kikurajembe Original 2015
Senior Member
- Feb 27, 2016
- 109
- 138
Wanajamvi
Poleni na majukumu ya kilasiku ya utafutaji wa rizki. Kama ninakosea basi mtanirekebisha lakini napenda kutoa ushauri wa bure kwa kijana mwenzetu Hamfrey Polepole. Leo katika taarifa ya habari ya ITV iliyosomwa na Dada yetu Neema Kindole. Tumemuona kaka yetu bado anatuaminisha kuwa yeye ni mwanachama na kada maarufu wa chama Fulani kwa kuvaa sare za chama hicho mpaka msibani. Hilo hatukatai.
Lakini afahamu kuwa taarifa za yeye kuwa katibu wa itikadi na enezi wa chama chetu kikongwe chenye rangi ya njano na kijani zilitangazwa hadharani kwenye media nchi nzima. Hivyo anafahamika ni nani na siyo rahisi kubadilishwa ama watu kumsahau.
Aidha kwakuwa Polepole huyo huyo alizunguka nchi nzima kwa wananchi kipindi cha kukusanya maoni ya rasimu ya katiba ya nchi alipata kufahamika sana na alipata umashuhuri sana kabla ya uchaguzi juu ya msimamo wake wa wazi wazi akisema yeye ni muumini wa serikali ... na pia kusisitiza haungi mkono katiba "P........zwa" na alisema yeye hana chama ni "MWANAHARAKATI" nadhani tuliowahi kuhudhuria pale Ubungo plaza mnaelewa ninachoongea.
Ni muda mfupi tu kampeni zilipoanza Ch.10 na kaka yetu "the king" alipokuwa akimleta LIVE katika MADA MOTO ndiyo tulipoanza kuona maajabu ya nchi yetu Tanzania mwanaharakati asiye na chama kupambana na watu kama wakina Mch.Msigwa ambao walikuwa na vyama na walijulikana na jamii yetu na watanzania wote kuwa ni wanachama wa chama Fulani. Hapo ch.10 ndiyo kila kitu kilisemwa na matokeo ya uwana harakati usiofungamana na upande wowote tumeuona.
Haikutosha kuwa mkuu wa wilaya yetu ya Ubungo bali pia kwa sasa nimsemaji wa chama chetu pendwa na kikongwe cha kijani na njano.
Tunajiuliza Maswali;
1. Je kumbe wakati akitueleza ndg zake kuwa yeye ni mwanaharakati huru hana chama, alikuwa akitudanganya na kwamba alikuwa na kadi ya chama? au alipewa akikaribia kuteuliwa nafasi ya ukuu wa wilaya?
2.Kama ni mgeni kwenye chama Je ameshapewa maelekezo juu ya uvaaji wa sare za chama?Unapovaa sare ya chama Fulani cha siasa unaashiria uwepo wa shughuli za kisiasa za chama hicho mahali hapo officially.Hata kama hujasema kitu uvaaji wa sare ni siasa na kampeni tosha. Na pia ni kama kujitangaza kwa vazi rasmi la chama whichi is totally politics.
Watu wana sympasy na mpendwa wao halafu wengine wanaibuka na sare za chama. Jamani siasa mpaka msibani je kama kila chama nao wangevaa sare zao hivi pale msibani ingekuwa ni uwanja wa siasa na kampeni zimeanza? Mbona mtangulizi wake wa nafasi hiyo alikuwa havai kwenye misiba? Basi kaka mtangulizi tunaomba usikabidhi office tu ukaondoka rudi ukajaribu kutoa muongoza kwa yale mazuri uliyoyafanya.
Huo ndiyo ushauri wangu kwa kaka yangu mpendwa H.Polepole aliyekuwa mwanaharakati huru asiye na chama mpaka mwezi Sept..2015. Ukisikia yupo ubungo plaza na team yake ya MHE.JUDGE WARIOBA, MHE.BUTIKU, MWANSHERIA WA ZANZIBAR, PROF.PALAMAGAMBA KABUDU, huwezi kukosa labda unaumwa na ukikosa mdahalo wao kwenda basi siku hiyo hapo nyumbani hata mechi ya Man utd vs Arsenal ama Liverpool vs Chelsea ama Elclasico Ch.no. 203 / 207 DSTV, huwezi kuangalia utangoja uone zamu ya kijana wetu mpendwa na mwanaharakati huru H.Polepole akipanda jukwaani na kupewa mic atoe madini.
Na kwa wote wenye vyama vyao tunapenda muhudhurie maziko au misiba ya ndugu zetu lakini sare za vyama vyenu hukohuko getini labda iwe imetangazwa rasmi kwa malengo ya kisiasa. Mnatuumiza msibani sio jukwaa la kisiasa. Kwani ukisema umetumwa namwenyekiti wako kumuwakilisha ukiwa umevaa kaunda suti yako black au any color kunashida gani?
Wikiend njema
Source: ITV