Elections 2010 Ushauri wa bure kwa ndugu zangu watanzania

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Habari zenu mabibi na bwana, pole sana kwa mihangaiko ya kusaka mkate wa kila siku. Napenda kuchukua fursa hii kuwapeni ushauri wa bure kabisa. Ushauri ambao utatusaidia sisi sote na vizazi vyetu, ushauri ambao hauhitaji mtu kwenda chuo na kuchukua degree ili aukubali.

Ikiwa zisalia siku tatu ili kupiga kura napenda ku point out tatizo kubwa linaloikumba nchi yetu nalo ni UCHUMI uliozorota na kusababisha maisha kuwa magumu kwa watanzania. Basi kama tunakubaliana kuwa Tanzania tatizo kubwa ni uchumi nadhani haihitaji darubini kujua katika wagomea urais yupo ni gwiji wa masuala ya uchumi na atakuwa mwarubaini wa tatizo la UCHUMI.

Sidhani kama Tanzania inahitaji wanasiasa wanao ongea sanaaaaa au waotukana wenzao sanaaaa. Vi vema tukajijua tuna matatizo gani ili tuweze kujikwamua na sio kushabikia wanasiasa wanaoongea mpaka povu za mdomo zinawatoka.

Fanyeni maauzi sahihi kumpatia kura zenu za ndio mgombea mwenye ueledi wa masuala ya uchumi, mchumi aliebobea kwenye maswala ya uchumi kwa ngazi ya kimataifa.

Shukran sana nadhani mtakuwa mmenielewa.

Msikose kumsikiliza Prof Ibrahim Lipumba ITV leo muone jinsi watu walivyojipanga kisera na kiakili.
 
Kwa mliopo majumbani anagalieni TBC 1 mpate kusikiliza sera za CUF mpate kumsikia Prof Lipumba
 
Back
Top Bottom