wakistukastuka kama upo Dares-Salaam nenda madukani karibu na soko kuu la Kariakoo mtaa wa pemba au nyamwezi kwenye maduka ya wauza Ma Dawa wa kipemba kawaulizie watakupa inanuka hiyo dawa harufu mbaya lakini inatibu maradhi mengi tu utaipata hiyo sehemu niliyokwambia inshallah tumia dawa moja kati ya hizo juu nilizokupa.................... quimby_joey
   
 9. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  ameanza kutumia chai ya mdalisini pamoja na kula kitunguu saumu na maganda yake, ntahakikisha anafanya hivyo kwa wiki 1 hadi 2 kisha tuangalie maendeleo yatakavyokua, nitakujuza mkuu......thanks @ Mzizimkavu
   
Loading...