Ni ajabu na kweli kuwa katika barabara hii polisi wamejizatiti na vi tochi kudhibiti mwendo na eti kuwa sasa hivi wako katika wiki ya nenda kwa usalama kukagua magari na hata kuthubutu kutoza mafaini magari yapitayo njia hii.
Tuwe fair serikali ilipaswa kufikishwa mahakamani kuwalipa fidia wote wanaopitisha magari yao katika njia hii huku wakilipa kodi zote stahili. Kuna haja gani ya kukagua magari kwenye njia yenye mashimo mashimo yenye ukubwa wa kushangaza katikati ya njia, labda kama ni kukagua ili kuthibitisha kuwa kweli kwa barabara kama ilivyo hakika yatakuwa yameharibika. Ukaguzi upi sasa? Wiki ipi ya usalama barabarani? Acheni ubabaishaji, shaurini barabara kutengenezwa kwanza kabla ya kuendekeza kuona vibanzi machoni pa wenzenu.
Tunakoelekea sasa ni kwenye mvua nyingi tu. Barabara kama iliyo kwenye hii clip itakuwa na tija gani kwa mwenye gari au mwenye kusafiri katika njia hii?
Wekezeni kwenye kutoa boriti kwenye macho yenu kabla ya kushadadia vibanzi kwenye macho ya wenzenu kimagumashi magumashi kumbe lengo lenu halisi ni pesa wala si usalama wa raia. Mengine yote kumbe ni machozi ya mamba tu hali kinachotafutwa ni kufikisha malengo ya faini mlizojiwekea ili mkajinufaishe wenyewe binafsi kwa mgongo wa serikali.
Angalia clip hii yenye hali ya ujumla ya barabara hii Benaco Nyakanazi yapata 90km.
Pathetic!
Pia soma; Sasa barabara ya Lusahunga – Rusumo yenye urefu wa kilomita 92, kujengwa kwa Bilioni 153