Ushauri wa bure kwa chadema/makamanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa chadema/makamanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by UNO, Sep 7, 2012.

 1. U

  UNO Senior Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siyo siri kuwa Mwenyekiti wa CDM Mh. Freeman Mbowe ameweza kuongoza chama kwa uweledi mkubwa hasa ukizingatia kwamba chama kina vijana wengi katika uongozi ambao wana mitazamo tofauti na ambao wangependa mambo yafanyike kwa kasi kwa kadri wanavyofikiri. Tunampongeza kwa hilo. Hata hivyo ningependa kutoa ushauri kidogo. Mnaweza kuuchukua au msiuchukue. Ni vizuri kuelewa kwamba watu wanatofautiana ki mtazamo na si lazima au siyo rahisi tukawa na fikra sawa. Ni muhimu basi, kama chama cha demokrasia mkavumiliana au kuheshimu mawazo ambayo ni tofauti na ya kwako. Pia, ningependa kusema kuwa, hakuna mtu ni "perfect". Kila mtu ana madhaifu (weaknesses) na mazuri (strengths) yake. Ni vizuri kulenga kwenye mazuri na kusahau madhaifu, kwa hivyo mtaweza kujenga umoja na chama chenye nguvu. Ninaamini kwamba; kila mtu amekuwa na mchango kwa hapo chama kilipofika. Kwa hivyo basi lenga kwenye mazuri ya kila mtu mtafika mbali. Kama kuna kukosoana ifanyike kwa hekima. Na nina amini viongozi wa juu wa CDM wana hekima kubwa. Hawakurupuki.

  Nawaasa vilevile wale walio na mitazamo tofauti. Ni vizuri kila mara mfikie "win -win situation". Badala ya upande mmoja kupoteza ("win - loose situation"). Na kama kila mara wewe utajiona au utajikuta uko tofauti na wenzako kimsimambo, lazima kutakuwa na tatizo. Tafuta njia ya kurekebisha. Mimi naamini mnahitajiana wote na kila mtu ana mchango.

  Nawakilisha.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Nimekusikia
  Ila sijajua unalenga kitu gani hasa, ungetoa mfano labda ningeelewa zaidi.

  Ila kumbuka, masuluhisho ya aina yote ni masuluhisho
  Unaweza chagua win-win situation au win-lose situation kutegemeana na tukio hilo.

  Kuna saa mapungufu ya mtu yanakuwa makubwa sana ukilinganisha na mazuri yake, hapo lazima niangalie win-lose situation.

  Hebu funguka zaidi basi. . .
   
 3. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  MBONA IVO VYTE VIPO KAKA pale si pa vilaza kama huko cc.
   
 4. e

  ezra1504 Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu unamaanisha nini mbona hueleweki? Kwani kuna kutosikilizana au kuheshimiana ndani ya chama? Funguka basi!
   
 5. u

  umumura Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  unawakilisha au unawasilisha?? Hueleweki! japo kwa maneno yako, tunambua kiwango cha ufahamu wako. am sorry!
   
 6. U

  UNO Senior Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakupata yote hayo yapimwe
   
 7. U

  UNO Senior Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I hope umeelewa mkuu
   
 8. U

  UNO Senior Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haiwezekani huelewi. Chama chochote (including CDM) kilicho na watu wenye fikra pevu, walio na mitazamo tofauti jinsi ya kufikia uamuzi au kutatua matatizo kuna wakati watatofautiana. That's my point.
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Hapokwenye red pamenivuta hisia...kuna wing halafu umoja.Kipi kimekuponyoka?Kama umoja basi ni wazi una mlenga Mbowe.Buwe ni mtu mmoja napenda sana watu open minded tangu akiwa mtoto.Ndio maana watu waliokuwa karibu naye na wenye akili walifanikiwa.Ila wajinga wajinga wanaangalia pafupi na kujikita kubomoa hakuwafumilia sana.
   
 10. U

  UNO Senior Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wewe tunambua ni nini???
   
 11. m

  mwakitundilo Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si useme tu umetumwa na zzk
   
 12. t

  tenende JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo?!
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nadhani kuna kiongozi anajirudi anaona keshatengwa kutokana na misimamo yake isiyo ya kichama na sasa anatumia watu, cha muhimu ni yeye kubadilika na kuomba radhi na kisha kushiriki kwenye kukijenga chama na wala sio kuleta hoja ya kulialia mbele za watu
   
 14. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  This one sounds like Zitto!!

  Anayajua madhambi yake kwa CDM, kwa hiyo anajaribu kujitetea indirectly!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...