JOSE KASANO
Senior Member
- Apr 23, 2013
- 122
- 95
Za majukumu wakuu,
Msaada wa taratibu za kisheria,
Wadau poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa na ya kuelimisha umma kwa masuala ya kisheria.
Samahani nawaombeni msaada wa taratibu za sheria za kazi.Kuna jamaa walikuwa wanafanya kazi katika taasisi fulani binafsi lakini wakawa wamekumbana na kadhia kubwa na mazingira magumu ya kazi katika taasisi hiyo hali iliyopelekea kuacha kazi katika taasisi hiyo.Vilevile wanakusudia kufungua mashtaka dhidi ya mwajiri wa taasisi hiyo kutokana juhuma mbalimbali ambazo amekuwa akiwafnyia wafanyakazi wake zinazokinzana na taratibu za kazi na sheria za kazi. Baadhi ya mazingira ama hujuma ambazo mwajiri huyo amekuwa akiwafanyia wafanyakazi wake ni pamoja na:
1. Mwajiri kuondoa kipengele cha gratuity kwenye mikataba ya wafanyakazi bila wafanyakazi kutaarifiwa ama kuridhia
juu ya uondoaji wa kipengele hicho muhimu kinachowakosesha haki ya kulipwa baada ya kumaliza mikataba.
2. Mwajiri kukataa wafanyakazi wasichangie kwenye mifuko ya hifadhi ya kijamii kama LAPF ,NSSF, PSPF n.k licha ya mikataba kuwa na vipengele hivyo.
3. Mwajiri kuwafanyisha kazi za ziada wafanyakazi baada ya muda wa kazi na nyingine zikiwa nje ya kituo cha
zinazofanyika hadi usiku kisha kuwadhulumu malipo ya kazi hizo.
4. Mwajiri kutowasikiliza wafanyakazi wake pale wanapokuwa na shida ama matatizo kama kuugua, kuuguza, kufiwa
n.k
5. Mwajiri kufanya hujuma kwa baadhi ya wafanyakazi wachache kuonesha kwamba anawachangia kwenye mifuko ya hifadhi ya kijamii kwa kutumia sehemu ndogo ya mishahara yao. Yaani kama mfanyakazi analipwa 500,000 kwa mujibu wa mkataba basi mwajiri anatenga mshahara huo kuonesha 200,000 kuwa ndio mshahara na 300,000 ni posho halafu kwenye uchangiaji wanahesabu 200,000 za mshahara.Kwa ujumla hizi ni hujuma mbaya inayowakosesha haki baadhi ya wafanyakazi hao licha ya kupigia kelele jambo hilo ila wameambulia vitisho.
6. Mwajiri kulipa mishahara bila kutoa salary slip jambo linaloathiri wafanyakazi kuweza kupata haki zingine vyanzo vingine za kuongeza kipato kama mikopo. Mishahara wakati mwingine inalipwa mikononi wakati watu wana mikataba na akaunt za benki.
7.Mwajiri kutowalipa wafanyakazi malipo halali kulingana na kazi wanazofanya na makubaliano kwa kigezo kuwa
hawana pa kwenda na hawawezi kumfanya lolote.
Kutokana na matatizo hayo pamoja na hujuma zinazofanyika na nyingi zikionesha mwajiri kukiuka mikataba aliyosainiana na wafanyakazi bila kuwashirikisha baadhi ya wafanyakazi wameamua kuacha kazi katika taasisi hiyo.
Pamoja na kuacha kazi wanakusudia kumfungulia mashtaka kwa hujuma ambazo ziko wazi na wana ushahidi wa hujuma hizo ikiwemo kumdai fedha zao halali ambazo wamekuwa wakidai bila mafanikio.
Wadau mnaombwa ushauri wa kisheria hususani uhalali wa mashataka, aina ya mashtaka na upatikanaji wa mawakili wa kusaidia kusimamia mashtaka husika.