Ushauri wa bure kwa 'Rockstar' Ali Kiba

Tarishi

Senior Member
May 9, 2008
103
133
Awali ya yote naomba nitangaze "mahaba" yangu (decralation of interest) kwa mwanamuziki nyota nchini Ali Kiba, kwamba mimi ni mshabiki wako wa kutupwa. una sauti nzuri, una kipaji cha hali ya juu, una jina Tanzania, Afika Mashariki, Afrika na duniani kote. Hiyo haina ubishi. Hivyo nisemayo hapa hayahusiani na hujuma ama ushabiki wa aina yoyote. Bali ni hasira tu. Naomba unisamehe kama nitakukwaza. Cos I feel you buddy!

Nimesukumwa kusema haya baada ya kuperuzi mtandaoni na kukuta picha yako hii Ali Kiba ukiwa na Diamond. Nikasema woow! (japo body language haisemi hivyo) na kufurahi kwamba kumbe mmeshawahi kukutana. Nilifurahi sana.

Hata hivyo, furaha yangu hiyo ikawa fupi (short lived) nikivuta kumbukumbu ya mambo kibao katika fani yenu nyie wawili (ninayoifananisha kama Yanga na Simba vile - najua Diamond ni Simba kindakindaki, hivyo bila shaka we Ali ni wa mitaa ya Twiga na Jangwani - aka Kaunda Stadium) maana mpo kama hampo vile.

Kama hizo kumbukumbu zangu haziko mbumbumbu kama nilivyo, hadi naandika haya nadhani kama ni mechi mabao ni 6-0, na Diamond ndiye mshindi. Yaani kila niamkapo nategemea Ali unafanya mashambulizi dhidi ya mpinzani wako Diamond, nakuta patupu. Yaani wewe umekuwa adimu mno katika tasnia wakati mwenzako kila uchao anakuja na ngoma mpya, tena sio ngoma tu bali NGOMA KALI.

Kumbukumbu zangu mbumbumbu zinaniambia kwamba umewahi kunukuliwa ukisema ukimya huamsha hisia. Yaani unajifanya Michael Jackson kwa kutoa kibao kimoja baada ya kingine kwa msimu, na kwamba kutoa vibao kila mara sio dili. Kaka Ali nakupa point blank kwamba hapo umenoa. Yaani ukisubiri siku kibao ndio utoe kitu kwa kujiamini utakubalika kwa mgongo wa kuwa wewe ni "Rockstar" kaa ukijua unakosea. Unatukosea mashabiki wako KAKA!! Tunahitaji vitu kila mara ili tujue ukio hai na fiti. Hayo mambo ya kuiga kina Beyonce na Jay Z (yaani hata kwenye insta huja-follow mtu kwa staili yao hao ni ujuha). Siku hazigandi KAKA ALI. Umwinyi, Ujuaji na kujiona uko juu vitakuzamisha! Piga kazi baba! Sie mashabiki zako tunategemea ukija kwenye show uje na jioya sio na ma "dusherere" na kubweka kama mbweha kila uchao.

Ona mwenzio Diamond anavyowika. Yeye ni mega star kama wewe lakini hategemei kubebwa na historia ya "ALIKUWA" (has been) kwa kutegemea nyota zilipendwa. Ona sasa ngoma yako latest ya "Mvumo wa Radi" ilivyododa. Hiyo ni bonge moja la ngoma lakini imepitwa na wakati. Najua una producer kabambe nchini (Man Water) lakini maudhui ya ngoma hiyo ni two years old! Wakati mwenzio Diamond kaibuka na vitu vya moto kibao ikiwemo hii ya "Baila" aliyo-shoot London, wakati wewe una ngoma kali kuliko hiyo/hizo ambazo hutaki kuzitoa eti kisa hutaki kumwaga lazi kila mara, Ujuha huo Ali Kiba! AMKA!

Sie mashabiki wako tumeshachoka na masebene yako ya "Dusherere" na tunataka utoke upya kila mara udhihirishe u "Rockstar" wako bhana! Hayo mapicha kwenye insta ya kuonesha fashion za mkeo na kujirusha na meneja wako Seven havisaidii kitu. Unatakiwa baada ya ndoa yako hata wakwezo wa Mombasa wajue kweli wana mkwe Star na sio bishoo wa kuishia kwenye Insta kuonesha leo umeenda wapi na mkeo kavaa nini. Huo ni UJUHA kaka. Piga kazi utuliwaze mashabiki zako!!!!!

Naomba nimalizie kwa kukupa ushauri wa bure: Acha nyodo, siku hazigandi, piga kazi, lete mambo mapya ili tujue kuwa naam! tunayemshabikia ana uwezo. Sio kuuza sura na makanzu yako (yanaboa!) huku ukitembelea nyota yako zilipendwa. Yaani unatakiwa utengeneze vitu na kuvimwaga hapo hapo. Kama ushauri huu utaupuuza basi jiandae kuanguka maana kila mtu nchini na nje anakuona wewe ni mtu wa makidai, mtu wa nyodo, usieambilika na juu ya yote unadhani yale ya kale yaliyokupaisha yatadumu. Acha ujuha wa Kiswahili, PIGA KAZI ionekane. Kazi mpya kaka tunataka kila uchao.

diamond_platnumz_congratulates_ali_kiba_for_the_marriage_h15990_10ec6.png
 
Ukweli ni kuwa alikiba aachane na producer man walter maana ndo anamtengenezea masebene ambayo yanakuja kumuharibia sokoni..angalia alikiba wa nakshinakshi,single boy,sinderela,makmuga ni tofaut na alikiba wa mvumo wa radi..(kwa maoni yangu wadau)
 
Ali alikua anasema hashindani na mtu sisi tukaendelea kusisitiza kua anashindana na Diamond. Muda ukapita anaendelea kubisha na sisi tunaendelea kukazania kua anashindana na Diamond.

Kisha wimbo wa Mvumo Wa Radi ukaja ukatoa bonge la plot twist kwenye historia ya muziki bongo.

The whole time Ali alikua anashindana na FM Academia.
 
Na kwako mleta uzi.

Ngoma kali haipimwi kwa masikio yanapata ladha gani kuusikiliza hupimwa kwa kuangalia umechukua tuzo ngapi, umefanya mauzo kiasi gani na umekaa kwenye chati za aina ipi duniani na namba ipi ilishikwa.

Viewers youtube siyo kipimo.

If na Fall za Davido ndiyo nyimbo zake bora wakati wote (mpaka sasa mwezi wa 7/2018) hata kama masikio yetu yanafurahi kusikiliza Aye, Skelewu au Gobe. Ni kwa vile hizo nyimbo zimefanya mauzo ya platinum, zimekaa kwenye chati nchi zaidi ya mbili na tuzo zimekuja nyingi tu kupitia hizo nyimbo.

Kwa hivyo vipimo halisi at this point wimbo wa Malumbano wa 20% ni bora kuliko wimbo wa Baila, Iyena, Sikomi na Kitu Gani wa Msaga Sumu.

Nitarudi
 
kinacho imbwa na bwana mzee na vitu anavyochezaa kwenye nyimbo zake nyingi ni vitu viwli tofauti kabisa yani sana ni mara mia usikilize audio kuliko uangalie video utatamani kulia na kuhoji hiyo crew yake.
Nawasilisha
 
Samahani,umesema wewe ni shabiki wake??? Sio kwa msuto huo nadhani angekujua angekupiga BAN
 
Awali ya yote naomba nitangaze "mahaba" yangu (decralation of interest) kwa mwanamuziki nyota nchini Ali Kiba, kwamba mimi ni mshabiki wako wa kutupwa. una sauti nzuri, una kipaji cha hali ya juu, una jina Tanzania, Afika Mashariki, Afrika na duniani kote. Hiyo haina ubishi. Hivyo nisemayo hapa hayahusiani na hujuma ama ushabiki wa aina yoyote. Bali ni hasira tu. Naomba unisamehe kama nitakukwaza. Cos I feel you buddy!

Nimesukumwa kusema haya baada ya kuperuzi mtandaoni na kukuta picha yako hii Ali Kiba ukiwa na Diamond. Nikasema woow! (japo body language haisemi hivyo) na kufurahi kwamba kumbe mmeshawahi kukutana. Nilifurahi sana.

Hata hivyo, furaha yangu hiyo ikawa fupi (short lived) nikivuta kumbukumbu ya mambo kibao katika fani yenu nyie wawili (ninayoifananisha kama Yanga na Simba vile - najua Diamond ni Simba kindakindaki, hivyo bila shaka we Ali ni wa mitaa ya Twiga na Jangwani - aka Kaunda Stadium) maana mpo kama hampo vile.

Kama hizo kumbukumbu zangu haziko mbumbumbu kama nilivyo, hadi naandika haya nadhani kama ni mechi mabao ni 6-0, na Diamond ndiye mshindi. Yaani kila niamkapo nategemea Ali unafanya mashambulizi dhidi ya mpinzani wako Diamond, nakuta patupu. Yaani wewe umekuwa adimu mno katika tasnia wakati mwenzako kila uchao anakuja na ngoma mpya, tena sio ngoma tu bali NGOMA KALI.

Kumbukumbu zangu mbumbumbu zinaniambia kwamba umewahi kunukuliwa ukisema ukimya huamsha hisia. Yaani unajifanya Michael Jackson kwa kutoa kibao kimoja baada ya kingine kwa msimu, na kwamba kutoa vibao kila mara sio dili. Kaka Ali nakupa point blank kwamba hapo umenoa. Yaani ukisubiri siku kibao ndio utoe kitu kwa kujiamini utakubalika kwa mgongo wa kuwa wewe ni "Rockstar" kaa ukijua unakosea. Unatukosea mashabiki wako KAKA!! Tunahitaji vitu kila mara ili tujue ukio hai na fiti. Hayo mambo ya kuiga kina Beyonce na Jay Z (yaani hata kwenye insta huja-follow mtu kwa staili yao hao ni ujuha). Siku hazigandi KAKA ALI. Umwinyi, Ujuaji na kujiona uko juu vitakuzamisha! Piga kazi baba! Sie mashabiki zako tunategemea ukija kwenye show uje na jioya sio na ma "dusherere" na kubweka kama mbweha kila uchao.

Ona mwenzio Diamond anavyowika. Yeye ni mega star kama wewe lakini hategemei kubebwa na historia ya "ALIKUWA" (has been) kwa kutegemea nyota zilipendwa. Ona sasa ngoma yako latest ya "Mvumo wa Radi" ilivyododa. Hiyo ni bonge moja la ngoma lakini imepitwa na wakati. Najua una producer kabambe nchini (Man Water) lakini maudhui ya ngoma hiyo ni two years old! Wakati mwenzio Diamond kaibuka na vitu vya moto kibao ikiwemo hii ya "Baila" aliyo-shoot London, wakati wewe una ngoma kali kuliko hiyo/hizo ambazo hutaki kuzitoa eti kisa hutaki kumwaga lazi kila mara, Ujuha huo Ali Kiba! AMKA!

Sie mashabiki wako tumeshachoka na masebene yako ya "Dusherere" na tunataka utoke upya kila mara udhihirishe u "Rockstar" wako bhana! Hayo mapicha kwenye insta ya kuonesha fashion za mkeo na kujirusha na meneja wako Seven havisaidii kitu. Unatakiwa baada ya ndoa yako hata wakwezo wa Mombasa wajue kweli wana mkwe Star na sio bishoo wa kuishia kwenye Insta kuonesha leo umeenda wapi na mkeo kavaa nini. Huo ni UJUHA kaka. Piga kazi utuliwaze mashabiki zako!!!!!

Naomba nimalizie kwa kukupa ushauri wa bure: Acha nyodo, siku hazigandi, piga kazi, lete mambo mapya ili tujue kuwa naam! tunayemshabikia ana uwezo. Sio kuuza sura na makanzu yako (yanaboa!) huku ukitembelea nyota yako zilipendwa. Yaani unatakiwa utengeneze vitu na kuvimwaga hapo hapo. Kama ushauri huu utaupuuza basi jiandae kuanguka maana kila mtu nchini na nje anakuona wewe ni mtu wa makidai, mtu wa nyodo, usieambilika na juu ya yote unadhani yale ya kale yaliyokupaisha yatadumu. Acha ujuha wa Kiswahili, PIGA KAZI ionekane. Kazi mpya kaka tunataka kila uchao.

View attachment 810306
Kama kuna mtu amesoma huu uzi mwisho anisimulie tafadhali....halafu mtoa mada hiyo ni fotoshopu sio Diamond huyo ni Neyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom