Ushauri wa haraka kwa chama cha mapinduzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa haraka kwa chama cha mapinduzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Nov 6, 2011.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni jambo lililo wazi kuwa kuna chuki kubwa inayoendelea kuenezwa kuhusu chama cha mapinduzi.
  Hata pale ambapo chama kimeshinda uchaguzi wako wanaobeza na kusema hakikushinda kwa kupendwa bali ni pesa yao imependwa . Ujanja wao umefanikisha.
  Leo mwandishi mmoja aliandika “ Kichwa kama CCM” wengine tumechukulia kuwa ana maana kuitwa CCM ni tusi.
  Amenikumbusha mama mmoja siku moja Hotelini jioni akiwa na watoto wake, watoto walikuwa wakisumbua na kutoka toka kwa kwenda kwenye giza nje. Mama yao alipofikiria njia ya kuwatisha ili wasiende nje aliwaambia “ Nyie njoni haraka CCM watawachukua” Wale watoto wakarudi haraka wanakimbia.
  Tuliosikia tulicheka kisha tukamwuliza kwa nini watoto wamerudi haraka kwa neno hilo. Akasema nataka watoto wangu wakue wakijua kuwa CCM ni kitu kibaya.
  USHAURI WA HARAKA
  Kutokana na hayo hapo juu utagundua kuwa chuki ni kubwa na tunakoelekea ni hatari. Ni jambo lisiloeleweka kuona bado pamoja na dalili hizi serikali ya CCM imeendelea kuwakumbatia wenye tuhuma za ufisadi na haijulikani msimamo wa chama ni upi?
  Bado polisi wameendeleza vitendo vya uonevu na kuacha misingi ya haki na usawa mbele ya sheria.
  Nashauri hatua za haraka za kuamua kimoja kuwa ufisadi ndio sera au kuupinga ndio sera zenu.
  Ni muhimu kuacha kuingilia upinzani na kiuwabughudhi kila kukicha.
  KWA KUZINGATIA CHUKI INAYOONGEZEKA KILA SIKU NI MUHIMU:
  Ni muhimu kuchukua hatua za haraka kukomesha uonevu, ubadhirifu na kuzingatia haki. Kila hatua kwa sasa iwe inafanywa kwa uangalifu. GHADDAFI HAKUJUA INGEISHIA ILIVYOISHIA, MISRI HAWAKUJUA. SYRIA HAWAKUJUA. Nashauri mbadilike haraka na kukemea wote wale ambao wanaharibu picha ya serikali na chama chake.
   
 2. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha,uncle wangu aliniomba kitu,nikamwambia ntakuletea baadaye.Kisha akaniambia,"uncle usiwe mwongo kama Ccm"
   
 3. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sikio la kufa.
   
 4. d

  december Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani magamba wamesikia!!
   
 5. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  ....watasikiaje wakati magamba yameishia kiunoni
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo linachekesha ila kwa kweli kuna haja ya wao kuona hatua za haraka za kuchukua.
   
 7. r

  raffiki Senior Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  kaka naungana na wewe kabisa..asilimia 100,kweli CCM ndio amani nchini kwetu. Tunaomba sana fanyenyi shughuli acheni malumbano urais huo ni majaliwa.....kwanza amani. Mfano hili la lema si vibaya kiongozi wa serikali hata wa mkoa akasema waachane nae bwana...we umati wa watu ukianza kukusanyka hiyo sio vizuri kwa mstakabali wa nchi...chuki inaanza kujengeka tena sana..itafikia hata watu wanaoipenda CCM wakaona kuwa wapinzani wanaonewa dawa ya vitu visivyo vya msingi ni kupuuza. Tukumbuke maneno ya baba wa taifa alisema..,nanukuu kipindi mrema anabebwaaaa...!alisema kuna watu wanapenda sana kubebwa,na kuna watu wanapenda sana kumbeba,waachani wafanye hivyo..na mwisho wake kila mtu anajua. CCM let us be careful
   
 8. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye Bold ni kweli kuwa serikali ilikuwa imepiga marufuku kumbeba Mrema au kusukuma gari lake.
  Baada ya Nyerere kusema hivyo kubebwa kwa Mrema kulipungua. Ikumbukwe kuwa viongozi wa vijana CCM waliandamana na kufanya mkutano usiokuwa na kibali. Kila mtu alilijua hilo hivyo unapokuwa una doubler standard unakosa moral authority ya kukemea kosa lile lile uliloliachia likatendeka.

  Kwa nini wasiwaache wanaotaka kuandamana kwa amani waandamane na wapewe ulinzi?
   
Loading...