Ushauri wa bure Kwa kafulila!!

Ni moja kati ya watu wa hovyo waliopo
 
Yani alipe watu wanaotumia huu mtandao ili iweje?

Mtandao mtaani kwangu kote huenda naujua mimi tu ndo alipe ma anonymous ili wa waambie nini ma anonymous
🙌🏾🙌🏾🙌🏾
 
Anajaribu kuwa relavant mzee.
Inadhani asipomantain hiyo status atakula wapi?
Huku kwetu watu wanaamini kwamba Siasa maana yake ni Uongo uongo unaofanana na Ukweli 😳🙌 !
Wanasiasa wengi wanaamini hivyo pia !
 
Hoja zake ni zipi na zako wewe za kumpundua ni zipi?!!!!
Kuna kipindi chochote au nchi yoyote unayoijua ambayo wananchi wake wote Wana uwezo wa kulipa ada na kujihudumia matibabu mazuri?!!!!! Chadema bhana, mtu akishawahama tu basi hawaishi kumsakama.
 
Kuna kipindi chochote au nchi yoyote unayoijua ambayo wananchi wake wote Wana uwezo wa kulipa ada na kujihudumia matibabu mazuri?!!!
Kuna mahali nimeandika wananchi wote? Sina huo uwendawazimu wa kudhani watanzania wote wana huo uwezo lakini angalau 90% ya watanzania wanatakiwa wawe na hakika ya maisha bora.
 
Unaruhusiwa na wala huvunji sheria kuamini unachoamini na hulazimishwi kuchukua kila unachosoma humu! Ndio uhuru wenyewe
Chief hata kama nina ufahamu mdogo ila hili haliniingii akilini yani watu wa humu walipwe kueneza propaganda kwa ajili ya audience kama mimi au? 😂😂

Over my dead body Kafulila atunze tu hizo pesa tukalewee, humu kama anailipa taasisi yenyewe ni sawa maana Ina wafuasi wengi nje hata ya hapa.

Anyway ni maoni ya msukuma tu kutoka Ikulwa,Geita
 
Matendo yake ni kama vile mtu umechomwa na mwiba halafu mtu mwingine ndiye ajipe haki ya kutafsiri kiwango cha maumivu unayopitia.

Watu kila siku umaskini wao unawaongezekea yeye yupo bize kusema maisha ni mazuri kuliko miaka iliyopita.
Unamkumbuka Kafulila wa miaka 10 iliyopita???
Yule ndo alikuwa mtu timamu wa kumsikiliza.
Huyu wa saizi ukimsikiliza ni "at your own expense "
 
Bora angekuwa anajibu wananchi sababu ya kushindwa kuwa na viwanda nchini vya chuma wakati madini hayo tunanayo na nishati ya makaa ya Mawe pia tunayo.yeye amekazana kusema uchumi himilivu kwenye karatasi
 
Bora angekuwa anajibu wananchi sababu ya kushindwa kuwa na viwanda nchini vya chuma wakati madini hayo tunanayo na nishati ya makaa ya Mawe pia tunayo.yeye amekazana kusema uchumi himilivu kwenye karatasi
Uchumi himilivu Kwa daraja/kiwango kipi?

Maana labda ni himilivu kwenye kukopesheka kwenye taasisi za kimataifa. Lakini huku mtaani uchumi wetu una uwezo wa kuhimili kuendesha maisha yetu ya Kila siku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…