Ushauri wa kichochezi: Rais Magufuli anzisha chama chako na uhame CCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,078
2,000
Umejipambanua kuwa ni mtu tofauti kimaneno na kimatendo. Umekuwa ukisema ukweli na kufuatilia jambo kwa makini, undani na kwa dhati ya moyo wako. Tumekuwa tukikuzongazonga tu kwa manenomaneno pale ambapo unasema 'zaidi' ya yale ya kuyasema.

Hata wewe Rais unajua kuwa CCM ni chama chenye makandokando mengi. Kwakuwa chama ni wanachama, CCM haijawahi kukwepa kashfa zote za kifisadi tabgu kuanzishwa kwake hadi sasa. CCM inahusika na vyote ambavyo sasa unapambana navyo. Kila wakitajwa, ni makada.

Aliyekuwa Rais wa Malawi, Hayati Bingu wa Mutharika alitoa mpya kwa siasa za Afrika. Alichaguliwa Rais kupitia chama kiitwacho United Democratic Front mwaka 2004. Mwaka mmoja tu, mwaka 2005, Hayati Mutharika akaanzisha chama chake cha Democratic Progressive Party na akashinda uchaguzi kwa chama kipya.

Chema chajiuza! Hayati Bingu alihama kwakuwa mtangulizi wake katika Urais, Bakili Muluzi alikuwa akimuingilia katika utendaji wake kupitia uongozi wa Muluzi kwenye UDF. Mutharika alitaka kufanya mambo makubwa bila kuingiliwa.

Kutokana na 'kuchafuka' kwa kutosha na kutisha kwa CCM, nakushauri Rais Magufuli uunde chama chako na kuhama CCM. CCM inakugharimu katika kutenda kwako kwakuwa kila uchao utawakuta wale wale wakiwa wamefanya yale yale. Ndimo utakutana na watu kama Mtemi Chenge. CCM itakulazimu kuilinda.

Kuilinda CCM ni kulinda mabaya yake. Kuilinda CCM ni kupambana kimaneno na kimatendo na wakosoaji wake. Kuilinda CCM ni kuaminisha watu kuwa sasa CCM inajisafisha na 'inatubu' hata kama ni kwa tabu. CCM inakuchafua na inachefua. Walioaminiwa kichama na hata Bungeni ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.

Jambo la busara na lisilo na hasara ni kuanzisha chama chako na kuhama CCM. Wazalendo wenzako tutakufuata huko. Tutakurejesha Ikulu kwa nguvu zaidi na ukiwa unajiamini zaidi kwakuwa hautakuwa na 'urafiki'. CCM, ilipofikia na vinavyoendelea, haisafishiki wala hailindiki. Hata overhaul ni kupoteza nguvu tu.

Hama CCM mzalendo, linda mali za Tanzania yetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,387
2,000
18952999_1336014753161384_8429699997380893310_n.jpg
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386

Kwani Lissu walikuwa AG kwenye serikali ipi Mkuu?Maana naona Mzee kwachukia kweli kweli akisikia tu jina la Lissu ni kama Shetani amesikia jina la Yesu
 
Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,944
2,000
Jambo la busara na lisilo na hasara ni kuanzisha chama chako na kuhama CCM. Wazalendo wenzako tutakufuata huko. Tutakurejesha Ikulu kwa nguvu zaidi na ukiwa unajiamini zaidi kwakuwa hautakuwa na 'urafiki'. CCM, ilipofikia na vinavyoendelea, haisafishiki wala hailindiki. Hata overhaul ni kupoteza nguvu tu.

Hama CCM mzalendo, linda mali za Tanzania yetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Pagumu !.
 
El cholo

JF-Expert Member
Oct 30, 2016
201
500
Mkuu wangu wewe tunakupata kadi ya pipooozz lini? Kwamaana nawewe unasukuma gari wakati umekaa siti ya pembeni kwa dereva.
 
Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,648
2,000
Kwani unafikiria sisi ambao hatukuwapa support ccm 2015 tulikuwa wapumbavu na malofa kama baadhi yao walivyosema? Lowasa sio msafi lakini ilikuwa ni nyenzo pekee ya kuivunja ccm, tupate mawazo mapya ikiwa ni pamoja na katiba mpya.. Maajabu ni kwamba Magufuli anaona watu wote ambao hawakumuunga mkono ni maadui namba moja... Kwa Ccm hii atapiga kelele, atachukia, atakesha usiku na mchana na hakuna ambalo atalifanya likafanikiwa kwa asilimia japo 20
Ccm ni ile ile......
 
nygax

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,086
2,000
Nawaza tu kwamba `chenge atakuwa mgombea uraisi kupitia chadema 2020'
`mawazo kila mtu anamawazo'
 
Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
7,073
2,000
Nakipa jina Chama Cha Wasukuma Tanzania (CCWT)..katibu mwenezi Bashite
 
Pancras Suday

Verified Member
Jun 24, 2011
7,838
2,000
Acha apambane nayo humohumo mpaka ikifika 2020 yenyewe yatakuwa yameiva yalishazoea vya dezo sasa yakione cha mtema kuni
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Sio kwa kuwa ni home boy mkuu.
Usikute Mtemi ni more patriotic kuliko tunavyodhani.
Ili tuende vizuri ulinzi kwa Mtemi uimalishwe.

Hata Mkapa na JK nao ni wazalendo sana tu,wasio wazalendo ni wale waliopinga hizi sheria na mikataba mibovu17 yrs ago
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Kwani unafikiria sisi ambao hatukuwapa support ccm 2015 tulikuwa wapumbavu na malofa kama baadhi yao walivyosema? Lowasa sio msafi lakini ilikuwa ni nyenzo pekee ya kuivunja ccm, tupate mawazo mapya ikiwa ni pamoja na katiba mpya.. Maajabu ni kwamba Magufuli anaona watu wote ambao hawakumuunga mkono ni maadui namba moja... Kwa Ccm hii atapiga kelele, atachukia, atakesha usiku na mchana na hakuna ambalo atalifanya likafanikiwa kwa asilimia japo 20
Ccm ni ile ile......

Hotuba nzima 60% habari za Lissu,pathetic
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom