Ushauri unahitajika, nitaepukaje hili?

Ushauri unahitajika, nitaepukaje hili?

Samboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2011
Posts
5,421
Reaction score
7,877
Habari zenu wana jamvi.

Kuna mwanamke tuliwahi kuwa wapenzi miaka 8 iliyopita, tulipendana sana kipindi hicho ila alikuja kuolewa na mwanamme mwingine ambae alikua anamtaka tangu tukiwa wote na alifanikiwa kumuoa baada ya wazazi wake kuwa wakali wakimwambia kwanini alikua hataki kuolewa na huyo jamaa maana jamaa alipeleka barua kwao binti alipokataa wakamwambia tunajua upo kwenye mahusiano na mtu fulani kwanini asije kujitambulisha? kama ana nia nzuri nawe?, mama yake alikua anajua natoka na bintie.

Sasa wakati hilo sekeseke likiendelea nkapata safari nikaenda Dom kibiashara sisi tulikua tupo Dar, ilinichukua miezi mitatu kurejea Dar nikakuta demu wangu kishaolewa na jamaa, demu akadai ilibidi akubali baada ya baadhi ya marafiki zangu kumwambia nimeenda kuoa na kipindi hicho si mimi wala yeye aliekua na simu na nilipokua mimi kulikua hamna mawasiliano kabisa ya simu.

Baada ya hapo ikapita miaka minne bila kuonana, siku moja nipo kwa rafiki yangu kuna kazi nilikua naifanya geto kwake, alipokutana na rafiki yangu akamwambia nipo kwake akaja pale kwa rafiki yangu tukawa tunapiga stori za hapa na pale nikajikuta hisia zinapanda juu yake lkn sikumwambia, kumbe nae amekutwa na hali kama yangu akaniambia nimekuona nimeishiwa nguvu kabisa na siwezi kuondoka hivihivi aidha tumalizane hapa kwa rafiki yako au twende gesti, tukajikuta tumevunja amri ya sita palepale.

Ikabidi nimkatie mawasiliano kwa sababu niliona tungeishia pabaya. Ila kila nikimuona nashinkwa na msisimko wa hali ya juu nae ni hivyohivyo.
Kilichonifanya niombe ushauri, wamehamia karibu na ninapoishi na familia yangu na anadai nimekua namkwepa ila sasa hivi amehamia karibu atanifata hadi home kama ntamkimbia tena.

Sio kwamba siwezi kumpotezea ila tunapokutana tuu naishiwa nguvu kama yeye.

Naombeni ushauri wa kufanya ili hali hii isinikute tena maana sipendi kumsaliti mke wangu, maana kila tukionana na huyu mwanamke tunakua na hisia za hali ya juu sana.

Ushauri tafadhali.
 
Mwanamme na familia yako usijue cha kufanya ili kuilinda ndoa yako? Wewe na yeye it wasnt meant to be so fungeni chapter
 
Wanawake ni wengi,
jali Mkeo kwani shamba ni lilelile na kulima ni hukohuko kutifua udongo na kupanda
wasiwasi wangu MTA-JAFUMWA NA KIBOGA KITATEMBEA
MKE WA MTU SUMU
 
wote wawili ni malaya mliokubuhu...sina ushauri kwa wahuni wasioheshimu ndoa
 
Ngono zembe ni hatari 'MKE WA MTU SUMU' subiri ukitembezwa uchi mtaa mzima kwa kuchepuka na mke wa mtu ndo uje uombe ushauri.
 
wote wawili ni malaya mliokubuhu...sina ushauri kwa wahuni wasioheshimu ndoa

Ni maoni yako ila sijasema km tunafanya ila ni siku ile tuu lkn kinachotokea tunapoonana ni kila mmoja kusisimka kimapenzi kwa hali ya juu sana, shida ndio ipo hapo,
 
Mmh hama tu hapo kama unaweza. Hiyo misisimko yenu itawapeleka pabaya. Mlishaachana ya nini kutamaniana?? Mshindeni shetani

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mwanamme na familia yako usijue cha kufanya ili kuilinda ndoa yako? Wewe na yeye it wasnt meant to be so fungeni chapter

Nimekuja hapa nipate mbinu zaidi za kulinda ndoa yangu na sio kwamba nataka niwe nae istoshe ana mme wake pia ishu ni tukionana tuu ni kosa tunajikuta tunatamaniana sana hata kama upite mda gani hali inakua hiyohiyo.
 
kwel kila siku kuna jipya mmu...wewe umeoa na yeye ameolewa lakini mkionana mnaishiwa nguvu hahahahahahhahahaaa tafuteni Energizers ili msiwe mnaishiwa nguvu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom