FredKavishe
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,090
- 318
KUFUFUA ATCL USHAURI WANGU:
Serikali ya awamu ya tano imeiamua kununua ndege kufufua shirika letu la ATCL ambalo lilikuwa mfu.Zimekuja ndege mbili kuna nyingine zinazidi kuja nazipongeza hizi juhudi za wazi kufufua shirika letu la ndege,hata tukiangalia Ilani za vyama 2015 nyingi ziliongelea jitihada za kufufua shirika letu la ndege.
Kuna hoja zimezuka sasa kuhusu hizi terrible teens ndege ambazo zinasemekana tumeagiza,sitacomment kuhusu hiyo hoja ya terrible teens.Hoja yangu itajikita jinsi ya kuendesha hili shirika kwa faida tusipate hasara tena.Ndege zinazokuja zina lengo za kutoka direct from USA to Tanzania,hapa ndo naona tatizo la hizi ndege kupata hasara kubwa sana,kwa sababu zifuatazo
1:Msimu wa watalii wengi ni mwezi wa 6,7,8,9 katika mwaka miezi mingine tuna watalii wachache je miezi hiyo tutajiendeshaje?
2:watalii sio wote wanatokea Marekani ni asilimia ndogo tu ambayo haiwezi kufika 50% ya watalii wote
3:Shirika la KLM linaleta ndege zake kwa week moja wanakuja mara 5 Tanzania itakua ngumu kuchukua soko lao
4:Bei ya Ndege ya kimataifa inakadiriwa itakua zaidi ya usd 224 kwa Tsh ni zaidi ya Bilioni 500 ambazo ni nyingi
5:Sisi ni wageni kimataifa itachukua muda kuweza kushindana na mashirika kama Kenya Airways,Ethiopian Airline.
TUFANYAJE KUWEZA KUTENGENEZA FAIDA NA ATCL NA KUINUA UCHUMI:
Nashauri tununue Ndege za Mizigo ikiwa kweli tuna nia ya kuinua uchumi na kuendesha shirika kwa faida nashauri tuagizie ndege za mizigo kwa pesa ambayo tungenunua ndege moja ya abiria tunapata ndege mbili za mizigo.Ndege moja ya mizigo inauzwa kuanzia usd Million 100-150 kwa fedha za kununulia hizi za abiria tunapata ndege mbili za mizigo ambazo zina uwezo wa kubeba tones 150 kwa safari moja.
KWANINI NDEGE ZA MIZIGO:
1:KILIMO
Tanzania inauza chakula kwenye nchi nyingi za Ulaya (Germany,Nethland,UK nk).Vyakula vinavyouza ni kama Njegere,Carrot,Maharage Machaga,Ndizi,Black Passasion nk.Ukiacha hiki Arusha na Kilimanjaro ni wakulima wazuri wa Kilimo cha Maua kinachoenda sana Uholanzi.Tatizo kwenye sekta hii hakuna Cargo Planes,Mizigo mingi husafirishwa kupitia Kenya kwenda kupakiwa kwenye Ndege kwenye Ulaya,Uarabuni,Marekani.
Shirika la Ndege KLM linakuja mara tano kwa week sio kuleta abiria bali kubeba mizigo ambapo wakitua KIA hepakia Tonnes 10 za vyakula au maua kupeleka nje.Wafanya biashara,wakulima wa kupeleka haya mazao nje na Maua wanasema wanasoko kubwa sana tatizo hawana Cargo Planes na ukipitishia Kenya ni gharama kuliko ukiwa na ndege direct kutoka kwenye uzalishaji mpaka kwa walaji.
Kwahiyo kuna soko kubwa sana la kubeba mizigo kwenda Ulaya kama hivyo chakula ambavyo vinahitajika vifike ulaya viwe fresh havijaribika kuhifadhiwa kwenye Cold room etc.
Lakini serikali ikiwahakikishia hawa wakulima na wafanyabiashara kitaleta tija kwenye sekta la Kilimo ambayo ndio asilimia 80 ya watanzania wanaitegemea itapelekea Company kama Fresh Green kulima zaidi kwa kutumia wakulima wadogo ili mwakani waweze kusafirisha zaidi chakula nje,kwa maana soko lipo kubwa.
Hii itatengeza Ajira,Kilimo chenye Tija,Masoko ya Nje Zaidi kwa taarifa Kenya huingiza zaidi ya Trilion 6 Tsh kwa mwaka kutokana na mauzo ya chakula cha nje.
2.KUTAWALA UKANDA WETU WA AFRICA MASHARIKI KWENYE KUBEBA MIZIGO
Ndege ikipeleka Mzigo nje kurudi haitarudi tupu kuna mizigo mingi inaagizwa kutoka mataifa mbalimbali kama Nguo,Magari ambayo ndege inaweza kurudi nayo kusafirisha gari moja saloon kutoka Japan ni Usd 1500 Gari hili lina uzito wa tani 2-1.5.kwa trip moja ya kurudi Ndege inaweza ikabeba hadi Magari 50 ambayo ni zaidi ya Usd 75000,bado kuna mizigo ya Afrika Mashariki inaweza ibebwa kwa ndege kwa unafuu zaidi kama Nguo nk.
Kwahiyo kuwekeza kwenye biashara ya kubeba mizigo hakuta letea hasara shirika wakati huo shirika likisoma soko la Abiria wa kawaida kuinua Utalii,Kama tulivyoona huko juu tayari kuna mashirika yanaleta Watalii hapa Nyumbani kuwapelekea shirika kule wakati wana kipindi cha miezi minne ndo wanakuja kwa wingi kutapeleka shirika kufa haraka.
Tatizo la kupata Watalii sio ndege tatizo letu hatujajitangaza sasa tunapokea watalii kama 1.5 m kwa mwaka na wote sio kwamba wanatoka Marekani.
Kuna watu watasema chakula chenyewe tunashindwa kujilima cha nje tutaweza,Serikali lazima iamue Kilimo kifanyike kwa Sayansi na Teknolojia tusilime kimazoea tena tulime kwa njia bora zenye tija tuzalishe zaidi.
Muhimu tuangalie uwekezaji upi una tija wa Mizigo ama Abiria.
KUHUSU RELI:
Naunga mkono juhudi za Serikali kujenga reli ya kati kiwango cha Standard Gauge,ni wazi hatuna kiasi cha kufikisha Reli kutoka Dar-Moro-Dom-Singida-Tabora-shinyanga-Mwanza-Kigoma ambayo itaunganisha nchi za Congo,Rwanda,Burundi,Uganda.Ujenzi huu ukadiriwa kuhitaji zaidi ya Trilion 17 kukamilika ni wazi ni pesa nyingi hatuwezi kuwa nazo ningeshauri yafuatayo…
1:Serikali ishirikishe Sekta Binafsi
Ni wazi ujenzi huu utaathiri uwekezaji waliofanya watanzania wenzetu kwenye sekta ya malori(kubeba mizigo) na Mabus ya kubeba abiria kutokana na Treni kubeba mizigo mingi na kuwahi kufika.Hivyo kuna lengo la serikali kukaa na sekta binafsi kuangalia inaweza kufanikisha ujenzi huu nashauri serikali wajenge Reli lakini uendeshaji tuwape sekta Binafsi wanunue mabehewa ya Abiria,na ya Mizigo.Uwezo wa kuwekeza wanao tuwape nafasi.
Kwakua sasa tunapata ukakasi wa wapi pa kupata pesa za kujenga Reli ni muhimu sekta Binafsi ikashirikishwa kununua Hisa za kusaidia huu ujenzi wa reli baadaye hizi dhamana zao zitabadilishwa kuingia kwenye uendeshaji wa reli.
Kwa thamini ya haraka ni zaidi ya Malori 20000 yatapata mtikisiko uwekezaji huu wa reli ukikamilika ukipiga hesabu kwa milioni 200 kwa roli moja unapata zaidi ya Trilioni 4 ambazo zinawezwa zikaingiza na sekta binafsi kufanya huu uwekezaji wa Reli ya kati ukafanikiwa vizuri najua kwa makusanyo yetu ndani ya miaka 5 ijayo hatuwezi kukosa zaidi ya Trilioni 10 tsh kutoka serikali kuu kuhusu ujenzi huu wa reli.
Reli ni muhimu kwa sababu mizigo itabebwa kwa usalama,unafuu,haraka kufika eneo husika pia itapelekea serikali kukusanya mapato zaidi hii kuinua uchumi,kupunguza mfumuko wa bei kwa upande mwingine.
Tusupport jitihada za serikali kujenga Reli ya kati na wakati huo huo tuwakumbushe kuwashirikisha sekta binafsi kwa sababu ni wahanga no moja reli hii ikikamilika.
Fred Kavishe