Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 421
Hao waoane tuu maana hawafuati dini yayote kwa sababu wameshatungana hadi mimba kuonesha kuwa ni asharati wazoefu.
Wakuu naomba mnichangie mawazo ya kumpatia ushauri muafaka rafiki yangu. Ni hivi, kuna jamaa ni rafiki yangu wa karibu sana (almost ndugu). Tumesaidiana kwa mambo mengi na kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka kama mitatu amekuwa na urafiki na msichana fulani, hatimaye kufikia uamuzi wa kujiweka tayari ili kufunga ndoa. Baada ya kujitambulisha kwenye pande zote mbili za familia, matatizo ndio yameanza kama ifuatavyo;
1. Rafiki yangu na huyo mchumba wake ni wakristo ila madhehebu tofauti; wao wameamua kila mtu abaki na thehebu lake ila ndoa ifungwe kwenye dhehebu la mwanamume. Lakini baba wa huyo binti amekataa katakata anataka ndoa ifungwe kwenye dhehebu la binti yake.
2. Pili, baba wa huyo binti amemtaka rafiki yangu asaini kiapo kuwa watoto wao watabatizwa na kulelewa kiroho kwenye dhehebu la binti yake (ie dhehebu la huyo baba mkwe).
3. Jamaa yangu alimpomweleza huyo binti kuwa masharti hayo ni magumu sana kwake, na hivyo kumtaka binti atoe msimamo wake, binti alimwambia kama itashindikana basi waachane.
4. Kwa sasa binti huyo ni mjamzito wa kama miezi mitano hivi, habari hiyo bado haijamfikia huyo baba mkwe.
Sasa basi, nilipomuuliza rafiki yangu anieleze msimamo wake....alinijibu kuwa mpaka sasa hajui afanye nini. Nilimuomba anipe wiki moja nijaribu kutafakari kwa vile nisingeweza kukurupuka ukizingatia uzito wa suala lenyewe.
Wadau naomba mistari ili niweze kutoa ushauri muafaka
Hapo sijaona udini wala udhehebu. Huyo dogo anataka kuoa mchawi ila hajui tu. Kusaini kiapo cha nini vile??? Hayo ndo madogoli live....welcome to withcraft society...ndo hao wanaogombea maiti.
We chukua mzigo....huyo dingi hafai kusikilizwa..hiyo ndoa haimuhusu kihivyo ..anavuka mipaka sasa ebo!!
Kuandikiana kiapo, huyo Mkwe kazidisha. Wajue kuwa MUNGU ni mmoja na hana dini.. ikibidi Jamaa yako akubali yaishe kwa sababu ameshamjaza! Ila kama ana imani hata wakiandika kiapo ni by the way hakuna litalompata.. Mpe pole sana.
Aangalie sana,la sivyo baba mkwe atakuwa hadi anamuingilia kwenye kuiongoza familia hiyo baada ya ndoa.
huyo baba naye anamatatizo ..kama wote ni wakristo kuna tatizo gani hapo?
na huyo baba hajui maandiko yasemayo mwanamke ataacha wazazi wake na ataambatana na mmewe nao watakuwa mwili mmoja
Swala la watoto ni juu ya Baba na mama kuamua wasali na sio babu yao
kaniuzi huyo baba mkwe ..Binti nae ka msimamo kake kako 50/50% Y
Huu ndio unafiki ninaoupigia kelele kila siku, kuonekana mtakatifu mbele za watu kwa kwenda kanisani kila siku na kupigania dhehebu lako wakati hata Mungu mwenyewe humuogopi.
Hivi dhehebu ndilo linalompeleka mtu peponi? Hapo kwenye mimba ndiyo starting point nzuri! Jamaa yeye akubali tu kufunga ndoa kwenye dhehebu la binti kwa kuwa dhehebu si kitu. Ila hilo la kusaini mkataba ni BIG NO! After all huwezi kuwachagulia watoto dhehebu kabla hawajazaliwa! Vipi baada ya kuzaliwa wakaaamua kubadili dini baada ya kuwa na umri wa miaka 18 na uhuru wa kuchagua wakitakacho huo mkataba utakuwa umesaidia nini?
Inabidi tubadilike na kusoma zaidi kuhusu hizi dini na madhehebu. Ukiwa na uelewa mpana zaidi huwezi kufungwa na madhehebu. Hapa nazungumzia madhehebu ya kawaida, siyo yale yenye mambo ya ajabu ajabu!
huyo baba naye anamatatizo ..kama wote ni wakristo kuna tatizo gani hapo?
na huyo baba hajui maandiko yasemayo mwanamke ataacha wazazi wake na ataambatana na mmewe nao watakuwa mwili mmoja
Swala la watoto ni juu ya Baba na mama kuamua wasali na sio babu yao
kaniuzi huyo baba mkwe ..Binti nae ka msimamo kake kako 50/50% Y
na ndio maana anaonekana ''mtakatifu'' kumbe tayari anakwenda ''nyama kwa nyama''.
Njia rahisi ni kumwambia huyo baba mkwe kwamba binti yake tayari ni mjamzito. Atalainika kama mrenda na ndoa itafungwa chap chap ili afiche aibu ya binti yake huko kanisani kwao!
Hapo sijaona udini wala udhehebu. Huyo dogo anataka kuoa mchawi ila hajui tu. Kusaini kiapo cha nini vile??? Hayo ndo madogoli live....welcome to withcraft society...ndo hao wanaogombea maiti.
We chukua mzigo....huyo dingi hafai kusikilizwa..hiyo ndoa haimuhusu kihivyo ..anavuka mipaka sasa ebo!!
Pamoja na mfumo dume kuwa watoto ni wa baba, jambo ambalo naamini ndio alivyokuzwa huyo rafiki yako. Lakini je, kuna maelezo au sababu zo zote alizotoa binti ni kwanini mzazi wake anataka mambo yawe hivyo? Ndoa ifungwe kwenye dhehebu la binti na watoto wafuate hivyo?
Je, huko nyuma hilo mlilijadili namna gani? Watoto wangekuwa dhehebu gani?
Na binafsi yako utakuwa umepungukiwa nini endapo watoto watakuwa dhehebu la huyo mwenzako?