Ushauri: VETA au kurudia kidato cha nne?

Ushauri: VETA au kurudia kidato cha nne?

Salaam wa ndg!

Nina kijana wangu wa kiume amemaliza kidato cha mwaka huu ila amepata daraja la 4 points 27, katika shule ya kata kunduchi beach.

kwa kifupi alikuwa anamaendeleo mazuri akiwa shule ya msingi na hadi alipofika kidato cha 2 , kuanzia hapo maendeleo yake yalishuka sana na akawa na utovu wa nidhamu shule na kimasoma ila akiwa nyumbani ni mtoto mtaratibu sana na nidhamu ya hali ya juu.

Sasa ndg zangu wana jamvi naombeni ushauri wenu kwa kijana wangu nimpeleke VETA au arudie kidato cha 4 ili kwamba apate alama za kumpeleka O'LEVEL?

Nimemuuliza kwa jinsi matokeo yalivyokuwa mabaya atafanyaje kujiendeleza? AKAJIBU eti anataka kuwa Polisi.

FUATA ANACHOTAKA, NAFASI YAKO NI KUMSHAURI TU. KAMA ANATAKA U POLISI MPELEKE HUKO HUKO. MDA WA KUMLAZIMISHA AFANYE UNACHOTAKA WEWE UMEPITA. UKIMPELEKA VETA AU KURUDIA KAMA HATAKI HATOSOMA, UTAPOTEZA MDA WAKO NA WAKWAKE.
 
Kama alivyoshauri mdau mmoja hapo juu ni vyema kama anapenda Upolisi itakua vizuri akianzia kwanza veta apate japo ujuzi wa ufundi fulani itakurahisishia pia kupata nafasi ya kuingia jeshini.
 
Back
Top Bottom