Prince jr 47
JF-Expert Member
- Aug 19, 2016
- 285
- 246
Habari zenu wana jukwaa hili la MMU na wote nawatakia heri ya Mwaka Mpya wa 2017 ukawe wenye baraka tele kwenu nyote.
Back to the topic,ni hivi mimi ni member wa siku nyingi sana wa humu jf ila nimeamua kutumia hii Id yangu nyingine kuleta hili tatizo kwenu.
Mimi ni kijana wa kiume ninasoma katika chuo kikuu kimoja wapo ndani ya nchi katika mkoa fulani,nilikuwa na girlfriend wangu ambae nimedumu(au kukaa nae) katika mahusiano kwa muda wa takribani mwaka mmoja sasa....
Tatizo lenyewe ni kwamba katika mahusiano yetu tumekuwa tukipendana sana na izingatiwe kuwa mimi ndie niliemtoa usichana wake,juzi kati wakati msimu wa sikukuu unaanza yeye na familia yake waliamua kusafiri kuelekea zanzibar kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu za krismas na mwaka mpya.
Alisafiri yeye,mama yake na mdogo wake wa kike,tatizo kuu ni kwamba tangu aende huko zanzibar amebadilika sana,amekuwa ni mtu ambae hanitafuti kabisa kwa mawasiliano kabisa,sio kama zamani nikimuuliza anasema yupo close na mama yake,nisipomtafuta kwenye simu ndo kabisa yeye hanitafuti wakati sio kawaida yake.
Kabla ya kusafiri nilimpinga sana kuhusu hiyo safari yake lakini yeye alionesha kung'ang'ania sana kwenda.
Tangu aende huko visiwani zanzibar amebadilika sana sio yule niliemjua mimi,nimemtafuta kwenye simu na kumueleza lakini ananijibu niache kulalamika yeye yupo kawaida tu,mimi hapa nilipo nina wasiwasi yawezekana kuna mtu anaemega tunda langu huko aliko na izingatiwe kwamba mpaka leo hawajarudi na huko waliko hawana ndugu hata wa kusingiziwa...maisha yao ni hotelini tu bas!
Please naombeni mnipe ushauri wakuu ninapatwa na hisia mbaya yawezekana ameshaanzishiwa ule mchezo mbaya wa 0713 ndo maana ananidharau na kuniona sifai,anasema kama vipi tuachane na sio kuanza kumfwatilia fwatilia,inaniuma sana kwa sababu ndio mwanamke wa pekee niliempenda na kuamua kutulia nae,na pia nina malengo nae.
Karibuni kwa ushauri,samahani kwa maelezo marefu na uandishi wangu mbovu.