Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,150
- 18,811
Wengi huamini chama tawala ndo dola yenyewe na kwa hili; wote walioko madarakani na wapinzani huona hivyo. Ndo maana unaona kuwa mara nyingi vyama vya upinzani vimekuwa vikijiweka katika nafasi ambapo vinaonesha kuwa dola ni sehemu ya Chama tawala.
Hapo si kweli Mkuu. Kama kuna mtu anayefanya kosa kuchanganya madaraka ya chama na serikali basi n CCM, ambao wanatumia kisingizio kwamba serikali lazima itekeleza sera zao kwa kuwa wao ndio walioko madarakani. Wapinzani wamekuwa wakililalamikia sana hili. Haiwezi kawa wapinzan ndio wanaokosea juu ya hili kwa sababu hawajawahi kuendesha serikali.
Kushindwa kwa upinzani kusimamisha Chama imara chenye mifumo imara ambayo inaheshimika na kuonekana kama mbadala wa CCM ni mojawapo ya sababu kubwa inayowafanya wananchi kuendelea kuiona na kuamini kuwa serikali ndo CCM na CCM ndo serikali.
Wapinzani watawezaje kusimamisha chama chenye nguvu wakati kila siku wako kwenye mpambano dhidi ya kila aina ya mbinu inayofanywa na CCM kuwadhoofisha kwa kutumia vyombo vya dola? Ni kama CCM ina sera rasmi ya kudhoofisha upinzani, kutowapa nafasi hata ya kupumua ili wapoteze muda mwingi kushughulika na mambo mengine badala ya kuimarisha vyama vyao. Kipofu yeyote anaweza kuuona huu mkakati wa CCM, ndani na nje ya Bunge.